Home dc_ilalaPosts

Mkuu wa Wilaya ya Ilala

@dc_ilala

Ukurasa rasmi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala DC - @mpogoloe S.L.P 15486
Followers
6,421
Following
19
Account Insight
Score
52.85%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
338:1
Weeks posts
DC MPOGOLO AIPONGEZA HALMASHAURI YA JIJI LA DSM KWA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA USAFI WA MAZINGIRA.
194 34
18 hours ago
Usafi wa Jiji baada za Mvua za Masika @elihurumamabelya
10 1
22 hours ago
Baadhi ya wanainchi wa Tabata jijini Dsm wampongeza Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kutenge fedha za ujenzi wa barabara ya Tabata bima - kimanga iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali jiji la Dsm. #kazinaututunasongambele 🇹🇿🇹🇿#karibujijiladsm @samia_suluhu_hassan @mwigulunchemba @ikulu_mawasiliano
17 0
1 day ago
Mapema Mei 15, 2026 Mkuu wa wilaya ya ilala Mhe. Edward Mpogolo ameshiriki hafla ya utiaji saini ya mkataba ujenzi uwanja wa kisasa wa klabu ya mpira wa miguu nchini Yanga. Hafla hiyo imehudhuliwa na mkuu wa mkoa wa dar es salaam mhe. Albert chalamila na muwekezaji wa klabu hiyo ndug: Ghali Said Mohammed pamoja na Rais wa klabu hiyo Eng. Hersi Ally Said na wanachama na vipenzi wa soko inchi. @yangasc @eng_hersi_said @gsmgroupofcompanies
6 0
1 day ago
BARABARA YA TABATA BIMA - KIMANGA YAPATA MWAROBAINI Mapema wiki hii Mei 12, 2026 Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na TARURA imeanza utekelezaji wa ukarabati wa barabara ya Tabata Bima–Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu na kuondoa changamoto ya usafiri kwa wananchi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema tayari Serikali imepokea fedha kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa mita 650 unaolenga kujengwa kwa kiwango cha zege. Mpogolo amesema maelekezo yametolewa kwa wataalamu kuondoa kifusi kilichokuwa kimewekwa katika eneo hilo ili kupisha ujenzi rasmi wa barabara hiyo, huku akisisitiza kuwa kazi zinaendelea usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanaanza kutumia barabara hiyo haraka iwezekanavyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amesema Halmashauri ya Jiji tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara hiyo ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto kubwa ya mashimo na kusababisha usumbufu kwa wananchi. Amesema kufuatia ziara ya ukaguzi iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, tayari maelekezo yametolewa kwa wataalamu wa jiji pamoja na Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala kuanza kazi ya ukarabati mara moja, huku mkandarasi akiwa tayari amekabidhiwa eneo la mradi. Mabelya ameeleza kuwa ukarabati wa kipande hicho cha takriban mita 650 unalenga kuboresha upitishaji wa magari na wananchi pamoja na kurahisisha shughuli za usafiri na mawasiliano kwa wakazi wa Tabata Bima na Kimanga. Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wataalamu wa TANROADS na TARURA kuhakikisha wanasimamia sheria za matumizi ya barabara ili kuzuia uharibifu unaotokana na magari yenye uzito mkubwa kupita kiwango kinachoruhusiwa. Amesema Serikali itaendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa karibu ili kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi. #kazinaututunasongambele 🇹🇿🇹🇿#karibujijiladsm @samia_suluhu_hassan @mwigulunchemba @ikulu_mawasiliano
69 8
1 day ago
CHALAMILA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIJI LA DAR ES SALAAM Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, leo tarehe 13 Mei 2026 amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kueleza kuridhishwa kwake na hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo. Katika ziara hiyo, Mhe. Chalamila ametembelea mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Gymkhana II uliopo Kata ya Kivukoni pamoja na miradi ya uboreshaji wa barabara ya Kitunda–Kivule–Msongola yenye urefu wa kilometa 10.395 pamoja na Barabara ya Kivule Majohe Junction yenye urefu wa kilometa 2.875, Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mhe. Chalamila amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na ubora wa kazi zinazoendelea kufanyika. “Miradi hii inaonesha dhamira ya Serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi. Nimeridhishwa na kasi ya utekelezaji pamoja na ubora wa kazi zinazoendelea kufanyika, hivyo niwahimize wasimamizi kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa,” amesema Mhe. Albert Chalamila, Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la dar es salaam , katibu tawala wilaya Ilala, viongozi mbalimbali pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri hiyo
78 4
3 days ago
