millardayo

@millardayo

Award winning TV/Radio Personality | Amplifaya @CloudsFMTZ |Journalist from Africa | Bookings [email protected] | 📍 DSM, Tanzania
Posts
85.7k
Followers
15.5m
Following
1,507
Account Insight
Score
83.58%
Index
Health Rate
80%
Users Ratio
10330:1
Weeks posts
105.27
Bandari House, (@bandarihousekurasini ), jengo la kisasa lililopo karibu na Bandari ya Dar es salaam mkabala na Kituo cha Mwendokasi cha Bandari, limeendelea kuvutia Wawekezaji, Watu binafsi, Mashirika pamoja na Kampuni mbalimbali za usafirishaji kutokana na ukaribu wake na huduma muhimu za bandari hali inayorahisisha shughuli za biashara na usafirishaji wa mizigo. Jengo hilo lenye ghorofa sita lina huduma ya maji muda wote, ulinzi na usalama wa saa 24 pamoja na eneo la maegesho ya magari huku likiwa limebuniwa mahsusi kwa biashara zinazotegemea huduma za Bandari pamoja na mazingira bora ya kibiashara kwa Wateja na Wawekezaji. Kwa wanaohitaji huduma zinazohusiana na Bandari hakuna sababu ya kwenda mbali kwani Bandari House ipo karibu kabisa na eneo la Bandari hatua inayorahisisha upokeaji na usafirishaji wa mizigo pamoja na kuongeza ufanisi wa shughuli za kila siku za kibiashara. #MillardAyoUPDATES
1,229 66
4 days ago
Kampuni ya Mkazi Solutions (@makazisolutions_tanga ) kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya za Muheza na Pangani, imetangaza fursa za uwekezaji wa viwanja katika miradi miwili iliyopo mkoani Tanga. Mradi wa kwanza ni Kilapula Azimio Farm, uliopo umbali wa kilometa 20 kutoka Tanga Mjini na kilometa 2 kutoka Mizani ya Pongwe. Eneo hili linapakana na barabara ya lami ya Tanga–Segera, bomba la mafuta la EACOP, reli ya kisasa (SGR), pamoja na stesheni ya Ngomeni ambayo ipo ndani ya mradi. Mradi wa pili ni Kipumbwi Satellite City ambapo huu ni mradi wa kimkakati unaounganisha Tanga kwa umbali wa kilometa 80, Dar es Salaam kwa kilometa 180, na Zanzibar kwa kilometa 60. Viwanja vya mradi huu vinapakana na bahari pamoja na barabara mpya ya lami, na vinapunguza umbali wa safari kati ya Tanga na Dar es Salaam kwa takriban kilometa 90. Aidha, mji wa Kipumbwi unatarajiwa kuwa kitovu kipya cha biashara kutokana na uwepo wa Bandari ya Kipumbwi, ujenzi wa soko la samaki pamoja na kiwanda cha kukaushia dagaa chenye thamani ya shilingi bilioni 1.3. Pia, ukaribu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Kisiwa cha Maziwe, vilivyopo umbali wa kilometa 30 tu kutoka bandari ya Kipumbwi, unaifanya fursa hii kuwa ya kipekee kwa uwekezaji wa kibiashara, kukuza utalii na kujenga mustakabali bora. Bei za viwanja ni nafuu, kuanzia shilingi milioni 2. Bei kwa mita ya mraba ni shilingi 3,000 kwa viwanja vya makazi, shilingi 5,000 kwa viwanja vya biashara, na shilingi 20,000 kwa Beach Plots. Hati hutolewa baada ya kukamilika kwa malipo. Kwa maelezo zaidi, tembelea ofisi za Makazi Solutions zilizopo Kijangwani, Zanzibar au Roundabout ya Mkwakwani, Tanga, au piga simu namba 0750 333 338. #MillardAyoUPDATES
1,062 67
14 days ago
