CRDB Bank Plc

@crdbbankplc

Wewe ni swahiba wetu wa nguvu, tunakusikiliza! 👂
Followers
411k
Following
68
Account Insight
Score
69.25%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
6049:1
Weeks posts
Benki ya CRDB imeendelea kuimarisha nafasi yake kama kinara wa sekta ya fedha nchini kwa kuongoza katika viashiria vikuu vya soko ikiwamo amana kwa asilimia 27, mikopo kwa asilimia 30, mali kwa asilimia 28 pamoja na faida baada ya kodi kwa asilimia 32, mafanikio yanayoonyesha nguvu ya biashara, imani ya wateja na uimara wa mkakati wa Benki hiyo sokoni. Akiwasilisha taarifa yake katika Mkutano Mkuu wa 31 wa Wanahisa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema Benki itaendelea kuwekeza kimkakati katika teknolojia, ubunifu wa kidijitali pamoja na mifumo ya kisasa ya utoaji huduma ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji, kuboresha uzoefu wa wateja na kuharakisha ukuaji wa biashara. Aidha, amesema Benki ya CRDB itaendelea kupanua uwepo wake katika masoko ya kikanda na kimataifa sambamba na kuimarisha nafasi yake kama taasisi kubwa zaidi ya kifedha Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku ikiendelea kujenga thamani endelevu kwa wanahisa na kuchochea ukuaji wa uchumi. #CRDBBank #AGM2026
95 1
1 day ago
Benki Isiyo na Mpinzani 💪📈. Matokeo ya fedha ya Robo ya Kwanza ya 2026 yanaonyesha Faida baada ya kodi imeongezeka kwa 18.9% hadi kufikia TZS Bilioni 206.2. Matokeo haya yanaifanya Benki yetu ya CRDB kuwa kinara katika viashiria vyote vya kiutendaji kama ifuatavyo: 🔹 Mali: Sh. Trilioni 23.9 (7.1%) 🚀 🔹 Mikopo: Sh. Trilioni 14.7 (6.8%) 🤝 🔹 Amana: Sh. Trilioni 16.2 (9%) 💰 🔹 Mikopo Chechefu: 2.85% 🏗️ Tunawashukuru wateja na wadau wetu kwa kuendelea kuiamini na kuifanya Benki yenu ya CRDB kuwa nambari 1 nchini 🙏 Safari inaendelea…pamoja hatua kwa hatua! #CRDBBank
1,508 165
18 days ago
Nyuma ya timu bora kuna Benchi la Ufundi. Nyuma ya Tangazo pendwa kwa sasa ‘CRDB Bank Federation Cup’ kuna timu kubwa iliyoshirikiana kwa pamoja kuanzia mbegu ya wazo ilivyopandwa hadi kuchipua na leo hii tunafaidi kujionea Tangazo hili. Je wewe umeliona? Kama kawa tumeli-pin kwenye kurasa zetu @crdbbankplc na @crdbbanksports #behindthescene #crdbbankfederationcup2026 #crdbbank #tunakusikiliza
19 0
41 minutes ago
Lake Tanganyika Kigoma kitawaka leo🔥 Jiji lenye utajiri wa mawese na migebuka kuna mbungi ya kukata na shoka itapigwa. Wale wa Mwanga, Burega, Buzebazeba na maeneo ya Jirani tunakutana uwanja wa Lake Tanganyika leo saa 10 jioni . Chama gani litaibuka na ushindi leo ? @mashujaafcofficial au @azamfcofficial ? #crdbbankfederationcup2026 #crdbbank #tukusikiliza
66 2
1 hour ago
Nyie Simba 🦁 wanalitaka msimu huu! ‎ ‎Wababe wa Soka nchini, wanamsimbazi wanaenda vitani na kiu ya kulinyakuwa Kombe la CRDB Federation Cup wamejitamba lakini @creez_favors anasema anaamini mambo hayatokuwa rahisi sana. Maneno ya @ahmedally_ yatageuka vitendo? Hebu tusubiri ukweli wa Dakika 90 ‎ ‎#crdbbankfederationcup2026 ‎#crdbbank ‎#tunakusikiliza
