Home tenmetPosts

Tanzania Education Network

@tenmet

🇹🇿 Mtandao wa Elimu Tanzania 🗣 #MiakaMitanoKufikiaMalengoEndelevu
Followers
5,482
Following
365
Account Insight
Score
32.22%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
15:1
Weeks posts
Strengthening education systems requires strong partnerships, sustained investment, and a shared commitment to ensuring that every child has the opportunity to learn, thrive, and reach their full potential. TEN/MET was honored to engage with Morten Sigsgaard and Mohamed Sabul from Global Partnership for Education (GPE) in a meaningful discussion on advancing education transformation in Tanzania. Through support from GPE under the Education Out Loud (EOL) initiative, TEN/MET has continued to champion innovative, community-driven interventions that are improving access to inclusive, equitable, and quality education for children across Tanzania. The partnership has contributed to stronger citizen engagement, increased accountability in education financing, and amplified voices of communities and civil society in shaping education reforms. As Tanzania advances major education sector reforms, including the implementation of the improved curriculum and the revised Education and Training Policy, sustained and increased investment in education remains more important than ever. While notable progress has been achieved, significant gaps still persist particularly in equitable access to learning, teacher support, learning environments, gender-responsive education, and reaching the most marginalized children and young people. Continued financing and strategic collaboration are critical to ensure that no learner is left behind. We commend GPE’s global commitment to supporting countries in strengthening resilient and inclusive education systems and financing transformative solutions that are helping nearly 750 million children across 96 countries access better education opportunities. Partnerships of this scale and vision are essential in accelerating progress toward quality education for all and building education systems that can respond to the evolving needs of learners and communities. #qualityeducationforall @wizara_elimutanzania @tamisemi @gpe.nordics @gpe.canada @ikulu_mawasiliano @gce_us @kinderdorfpestalozzi
54 1
3 days ago
Ikiwa ni muendelezo wa juhudi za kutoa elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi, @tenmet kwa kushirikiana na mwanachama wetu Faraja Human Development Tanzania ( @farajahdtz ), tumefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ili kuongeza uelewa wa jamii kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi, namna ya kukabiliana nazo pamoja na fursa zinazoweza kuinua maisha ya wananchi kiuchumi na kijamii. Tunaamini kuwa elimu na ushirikishwaji wa jamii ni msingi muhimu wa kujenga ustahimilivu na kulinda mazingira kwa maendeleo endelevu. @vpotanzania #TENMET #ClimateAction #ClimateEducation #ElimuYaTabianchi #UtunzajiMazingira
35 0
4 days ago
Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) is inviting qualified and experienced candidates to apply for the position of Project Officer (2 Positions) to support the implementation, coordination, monitoring and reporting of education projects aimed at strengthening teacher motivation and improving education outcomes in Tanzania. Location: Dar es Salaam Contract Duration: One year (Renewable based on performance) Application Deadline: 17th May 2026 Submit your application to: [email protected] Cc: [email protected] Subject line: Application for Project Officer Only shortlisted candidates will be contacted. #TENMET
285 2
7 days ago
Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) is inviting qualified and experienced consultants or firms to conduct a Research Study on the Level of Community Awareness on the Re-entry Agenda aimed at generating evidence to inform advocacy strategies, identify knowledge gaps and support targeted interventions for the reintegration of young mothers into the education system. Deadline: 17th May 2026 Submission: Send your application to [email protected] Cc: [email protected] Subject line: Consultancy Service to Conduct Research Study on the Level of Community Awareness on Re-entry Agenda Only shortlisted candidates will be contacted. #TENMET
108 2
7 days ago
Leo, Mei 07, 2026, @tenmet tumepata fursa ya kushiriki kikao cha Bunge jijini Dodoma kikao muhimu sana kwa sekta ya elimu nchini, ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf F. Mkenda (Mb), amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2026/27 ya wizara hiyo. 📚✨ Katika hotuba hiyo ya bajeti iliyoongozwa na kauli mbiu ya “Uwekezaji katika Elimu na Ujuzi, Sayansi na Teknolojia kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi na Shindani”, Prof. Mkenda amesema kuwa lengo ni kuwa na Mtanzania aliyeelimika, mwenye maarifa, stadi na mtazamo chanya utakaomwezesha kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa. Aidha, ili kuwezesha utekelezaji wa malengo yaliyoanishwa kwa mwaka wa fedha 2026/27, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,394,423,829,000.00. Moja ya vipaumbele vya wizara ni kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya awali, msingi, sekondari pamoja na ualimu nchini. 🙌🏽 @tenmet tunapongeza hatua hii muhimu katika kuendelea kuimarisha sekta ya elimu nchini, hususan jitihada za @wizara_elimutanzania kuandaa Kiunzi cha Kitaifa cha Uboreshaji wa Vituo vya Walimu (Teacher Resource Centers – TRC) ili vitumike kama kumbi za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) pamoja na Teknolojia za Kidijitali (DigiSTEM Hubs).💡 TEN/MET tutaendelea kuunga mkono jitihada hizi katika kuhakikisha uwepo wa elimu bora, jumuishi na inayomwandaa Mtanzania wa sasa na wa baadaye. 🌍 📖 #ElimuBora #STEM #DigiSTEM #TENMET #Bajeti2026_27 ElimuKwaMaendeleo @campaignforeducation @wizara_elimutanzania @ikulu_mawasiliano @tamisemi
47 0
10 days ago
TEN/MET inawatakia Mtihani mwema wanafunzi wote wa kidato cha sita. #NECTA #Exams
14 0
13 days ago
TEN/MET Secretariat extends it’s heartfelt appreciation to all partners, stakeholders and participants who made #GAWE2026 in Songwe a powerful and impactful success. Your commitment, collaboration and shared vision truly brought this year’s theme to life. The TZS 53 million contribution for leaving a mark by improving infrastructure and granting access to education for children with disabilities is not just a milestone, but a reflection of what is possible when we invest together in domestic solutions for inclusive and quality education. Thank you for being part of this journey, your support is shaping lasting change and together we continue moving forward. #GAWE2026 #DomesticResourceMobilization Cc: @wizara_elimutanzania @tamisemi @ikulu_mawasiliano @wizara_afyatz @mandeleoyajamii @urtmof @campaignforeducation @ubongoimpact @beyond_inclusion24 @wizara_elimutanzania @tamisemi @shuledirect @bracmaendeleo @camfed @tai_impact @plan_tanzania @roomtoread_tz @officialktotz @actionaidtz @righttoplayintl @momba_dc @mkoa_wa_songwe @sematanzania @shivyawata @mtwangonet
55 0
13 days ago
Happy Workers Day to all Workers ✊🏾📚!! Your dedication, hard work and daily contributions continue to drive progress, strengthen communities and build a brighter future for all. #TENMET #labourday #workers #meimosi
22 0
17 days ago