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo Mei 16, 2026 amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Botswana, Hayati Festus Gontebanye Mogae, yaliyofanyika Jijini Gaborone. Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Kikwete amesema Tanzania inaungana na Serikali pamoja na Wananchi wa Botswana katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kufuatia kifo cha kiongozi huyo mashuhuri wa Bara la Afrika. Katika hotuba yake, Dkt. Kikwete amesema kuwa wakati wa uongozi wa Hayati Mogae, ushirikiano na uhusiano wa kindugu kati ya Tanzania na Botswana uliendelea kuimarika kwa kiwango kikubwa ambapo akizungumzia mapenzi ya Hayati Mogae kwa Tanzania, Dkt. Kikwete amesema "Hayati Rais Mogae alikuwa rafiki wa kweli wa Tanzania na aliipenda nchi yetu kwa dhati.” Dkt. Kikwete pia alieleza kuwa Hayati Rais Mogae alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umoja, mshikamano na amani barani Afrika, sambamba na kushiriki kikamilifu katika juhudi mbalimbali za usuluhishi wa migogoro katika mataifa tofauti ya Afrika. "Napenda pia kueleza kuwa binafsi nilipata heshima ya kufanya kazi na Rais Mogae kwa mara ya kwanza alipokuwa Makamu wa Rais, wakati mimi nikihudumu kama Waziri katika Serikali za Rais Ali Hassan Mwinyi na Rais Benjamin Mkapa. Nilianza kama Naibu Waziri wa Nishati na Madini, baadaye nikawa Waziri wa Maji, Nishati na Madini, kisha Waziri wa Fedha, na tulifanya kazi vizuri sana ndani ya SADC. Baadaye, alipokuwa Rais wa taifa hili kubwa, mimi nilikuwa nikihudumu kama Rais wa nchi yangu pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." "Rais Mogae alikuwa mtu mzuri kufanya naye kazi. Alikuwa mwenye misimamo, mwadilifu, na siku zote alikuwa akisema kile alichokiamini, lakini kwa upole na heshima.” Amesema Dkt. Kikwete #MillardAyoUPDATES
706 49
4 hours ago
Ndugu Wilson Michael, Mkazi wa Mwanza amesema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) (@wcf_tz ), umekuwa msaada mkubwa kwake baada ya kupata ajali kubwa akiwa kazini mwaka 2022 wakati wa ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi. Wilson amesema ajali hiyo ilisababisha kuvunjika uti wa mgongo akiwa kazini jambo lililomfanya ashindwe kurejea tena kwenye shughuli zake za kazi kutokana na hali yake kiafya. Amesema baada ya ajali hiyo alipitia kipindi kigumu cha matibabu na changamoto mbalimbali za maisha, lakini WCF ilisimama naye tangu mwanzo hadi wakati huu kwa kugharamia matibabu pamoja na kumpatia fidia inayomsaidia kwa kiasi kikubwa kuendelea na maisha. Kwa mujibu wa Bw. Wilson, faraja na msaada anaoupata kutoka WCF vimempa matumaini mapya licha ya madhara aliyoyapata kutokana na ajali hiyo ya kikazi. Aidha, amesema uwepo wa WCF ni muhimu kwa Wafanyakazi wote nchini kwani huwapa uhakika wa msaada wanapopatwa na ajali au madhara wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi, na kutoa ombi kwa waajiri wote nchini kujisajili na Mfuko huo pamoja na kuwasilisha WCF michango ya wafanyakazi wao wote kwa wakati ili kuwa kinga kwao watakapopata changamoto kazini # MilladAyoUPDATES
830 35
4 hours ago
Unapanga safari ya kwenda China? 🇨🇳 Tuachie sisi tukusaidie kupata visa yako kwa urahisi na bila stress. ✔️ Mchakato wa haraka ✔️ Ushauri wa kitaalamu ✔️ Huduma ya uhakika Wasiliana nasi leo: +255 743 794 416 +255 769 567 651 #Cielotravels #ChinaVisa #
84 6
6 hours ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote pamoja na Ujumbe wake, Ikulu Jijini Dar es salaam hii leo Mei. 16, 2026. #MillardAyoUPDATES
5,832 341
7 hours ago