Mzazi Akishiriki, Mtoto anafanikiwa. Ni kampeni yenye lengo la kuongeza ushiriki wa Wazazi katika maendeleo ya elimu, Kuboresha ufaulu wa wanafunzi, Kuimarisha ushirikiano kati ya walimu na wazazi pamoja na kujenga mazingira bora ya kufundisha na kujifunzia. TUMEDHAMIRIA HALMASHAURI YA JIJI KUJENGA UMOJA KATI YA WAZAZI NA WALIMU NA SERIKALI. @jiji_la_dsm @samia_suluhu_hassan @elihurumamabelya @ikulu_mawasiliano @tamisemi @millardayo @cityfmdsm @dc_ilala @mcmwakyoma_ @dr.hmwinyi @mwigulunchemba @profrizikishemdoe @officialshetta
17 9
3 days ago
Tushiriki ili tujadili kwa pamoja Mafanikio ya watoto wetu. #shulekwashule
58 13
3 days ago
KAMATI YA FEDHA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM IKIONGOZWA NA MSTAHIKI MEYA MHE. NURDIN BILAL YARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 11 Mei 2026 imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kata mbalimbali za Jiji hilo kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa miradi pamoja na thamani ya fedha. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Mombasa–Moshi Bar yenye urefu wa kilomita 0.3 katika Kata ya Ukonga, ujenzi wa Kituo cha Polisi Bonyokwa katika Kata ya Bonyokwa, ujenzi wa vyumba 20 vya madarasa na matundu 45 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Bonyokwa kata ya Bonyokwa pamoja na ujenzi wa vyumba 20 vya madarasa na matundu 45 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Liwiti iliyopo Kata ya Liwiti. Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhe.Nurdin Bilal amesema kamati hiyo imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka wasimamizi wa miradi kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa. “Miradi hii ina mchango mkubwa katika kuboresha huduma kwa wananchi wetu, hivyo ni wajibu wa kila msimamizi kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kupitia ubora wa kazi zinazotekelezwa. Tunaendelea kusisitiza uwajibikaji na usimamizi madhubuti ili wananchi waweze kupata huduma bora,” amesema Mhe. Bilal. Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndg. Elihuruma Mabelya amesema Halmashauri inaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo kwa karibu ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati, kwa ubora unaotakiwa na kuwanufaisha wananchi wa Jiji la Dar es Salaam. Ameeleza kuwa ushirikiano kati ya viongozi, wataalamu na wananchi umeendelea kuwa chachu ya mafanikio ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Jiji letu. Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Fedha na Utawala ya kufuatilia maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
406 30
5 days ago
Mpema mei 9,2026 Mkuu wa wilaya ya ilala alizindua na kuweka Jiwe la msingi Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Ulongoni B iliyojengwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo Mhe. Edisa Mwambeleko akishirikiana na wadau Mbalimbali wa maendeleo. Aidha Mpogolo alimpongeza jitihada za Mwenyekiti wa Mtaa wa Ulongoni B kwa kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo na kuwasii wanainchi wa Mtaa ya Ulongoni kuendelea kutoa ushilikiano na kuunga mkono jitihada za Serikali . Hafla hiyo iliudhuliwa na Mwenyekiti wa ccm wilaya ya ilala Ndg. Alhaji Said Sultan Sidde, Diwani wa kata ya Gongolamboto @advocate_ken_mlawa wadau wa maendeleo pamoja na wanainchi wa mtaa wa Ulongoni B #jijiletu #kazinaututunasongambele 🇹🇿🇹🇿 #karibujijiladsm #lipakodikwamaendeleo @samia_suluhu_hassan @mwigulunchemba @ikulu_mawasiliano @msemajimkuuwaserikali @officialshetta @elihurumamabelya @mpogoloe @ortamisemi @tumeyauchaguzi_tanzania @crdbbankfoundation @officialshetta @bunge.tanzania @maendeleoyajamii albert_john_chalamila @gersonmsigwa @cityfmdsm @charangwaselemani @zungumussa @advocate_ken_mlawa
55 0
6 days ago
Mpema mei 9,2026 Mkuu wa wilaya ya ilala alizindua na kuweka Jiwe la msingi Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Ulongoni B iliyojengwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo Mhe. Edisa Mwambeleko akishirikiana na wadau Mbalimbali wa maendeleo. Aidha Mpogolo alimpongeza jitihada za Mwenyekiti wa Mtaa wa Ulongoni B kwa kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo na kuwasii wanainchi wa Mtaa ya Ulongoni kuendelea kutoa ushilikiano na kuunga mkono jitihada za Serikali . Hafla hiyo iliudhuliwa na Mwenyekiti wa ccm wilaya ya ilala Ndg. Alhaji Said Sultan Sidde, Diwani wa kata ya Gongolamboto @advocate_ken_mlawa wadau wa maendeleo pamoja na wanainchi wa mtaa wa Ulongoni B #jijiletu #kazinaututunasongambele 🇹🇿🇹🇿 #karibujijiladsm #lipakodikwamaendeleo @samia_suluhu_hassan @mwigulunchemba @ikulu_mawasiliano @msemajimkuuwaserikali @officialshetta @elihurumamabelya @mpogoloe @ortamisemi @tumeyauchaguzi_tanzania @crdbbankfoundation @officialshetta @bunge.tanzania @maendeleoyajamii albert_john_chalamila @gersonmsigwa @cityfmdsm @charangwaselemani @zungumussa @advocate_ken_mlawa
13 0
6 days ago