Home itvtzPosts

ITV TANZANIA

@itvtz

Official Instagram account for ITV Tanzania P.O.Box 4374, DAR ES SALAAM Tel: 065 877 7144 , 0767777147 Email:[email protected] 👍@radioonetanzania
Posts
66.0k
Followers
2.0m
Following
6
Account Insight
Score
55.59%
Index
Health Rate
80%
Users Ratio
342305:1
Weeks posts
81.08
934 30
15 days ago
#PONGEZI: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, ameipongeza ITV kwa mchango wake mkubwa katika kuhabarisha, kuelimisha na kuujuza umma kupitia habari zenye weledi na uzalendo.
104 16
5 days ago
#HABARI:Benki ya NMB Plc imepata ufadhili wa jumla ya Dola za Marekani milioni 180, sawa na takribani Shilingi Bilioni 468.1 za Kitanzania, kutoka IFC, British International Investment na Norfund, kwa ajili ya kuongeza mikopo kwa biashara ndogo ndogo na za kati, sekta ya kilimo, wanawake wajasiriamali na biashara zinazoongozwa na vijana nchini Tanzania. Ufadhili huo unajumuisha Dola milioni 100 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa, IFC, sawa na takribani Sh bilioni 260; Dola milioni 50 kutoka British International Investment, BII, sawa na takribani Sh bilioni 130; na Dola milioni 30 kutoka Norfund, sawa na takribani Sh bilioni 78. Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Kigali, Rwanda, pembezoni mwa Mkutano wa Wakurugenzi Wakuu Afrika, Africa CEO Forum. Akizungumza wakati wa utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema ufadhili huo ni ishara ya imani ya taasisi za kimataifa kwa mkakati wa NMB na nafasi yake katika kusaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia sekta binafsi, kilimo, wanawake na vijana. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Kanda ya Afrika wa BII, Chris Chijiutomi, alisema uwekezaji huo unaendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya BII na NMB, huku ukilenga kusaidia upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa MSMEs na biashara za kilimo. NMB inatarajiwa kutumia fedha hizo kuongeza mikopo, kuimarisha minyororo ya thamani ya kilimo na kupanua fursa.
296 6
5 hours ago
#HABARI: Wawekezaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika kahawa mkoani Kagera wameiomba Serikali kutenga fungu la fedha ili kuviwezesha viwanda vya ndani. Hatua hiyo itasaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora wa juu zinazokidhi viwango vya kimataifa. Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa kiwanda cha AMMIZA, Amiry Hamza, wakati akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB). Wajumbe hao walikuwa wametembelea kiwanda hicho kilichopo katika Manispaa ya Bukoba. Akijibu ombi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Prof. Aurelia Kamzora, amewashauri wawekezaji hao kujiunga na mfuko wa SANNVI. Amesema kuwa kujiunga na mfuko huo kutawawezesha kupata uwezeshwaji wa kiuchumi wanaouhitaji. Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania Follow @itvtz @radioonetanzania @capitaldigitaltanzania .
67 1
5 hours ago
FT: Simba 4-0 TRA
773 25
6 hours ago
#HABARI: Kutokana ya kuendelea kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii pamoja na athari zake kwa wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo hatarini, wadau wameibua mkakati maalum Wa kukabiliana na vitendo hivyo nchini. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kuanzishwa kwa mpango maalum wa uhamasishaji na kuwajengea uwezo viongozi mbalimbali, walimu pamoja na wanafunzi mkoani Arusha ili waweze kutumia uongozi wa mguso katika kuibua, kupinga na kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
35 2
6 hours ago
#HABARI: Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kushirikiana na Wananchi katika kutatua na kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto mbalimbali ikiwemo migongano baina ya binadamu na Wanyamapori Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameyasema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb),kwa lengo la kueleza mafanikio ya serikali katika wilaya hiyo pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. Katika ziara hiyo, Dkt. Kijaji ametumia fursa hiyo kukutana na wakazi wa eneo hilo na kusikiliza changamoto zao, hususan zinazohusu migongano kati ya binadamu na wanyamapori. Aidha, Dkt. Kijaji amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao katika ikutatua kero zinazowakabili, ikiwemo migongano baina ya binadamu na wanyamapori.
61 0
6 hours ago