TENMET KUACHA ALAMA MOMBA KWA KUCHANGIA UJENZI, MADAWATI NA VITI MWENDO KWA JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 53. Awali katika sherehe za kufunga Juma la Elimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa ELimu TEN/MET Bw. Simon Nanyaro kwa niaba ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) aliiomba serikali kuchukua kupitia wizara za kisekta kutenga bajeti ya kujenga karakana itakayo ongeza ufanisi katika utekelezaji wa masomo ya amali pamoja na kuajiri walimu wa amali na dereva katika shule ya sekondari Msangano ili kusaidia ufanisi katika ujifunzaji wa matumizi ya vyombo vya amali, ambapo suala la dereva lilitatuliwa papo hapo. Mwenyekiti wa Bodi ya TENMET Bw. Simon Nanyaro amesema, “katika ziara yetu ya siku tatu, tumeshuhudia juhudi za serikali kupitia program za IPOSA, MEMKWA, Amali, Elimu Masafa pamoja na mpango wa chakula na lishe shuleni na kurejesha shuleni Watoto waliokatiza masomo kwasababu mbalimbali (Re-entry). Pamoja na changamoto tulizoziona, kuna mengi mazuri ya kujivunia basi nasi tuiopongeze serikali kwa hatua tuliyofikia, baada ya kusema hayo, napenda kutumia fursa hii kuwajulisha kuwa Sekretarieti ya Mtandao wa Elimu Tanzania, kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu katika Mkoa wa Songwe, hususan Wilaya ya Momba, kama ilivyoainishwa hapo awali, tutachangia kiasi cha shilingi Millioni 53,250,000 ikiwa ni mchango wetu katika kutatua baadhi ya changamoto hizi ili kuboresha mazingira shuleni”. Uwekezaji huu umewafurahisha sana wana Momba, akizungumizia hatua hii iliyichukulia na TEN/MET Bi. Neema Ngungulu (mzazi) amesema kuwa, amefurahishwa sana kwa juma la Elimu kufanyika katika kata yao ya Nkangamo, Kijiji cha Chiwanda huku akisisitiza kuwa uwekezaji uliofanywa na Mtandao wa Elimu (TEN/MET) ni mkubwa kuliko walivyotarajia na kwamba utasaidia kuboresha elimu ya Watoto wao kijijini hapo. Cc: @wizara_elimutanzania @tamisemi @ikulu_mawasiliano @wizara_afyatz @mandeleoyajamii @urtmof @campaignforeducation @ubongoimpact @beyond_inclusion24 @wizara_elimutanzania @tamisemi @shuledirect @bracmaendeleo @camfed @tai_impact @plan_tanzania @roomtoread_tz @officialktotz @vipamarurukwa @righttoplayintl @tai_impact
32 0
23 days ago
KAIMU KATIBU MKUU, NA MKURUGENZI WA UTHIBITI UBORA WA SHULE, WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA DKT. EPHRAHIM SIMBEYE, ATOA WITO KWA WADAU WA ELIMU NA WAZAZI KUIMARISHA USIMAMIZI NA UWAJIBIKAJI ILI KUWAWEZESHA WANAFUNZI KUKAMILISHA MZUNGUKO WA MASOMO MOMBA. Katika hotuba yake ya kufunga Juma le elimu mkoani songwe, Dkt Ephrahim Simbeye, akimuwakilisha Katibu Mkuu wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia amewataka wadau wa elimu kuimarisha uwajibikaji hasa wazazi kwa kushiriki kikamilifu katika elimu ya watoto kwa kuhakikisha wanawaandikisha na kuwasimamia kukamilisha mzunguko wao wa masomo. Pia ameitaka sekta binafsi kuwekeza katika elimu na AZAKI kuendelea kuhamasisha mabadiliko ya kijamii akisema kuwa jitihada hizi zitakua ni zao la taifa lililo na raslimali bora na lenye maendeleo. Aidha, Dkt. Simbeye amesema kuwa wakati wa ziara zilizofanyika na wadau shuleni, tumeona mambo mbalimbali mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akisisitiza namna midahalo ya kijamii, na majadiliano ya wadau, yalivyochangia katika kuongeza uelewa wa kina kuhusu hali halisi ya elimu katika Wilaya ya Momba na Mkoa wa Songwe kwa ujumla. Pia uamuzi wa Dkt Simbeye kutatua changamoto ya dereva katika shule ya sekondari ya Amali Msangano umewafurahisha wadau, waalimu na hasa wanafunzi wa shule hiyo kwani ameagiza dereva apelekwe shuleni hapo mara haraka iwezekanavyo ili kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa urahisi Zaidi matumizi ya vifaa hivyo vya amali. Cc: @wizara_elimutanzania @tamisemi @ikulu_mawasiliano @wizara_afyatz @mandeleoyajamii @urtmof @campaignforeducation @ubongoimpact @beyond_inclusion24 @wizara_elimutanzania @tamisemi @shuledirect @bracmaendeleo @camfed @tai_impact @plan_tanzania @roomtoread_tz @officialktotz @vipamarurukwa @righttoplayintl
60 1
23 days ago
KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, NA MKURUGENZI IDARA YA UTHIBITI UBORA WA SHULE, DR. EPHRAHIM SIMBEYE AHITIMISHA JUMA LA ELIMU MKOANI SONGWE. TENMET imehitimisha rasmi maadhimisho ya Juma la Elimu (#GAWE2026) tarehe 24 April 2o26, kwa kuchangia jumla ya shilingi Mil 53 za Kitanzania katika kuboresha miundombinu ya ujifunzaji na kufundishia pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa shule tatu mkoani Songwe, wilaya ya Momba. Akihitimisha rasmi Juma la ELimu, mgeni rasmi, Kaimu Katibu Mkuu Wizara Ya Elimu Sayansi Na Teknolojia na Mkurugenzi Idara ya Uthibiti Ubora Wa Shule, Dr. Ephrahim Simbeye ameipongeza TEN/MET kwa kuratibu kwa mafanikio makubwa maadhimisho ya Juma la Elimu pamoja na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, uongozi wa Mkoa wa Songwe, na wadau wote waliofanikisha utekelezaji wa shughuli za Juma la Elimu. Dkt. Simbeye amesisitiza kuwa juma la elimu, #GAWE2026 limekuja katika wakati muhimu sana ambapo sekta ya elimu inahitaji mjadala wa kina kuhusu uendelevu wa ufadhili wa elimu kutokana na changamoto ya hivi karibuni, ya kupungua kwa misaada ya maendeleo katika sekta ya elimu. “Agenda hii ya ugemaji wa rasilimali za ndani kwa ajili ya elimu inajibu umuhimu wa Serikali kuendelea kutenga fedha ili kukamilisha miundombinu ya shule na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wote wanapata haki yao ya msingi ya kupata elimu. Aidha serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote ikiwemo Mtandao wa Elimu Tanzania katika kuboresha utoaji wa elimu nchini”, amesema Dkt. Simbeye. Cc: @wizara_elimutanzania @tamisemi @ikulu_mawasiliano @wizara_afyatz @mandeleoyajamii @urtmof @campaignforeducation @ubongoimpact @beyond_inclusion24 @wizara_elimutanzania @tamisemi @shuledirect @bracmaendeleo @camfed @tai_impact @plan_tanzania @roomtoread_tz @officialktotz
34 0
23 days ago
TEN/MET YATEMBELEA SHULE YA MSINGI NDALAMBO KUJIONEA MPANGO WA ELIMU CHANGAMANI KWA VIJANA WALIO NJE YA SHULE (IPOSA) NA ELIMU JUMUISHI #GAWE2026 Leo April 23, 2026, katika maadhimisho ya Juma la Elimu wilayani Momba, wadau wa elimu wametembelea Shule ya Msingi Elimu Maalumu na kituo cha IPOSA Ndalambo iliyoanzishwa mwaka 1959. Shule hii imeonesha mafanikio makubwa katika kurejesha matumaini kwa vijana waliokua wamekata tamaa kwa kuwapa fursa ya kupata ujuzi kupitia IPOSA, upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wote, uwepo wa bustani ya mboga mboga na kitalu cha bustani ya miti. Kupitia kituo cha elimu changamani kwa vijana walioko nje ya shule, vijana wanajufunza fani zifuatazo ushoni, uselemala, uashi,uchomeleaji, upishi na elimu ya ujasiriamali. Shule ya Ndalambo pia ina jumla ya wanafunzi 52 wa elimu maalumu/jumuishi. Akizungumzumza na ugeni wa TEN/MET, Mhe Diwani, Samuel Kilanga ameeleza kuwa licha ya juhudi za serikali na wadau kuwezesha shule hiyo, shule inakabiliwa na changamoto zikiwemo upungufu wa madarasa, vyoo, walimu wa elimu maalumu na miundombinu mingine muhimu, huku akiomba wadau waendelee kuwekeza ili kutatua changamoto hizi. Awali, mwalimu mkuu wa shule alibainisha mafanikio ikiwa ni pamoja na, kurejesha wanafunzi waliokatisha masomo hususan mabinti, pamoja na kuongeza mwamko wa jamii kuchangia elimu ambapo kwa miaka minne wamekua wakijenga madarasa ambayo yanahitaji nguvu Zaidi ili kukamika. Mkurugenzi wa TENMET Bi. Martha Makala, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau katika kuboresha elimu jumuishi, akieleza kuwa #GAWE2026 ni fursa ya kujadili na kupata suluhisho endelevu kwa changamoto zilizobainishwa. @wizara_elimutanzania @tamisemi @ikulu_mawasiliano @wizara_afyatz @maendeleoyajamii @urtmof @campaignforeducation @ubongoimpact @beyond_inclusion24 @wizara_elimutanzania @tamisemi @shuledirect @bracmaendeleo @camfed @tai_impact @plan_tanzania @roomtoread_tz @officialktotz
68 4
25 days ago