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema kitendo cha Wananchi kushangilia pindi Viongozi wa Nchi Wanaporafiki ni matokeo ya Chuki na hasira kubwa iliyojengwa kwa Wananchi na Vingozi ikiwemo yaliyotokea katika uchaguzi Mkuu wa Octoba 2025. Akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa kuhusu mwelekeo na Khatima ya Tanzania, leo May 16, 2026, Jijini Dar es salaaam, Othman amesema “Mshikamano wa kijamii umeyumba sana tunasema pamoja na utamaduni huu wa Mtanzania wa kuwa na mshikamano, kuwa na uvumulivu lakini kwa yaliyotokea katika uchaguzi basi umeyumbisha sana mshikamano huu wa Kitaifa tumeona Chuki kubwa ambayo imejengwa hasira kubwa ambayo iko kwa Wananchi” “Tunachosikitika na kinachosikitisha ni kwamba viongozi badala ya kuona hili ni tatizo walichukulie hatua wao wanalaani watu wanaoshangilia Kiongozi anapofariki haya ni matokeo tu ya kile ambacho mmekitengeneza sasa wakulaaniwa ni nani? Ndie aliyevuna matokeo au aliyesababisha tukafika hapa ndio maana mimi nasema haya yote ni matokeo ambayo mimi nayaita uasi katika Nchi hii na uasi mkubwa ni pale ambapo mna Viongozi ambao hawataki kwa makusudi, wanavuruga misingi ya Katiba, misingi ya Sheria katika Nchi na kutufikisha hapa tulipo” #MillardAyoUPDATES
2,020 141
8 hours ago
Chaguo sahihi kutoka @babyshop._tz kwa wazazi wanaotaka kufundisha mtoto kula kwa uhuru, usalama na kujitegemea. . 📍Mlimani city 📍Gsmmall Msasani 📍Gsm Plaza- Kamata 📍Salamander Tower 📍Dodoma-Shoppers Plaza
64 9
8 hours ago
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema unahitajika kufanyika mjadala wa Kitaifa kuhusu mustakabali wa Nchi baada ya Ripoti ya Jaji Othman Chande kuhusu vuguvugu la Oktoba 29, 2025. Akizungumza leo May 16, 2026 Jijini Dar es salaam, wakati wa Mjadala wa Kitaifa Kuhusu Mwelekeo na Hatma ya Tanzania, Othman amesema, “Ndugu washiriki, nikiri kwamba hii ni mara ya kwanza kwa chama chetu kuandaa mjadala wa Kitaifa wa namna hii, tumefanya hivi kama tulivyoelekezwa kufanya tafakuri kuhusu Nchi yetu tulipotoka, ilipo sasa na yale tunayoyaona kuhusu mustakabali wa Taifa letu.” “Niseme kwa ufupi, bado tunaona kiza kinene kimetanda, na bado kipo mbele yetu, kwasababu hiyo, tukaona sisi kama sehemu ya kutekeleza wajibu wetu wa Kikatiba kama Chama cha Siasa na kama sehemu ya Watanzania, tuchukue hatua hii ya kuwaomba wenzetu pamoja na Wadau mbalimbali tushirikiane kuutazama mustakabali wa Nchi yetu na kufanya hili kuwa sehemu ya mjadala wa Kitaifa ili kupata mustakabali mwema wa Nchi, baada ya yote yaliyopita na hata baada ya kutoka kwa Ripoti ya Jaji Chande, sidhani kama kuna Mtanzania anayeweza kuona kwa uhakika tunakoelekea mpaka sasa.” Amesema Othman Masoud Othman. #MillardAyoUPDATES
5,868 224
9 hours ago
#MillardAyoMagazeti Tz & Kenya May 16, 2026
510 12
15 hours ago
Hapa si Uturuki wala China ni @gsmhometz , ndani ya GSM Plaza Kamata, na mzigo mpya umeingia madukani! Wahi mapema, maana huu ni ubora usiopaswa kukukosa. Pata furniture bora na za kisasa kwa matumizi yako ya nyumbani au ofisini. Karibu GSM Home ujionee mwenyewe tofauti.
228 11
22 hours ago
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili nchini Botswana leo Mei 15, 2026, kumwakilisha Samia Suluhu Hassan katika shughuli za Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Botswana, Festus Gontebanye Mogae, aliyefariki dunia Mei 8, 2026 akiwa na umri wa miaka 86. Mazishi hayo yanatarajiwa kufanyika kesho, Mei 16, 2026, Jijini Gaborone ambapo baada ya kuwasili nchini humo, Dkt. Kikwete alisaini Kitabu cha Maombolezo katika Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Botswana, ambapo alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Botswana, James Bwana, pamoja na Spika wa Bunge la Botswana, Dithapelo Keorapetse, na Katibu wa Bunge hilo, Dkt. Gabriel Goitsemodimo Gosiame Malebang. #MillardAyoUPDATES
5,584 1,172
22 hours ago