‎#HABARI: Rais wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kitakachotumika kujenga jengo la madrasa katika Kata ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya elimu ya dini kwa watoto wa eneo hilo. ‎ ‎Fedha hizo zinatajwa kuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Vingunguti, hususan watoto waliokuwa wakilazimika kusomea nje kutokana na ukosefu wa miundombinu rafiki ya kujifunzia. Ujenzi wa madrasa hiyo unatarajiwa kutoa mazingira bora na salama ya kujifunzia pamoja na kuongeza hamasa ya elimu ya dini kwa watoto na vijana wa kata hiyo. ‎ ‎Akizungumza mara baada ya kukabidhi eneo hilo kwa viongozi wa dini wa Kata ya Vingunguti, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia inaendelea kugusa maisha ya wananchi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya pamoja na maendeleo ya kijamii. ‎ ‎Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Segerea, Agnesta Kaiza, ambaye alikuwa miongoni mwa waliofanikisha upatikanaji wa eneo hilo, amesema ushirikiano kati ya viongozi wa serikali, wananchi na viongozi wa dini umewezesha kufanikisha hatua hiyo muhimu kwa maendeleo ya watoto wa Vingunguti. ‎ ‎Mheshimiwa Kaiza amesema serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa wakati, huku akisisitiza kuwa elimu ya dini ni msingi muhimu katika kujenga taifa lenye maadili, heshima na uwajibikaji. ‎ ‎ Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania Follow @itvtz @radioonetanzania
97 7
6 hours ago
HT: Simba 2-0 TRA
344 9
7 hours ago
Kwa haya na Mengine mengi usikose kuungana nasi ifikapo Saa mbili kamili usiku. . Unaweza pia kutazama Taarifa yetu ya Habari kupitia Youtube na Facebook #ITVTanzania . Usisahau Ku-Subscribe ili kupata Taarifa zetu za #Habari kila zinapotufikiaKwa haya na Mengine mengi usikose kuungana nasi ifikapo Saa mbili
38 2
7 hours ago
#HABARI:Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-Centre) kimetoa mafunzo kwa maafisa wa madawati ya PPP kutoka mamlaka mbalimbali za serikali kwa lengo la kuwaimarisha katika uibuaji, uchambuzi na usimamizi wa miradi ya ubia nchini. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo maafisa kutoka serikali kuu, mamlaka za serikali za mitaa pamoja na wadau wa sekta binafsi ili waweze kuelewa kwa kina utekelezaji wa miradi ya PPP na majukumu yao ya kisheria. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Maandalizi na Uchambuzi wa Miradi ya PPP. Augustino Saibull amesema kitengo hicho kina jukumu la kutoa usaidizi wa kiufundi kwa taasisi za serikali katika kuandaa maandiko ya miradi pamoja na kufanya uchambuzi wa miradi inayowasilishwa. Amesema pia PPP-Centre hutoa mafunzo kwa taasisi za serikali na sekta binafsi kuhusu utekelezaji wa miradi ya PPP ili kuongeza uelewa na ufanisi katika utekelezaji wa miradi hiyo. Ameongeza kuwa sababu kubwa ya kuendesha mafunzo hayo ni kuwakumbusha maafisa hao wajibu wao wa kisheria pamoja na kuwapa uelewa mpana wa taratibu za PPP kuanzia hatua ya uibuaji wa miradi, maandalizi, ununuzi hadi usimamizi wake. Aliongeza kuwa mafunzo hayo ni endelevu kutokana na mabadiliko yanayoendelea kujitokeza katika mazingira ya biashara na sheria zinazosimamia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi. “Dhana ya PPP inaendelea kukua duniani kote, hivyo watendaji wanahitaji mafunzo ya mara kwa mara ili kwenda sambamba na mabadiliko hayo,” amesema
27 0
7 hours ago
‎#HABARI: Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuhakikisha Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Chemba unakamilika kwa wakati ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Wilaya ya Chemba. ‎ ‎Waziri Mkuu amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Chemba unaotekelezwa kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Chemba. ‎ ‎Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji kutoka Wizara ya Maji, Eng. Charles Mafie amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 11 unatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 18,141 wa Mji wa Chemba pamoja na vijiji vya Chemba, Chambalo, Kambi ya Nyasa, Gwandi, Paranga na Makamaka. ‎ ‎Amesema mradi huo umefikia asilimia 76 ya utekelezaji na unahusisha ujenzi wa visima vitatu vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita 207,000 kwa saa, matenki ya kuhifadhi maji, kituo cha kusukuma maji pamoja na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji yenye urefu wa kilomita 60. ‎ ‎Amesema mradi huo utaongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 37 ya sasa hadi asilimia 100 na kuongeza uzalishaji wa maji kutoka wastani wa lita laki moja na sabini kwa siku hadi kufikia zaidi ya lita milioni tatu kwa siku. ‎ ‎Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi M/s Megha Engineering and Infrastructure Limited (MEIL) chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri WAPCOS Limited. ‎ ‎Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kuhakikisha wanawalipa kwa wakati vijana, mafundi na vibarua wanaoshiriki katika utekelezaji wa kazi kupitia mikataba ya ushirikiano (subcontracting).
104 4
10 hours ago