Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Edward Mpogolo @mpogoloe amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya @elihurumamabelya kutenga zaidi ya Shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya uboreshaji na Utunzaji wa Mazingira ndani ya Jiji hilo.
Mpogolo ametoa tamko hilo leo Mei 16 2026 mara baada ya kutembelea Fukwe za Dengu Beach na kujionea shughuli mbalimbali zinazoendea kwa lengo la Utunzaji wa Mazingira ikiwemo zoezi la kuweka sawa udongo ili Fukwe hizo ziweze kutumika kwenye shughuli za michezo.
Wakati huo huo ametoa wito kwa Wadau mbalimbali na Taasisi Binafsi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam za kupendezesha Jiji kwani Wilaya ya Ilala ndio kitovu cha kupokea Wageni pindi wanapoingia Nchini.
________________________________________________
SIKILIZA 91.7 FM CITY FM DAR ES SALAAM KWA HABARI MBALIMBALI, ELIMU YA FYA, SIASA, MICHEZO NA BURUDANI.
#cityfmdigital #citysports #cityfmdsm #mzeewakibendera
BARABARA YA TABATA BIMA - KIMANGA YAPATA MWAROBAINI Mapema wiki hii Mei 12, 2026 Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na TARURA imeanza utekelezaji wa ukarabati wa barabara ya Tabata Bima–Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu na kuondoa changamoto ya usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema tayari Serikali imepokea fedha kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa mita 650 unaolenga kujengwa kwa kiwango cha zege.
Mpogolo amesema maelekezo yametolewa kwa wataalamu kuondoa kifusi kilichokuwa kimewekwa katika eneo hilo ili kupisha ujenzi rasmi wa barabara hiyo, huku akisisitiza kuwa kazi zinaendelea usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanaanza kutumia barabara hiyo haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amesema Halmashauri ya Jiji tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara hiyo ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto kubwa ya mashimo na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Amesema kufuatia ziara ya ukaguzi iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, tayari maelekezo yametolewa kwa wataalamu wa jiji pamoja na Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala kuanza kazi ya ukarabati mara moja, huku mkandarasi akiwa tayari amekabidhiwa eneo la mradi.
Mabelya ameeleza kuwa ukarabati wa kipande hicho cha takriban mita 650 unalenga kuboresha upitishaji wa magari na wananchi pamoja na kurahisisha shughuli za usafiri na mawasiliano kwa wakazi wa Tabata Bima na Kimanga.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wataalamu wa TANROADS na TARURA kuhakikisha wanasimamia sheria za matumizi ya barabara ili kuzuia uharibifu unaotokana na magari yenye uzito mkubwa kupita kiwango kinachoruhusiwa.
Amesema Serikali itaendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa karibu ili kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.
@samia_suluhu_hassan@mwigulunchemba@ikulu_mawasiliano
Umoja wetu ni Nguvu yetu ya kuwa Watumishi wema na Bora kwa Ilala. Mungu atusaidie USIWE URAFIKI WA KUKAA VIJIWENI BALI UWE URAFIKI WA UTUMISHI WA WATU.
Hongera Cde. Mtendaji Mkuu wa Jiji @elihurumamabelya
Hongera sana Mdogo wangu na rafiki yangu Abdul-Rahaman Abdallah na Mkeo Bi. Sakina kwa kuwa na Ndoa nzuri sana. " _Ndoa ni safari ya upendo, subra na rehema. Mwenyezi Mungu awajalie maisha yenye amani, baraka na furaha isiyoisha. "Na miongoni mwa ishara zake ni kuwa amewaumbia wake zenu ili mpate utulivu kwao, naye akaweka baina yenu mapenzi na rehema.”
— Qur’an 30:21
@abdulrahman_abdallah_kassim
Nimepokea kwa shukrani kubwa kishikwambi (Tablet) nilichokabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Jonas Mpogolo @mpogoloe , akiwa sambamba na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Nurdin Bilal Juma @officialshetta .
Mhe. Edward Jonas Mpogolo @mpogoloe amesema:
“Ni jambo jema kwenda na wakati kwa Halmashauri kubwa na yenye viongozi wazuri wenye maono ya kuwatumikia watu kwa kupunguza matumizi ya gharama za ununuzi wa karatasi.”
Hatua hii ni sehemu ya kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kiuongozi kwenye kata zetu. Tunazidi kuishukuru Serikali yetu tukufu pamoja na watendaji wote wanaoendelea kuweka mazingira bora ya utendaji kazi kwa viongozi na watumishi kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo yenye tija.
cc: @jiji_la_dsm , @mpogoloe@elihurumamabelya@officialshetta@dc_ilala , @nassibukitabu ,
..............................
#DiwaniJangwani #NHK #NassibKitabu #jijiletu #SiasaNaUchumi #kazinaututunasongambele #karibujijiladsm #JangwaniInasonga #MaendeleoNiJukumuLetu
BARABARA YA TABATA BIMA - KIMANGA YAPATA MWAROBAINI Mapema wiki hii Mei 12, 2026 Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na TARURA imeanza utekelezaji wa ukarabati wa barabara ya Tabata Bima–Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu na kuondoa changamoto ya usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema tayari Serikali imepokea fedha kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa mita 650 unaolenga kujengwa kwa kiwango cha zege.
Mpogolo amesema maelekezo yametolewa kwa wataalamu kuondoa kifusi kilichokuwa kimewekwa katika eneo hilo ili kupisha ujenzi rasmi wa barabara hiyo, huku akisisitiza kuwa kazi zinaendelea usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanaanza kutumia barabara hiyo haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amesema Halmashauri ya Jiji tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara hiyo ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto kubwa ya mashimo na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Amesema kufuatia ziara ya ukaguzi iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, tayari maelekezo yametolewa kwa wataalamu wa jiji pamoja na Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala kuanza kazi ya ukarabati mara moja, huku mkandarasi akiwa tayari amekabidhiwa eneo la mradi.
Mabelya ameeleza kuwa ukarabati wa kipande hicho cha takriban mita 650 unalenga kuboresha upitishaji wa magari na wananchi pamoja na kurahisisha shughuli za usafiri na mawasiliano kwa wakazi wa Tabata Bima na Kimanga.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wataalamu wa TANROADS na TARURA kuhakikisha wanasimamia sheria za matumizi ya barabara ili kuzuia uharibifu unaotokana na magari yenye uzito mkubwa kupita kiwango kinachoruhusiwa.
Amesema Serikali itaendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa karibu ili kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.
#kazinaututunasongambele 🇹🇿🇹🇿#karibujijiladsm