Ni heshima kubwa kusimama karibu na Mama yetu mpendwa, Mh. @salma_kikwete
Asante kwa moyo wako wa upendo, unyenyekevu na kujitoa kwa jamii. Umeendelea kuwa taa ya matumaini na mfano wa kuigwa kwa wengi. Mwenyezi Mungu akupe afya njema na azidi kukuongoza katika kila hatua 🤲
Mwenyezi Mungu alitujalia moyo wa upendo 🤍
Hakika kidogo tulichopata tulijitahidi kuwapa furaha wale wenye uhitaji.
Nakumbuka tulipotembelea kituo cha watoto yatima Goba… siku hiyo haikuwa tu ya kutoa, bali ilikuwa ya kujifunza. Tulijifunza kuwa furaha ya kweli haipo kwenye wingi wa ulicho nacho, bali kwenye uwezo wa kushirikiana na kugusa maisha ya wengine.
Tabasamu lao lilitufundisha maana halisi ya shukrani 🙏
Na mioyo yao ilitukumbusha kuwa kutoa ni baraka, si kupungua.
Tuendelee kusaidiana pale tunapoweza 🤝
Kwa sababu kidogo chako kinaweza kuwa kila kitu kwa mtu mwingine.
.
.
.
#TBT #ThrowbackThursday #TBTMoments #Memories #flashback
SpreadingLove| HelpingHands|CharityLife|GiveBack|
Upendo Baraka❤️| KutoaNiBaraka| Goba DarEsSalaam
Ni vyema kama kijana kupata muda kuiangalia hii podcast kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa @dr_ibrachenza ambayo yanaweza kukuonesha umetoka wapi na upo wap na unaenda wap katika maisha kiufupi kuna mengi sana yamezungumziwa humo.
Shukran br @amrisaly kwa kutusogezea madini sisi vijana.🤝
#podcast
CHELEWA UKIWA NA LENGO BORA KULIKO KUKIMBIA BILA MWELEKEO.. MAFANIKIO SI MBIO, NI MWENDO WA UHAKIKA NA MAAMUZI SAHIHI.
#motivation
#inspiration
#tanzania
#weddingphotographer
#repost from @sheikh_suleimantz .... Soma caption👇👇
Huyu ni mtoto Issa kutoka nchini Iraq 🇮🇶, mwenye umri wa miaka 11. Anasumbuliwa na maradhi yaliyosababisha kupotea kabisa kwa muonekano wake wa awali, hali ambayo imeendelea kubadilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
Alhamdulillah, sisi kama Zanhelp Association tumefanikiwa kuchangia katika juhudi za matibabu ya mtoto Issa. Hii imewezekana kwa ushirikiano wenu nyote mnaotuunga mkono katika harakati zetu mbalimbali za kusaidia jamii zenye uhitaji.
Muda wowote kuanzia sasa, mtoto Issa atasafiri kuelekea India kwa ajili ya matibabu zaidi, baada ya kukamilika kwa kiwango cha fedha kinachohitajika kwa matibabu yake.
Tumuombee dua 🙌 Allah amfanyie wepesi katika matibabu yake na amrejeshee afya njema.
AMEEEN.
Alhamdulillah tumepata ushindi dhidi ya mtani 🐸 hakika huu ushindi umerudisha heshima na kujiamini kwa wachezaji hata mashabiki wa simba.
Credit ✅️ kwa Refa wa mchezo amejuwa nini maana ya debi hakika amechezesha mchezo vizuri sana.
Credit ✅️ kwa wachezaji wote kwa kucheza vizuri sana.
Credit ✅️ kwa benchi la ufundi hakika wamekisuka vyema kikosi.
Tukutane May 3 jumapili. 🇹🇿
#simba #mapinduzicup #tanzania #zanzibar
Alhamdulillah 🤲 weekend hii ilikuwa ya kipekee sana tulikusanyika na watoto wetu katika dua, tukashirikiana kwa upendo na chakula. Hakika baraka zilikuwepo pale palipokusanyika mioyo safi ❤️
#dua #tanzania #instagram
Mpende sana mama yako… ❤️
Hakika radhi yake ni njia ya baraka zako.
Pepo ipo chini ya nyayo zake,
na ukimheshimu kwa dhati, maisha yako yatafunguka kwa namna usiyotegemea.
Na kama ameshatangulia mbele ya haki,
usimuache… muombee dua, mfanyie mema kwa niaba yake 🤲
Kumbuka hili:
Huwezi kujenga ndoa yenye amani na baraka,
kama hukujifunza kuthamini chanzo chako — mama yako.
Mpende akiwa hai,
na akiondoka… endelea kumpenda kwa dua. ✨
#Mama #Heshima #Baraka #Maisha #Ndoa