1 month ago
Mwenyezi Mungu alitujalia moyo wa upendo 🤍
Hakika kidogo tulichopata tulijitahidi kuwapa furaha wale wenye uhitaji.
Nakumbuka tulipotembelea kituo cha watoto yatima Goba… siku hiyo haikuwa tu ya kutoa, bali ilikuwa ya kujifunza. Tulijifunza kuwa furaha ya kweli haipo kwenye wingi wa ulicho nacho, bali kwenye uwezo wa kushirikiana na kugusa maisha ya wengine.
Tabasamu lao lilitufundisha maana halisi ya shukrani 🙏
Na mioyo yao ilitukumbusha kuwa kutoa ni baraka, si kupungua.
Tuendelee kusaidiana pale tunapoweza 🤝
Kwa sababu kidogo chako kinaweza kuwa kila kitu kwa mtu mwingine.
.
.
.
#TBT #ThrowbackThursday #TBTMoments #Memories #flashback
SpreadingLove| HelpingHands|CharityLife|GiveBack|
Upendo Baraka❤️| KutoaNiBaraka| Goba DarEsSalaam
6
0