1,118 17
3 hours ago
Hili mbungi la leo 🙌🏿, tusubiri dakika 90’ tu ⚽️. Mnyama mkali 🦁 @simbasctanzania kukipiga dhidi ya wakusanya mpato wa nchi @traunitedsportsclub . Hii ndo ile siku ya mtoto hatumwi dukani maana kuna timu italia 😢 nyingine itacheka 😂. Tukutane 12:30 jioni katika dimba la KMC . Unamwona nani Man of the Match leo? 👀 Tuambie kwenye comment #crdbfederationcup2026 #crdbbank #tunakusikiliza
884 20
4 hours ago
Wanasema kazi na bata… na kweli baada ya siku mbili za kazi kubwa zilizopambwa na habari njema ya gawio nono linaloendelea kukua mwaka hadi mwaka, ukafika wakati wa kusherehekea kupitia CRDB Bank Wanahisa Gala 2026. ✨ Wanahisa wetu waliungana katika usiku maalum wa kusherehekea mafanikio ya benki yetu, tukiongozwa na Mbunge wa Arusha na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Paul Makonda. Burudani ilisimamiwa kwa kiwango cha juu na A-Town finest G Nako pamoja na Toto Bad Marioo waliohakikisha shangwe za gawio haziishii ndani ya ukumbi wa mkutano pekee. 🎶 Tunatoa shukrani za dhati kwa wanahisa wetu wote na wadau mbalimbali walioungana nasi katika siku hizi mbili zilizogusa nyoyo za wengi na kuendelea kuonesha imani kubwa waliyonayo kwa Benki ya CRDB. Tukutane tena mwakani katika Mkutano Mkuu wa 32 wa Wanahisa. 🤝 #CRDBBank #AGM2026
691 5
13 hours ago
TZS 500,000 💰 zileee… Kwa mfano wewe ni @pacom_zouzoua umetoka kulamba TZS 500,000 zako za Man of the match kwenye #crdbbankfederationcup2026 ungefanyia nini 👀 ? Mimi ningeweka kwenye TemboCard Prepaid 💳 yangu nikatishe weekend hii na shopping 🛒 mwendo wa Shwaaa niingie kwenye droo ya kushinda tiketi kwenda kucheck Fainali za FIFA WORLD CUP 2026 au TV inch 85 mpyaaaaaa!!! Hongere sana Pacome, leo ulikuwa on 🔥 #crdbbankfederationcup2026 #crdbbank #tunakusikiliza
618 14
15 hours ago
Simu zimeita huko Isamuhyo 🏟️ Hello Coastal Union 📞 nusu fainali panafananaje huko? Kuna baridi tuje na masweta au kijoto fulani hivi tubebe misuli? - alisikika Muda akihoji 😎 #crdbbankfederationcup2026 #crdbbank #tunakusikiliza
1,288 4
16 hours ago
Wananchiii waleeee nusu fainali⚽️! Mechi dume na ya kukata na shoka imetamataki kwa wananchi kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumchapa Jkt Tanzania goli 2️⃣ kwa bila . Hongerani @yangasc #crdbbankfederationcup2026 #crdbbank #tunakusikiliza
428 3
16 hours ago
Dakika ya 48’ @jkt_tanzania_fc 🆚 @yangasc Boli ⚽️ linapigwa kisawa sawa hapa wa Meja Jenerali Isamuhyo, wanaume 22 wakivuja jasho kutinga hatua ya nusu fainali ya #crdbbankfederationcup2026 #crdbbankfederationcup2026 #crdbbank #tunakusikiliza
1,111 2
17 hours ago
Half time @jkt_tanzania_fc 0️⃣ 🆚 2️⃣ @yangasc . Nini kifanyike kipindi cha pili kwa JKT? 👀 #crdbbankfederationcup2026 #crdbbank #tunakusikiliza
189 3
17 hours ago