INFOCUS HATUWADAI PICHA, AKILI ALUMNI MARATHON
Msimu wa kwanza wa Akili Alumni Marathon 2026 ulikuwa na changamoto zake za hapa na pale, lakini kwenye suala la picha na video za tukio zima, kampuni ya
@infocusstudio.tz imefanya kazi ya kiwango cha juu kuliko maelezo.
Wamehakikisha kila mwanariadha anapata kumbukumbu yake, kila hatua muhimu ya marathon inanasa vizuri, na tukio lote linapata hadhi, uzito, na heshima inayostahili. Kwa kweli, wameibeba taswira ya Akili Alumni Marathon kwa ustadi mkubwa sana.
Jambo la kipekee zaidi ni kwamba Mkurugenzi wa InFocus, Joshua Moshi, mwenyewe alihakikisha anafika kwenye tukio ili kusimamia kazi ifanyike kwa weledi, umakini, na ubora mkubwa.
Hilo peke yake linaonyesha namna gani waliichukulia event hii kwa seriousness ya hali ya juu.
Pichani Joshua Moshi anaonekana akiwa nyuma ya Mgeni wetu wa Heshima, Mhe. Asma Mwinyi, pamoja na wageni wengine, ishara kwamba hakuwa mbali na tukio, bali alikuwa katikati ya kuhakikisha kila kitu kinanaswa kama kinavyostahili.
Tunapenda kuwashukuru sana InFocus na hasa Joshua Moshi kwa professionalism yao, kujitoa kwao, na namna walivyohakikisha hakuna moment muhimu inapotea. Kwa yeyote mwenye tukio lolote iwe ni event, uzinduzi, harusi, conference, birthday, au shughuli yoyote muhimu, tunawa-recommend InFocus kwa moyo wote.
Wana uwezo wa kubeba tukio lako lote kwa ubora wa hali ya juu mpaka hata wewe mwenyewe ushangae matokeo yake.
Asanteni sana InFocus. Asante sana Joshua Moshi.
Mmeacha kumbukumbu za mwaka wa mbele kwenye Akili Alumni Marathon.
Swipe kuona picha za mwaka wa mbele.
@infocusstudio.tz
@josh4mosh