Wenye Ideas kubwa ni wengi lkn wachache sana wanaweza kubadilisha ideas zao kuwa uhalisia,kila siku watu wanaota kuanzisha biashara, kubadili career, kusoma new skills, au kubadilisha maisha yao lakini wanagota kwenye ideation stage
Kim Parell anaandika kuwa tofauti ya wale wanao fanikiwa na wale wasiofanikiwa sio Kipaji, Akili au Bahati ni UTEKELEZAJI
Kwenye kitabu chake The eXecution Factor, anaelezea kuwa utekelezaji ndio ujuzi muhimu ambao unampa mtu mafanikio,ideas kubwa na kubwa ziko kila pahala lkn uwezo wa kufanyia kazi na kupata matokeo ni adimu na huo uadimu ndio unatengeneza washindi
Execution factor ni ule uwezo wa kubadilisha mawazo kuwa vitendo,na vitendo kuwa matokeo,sio kufanya kazi kwa bidii, au kuwa na perfect plan , badala yake ni kuwa na focus na nidhamu hivyo ndivyo vitakavyo kufanya usonge mbele bila kuogopa kufeli au kutokuwa na uhakika wa kile unachohitaji kukifanya
Kwenye kitabu chake anasisitiza kuwa utekelezaji sio kipaji cha kuzaliwa ni ujuzi ambao hata wewe unaweza KUJIFUNZA, Ukiamua, ameelezea kiundani vitu 5 ambavyo ni foundation ya kuwa mtekelezaji:-
1. Vision
2. Passion
3. Action
4. Resilience &
5. Relationship
Hivi nitavieleza vizuri kwenye andiko linalofuata lakini nitaeleza kidogo vinatufunza nini:-
1.Tusisubiri kila kitu kiwe tayari ndipo tuanze, na hapa Mimi nita mquote Mark Zuckerberg " Ideas don't come out fully formed they only become clear as you work on them"
2. TuFocus , ukiwa unatekeleza jambo vya kukuvuta shati haviwezi kukosa hivyo tunapaswa kufilter distraction zote ambazo havitusaidii kutimiza malengo yetu
3.TuPime matokeo yetu, Utekelezaji unakuwa bora pale ambapo unaweza kupima matokeo,
4.Tuwajibike,lazima tutengeneze utaratibu wa kujiwajibisha, uwajibikaji unalinda ubora wa kile tunachokifanya
5.Tuwe wanyumbulifu, kwasababu execution sio jambo lililonyooka, lazima kutakuwa na ups and downs, it's like a rollercoaster, hivyo unyumbulifu utatufanya tubaki michezoni
The eXecution Factor ni ukumbusho kuwa mafanikio hayaja hifadhiwa kwaajili ya walio bora zaidi, bali ni kwaajili ya wale wenye kujitoa, na utekelezaji ni daraja kati ya pale ulipo na kule unakotaka kwenda.
Happy New Year Fam😎🤏
Wanasema "Don't announce your next step before taking it" nakubaliana nayo lakini sio kwenye kila kitu
NI rule ambayo wengi wanaitumia, kila mtu kwa Imani na malengo yake, na hata mimi kuna pahala naitumia na Ina work , Lakini binafsi huwa situmii kwenye kila kitu
Kuna hatua ukitaka kuzipiga unapaswa kuzi expose ili upate external motivation ya kuzipiga kwa ubora na kwa muendelezo, na kuwa na uwezo wa kufanya improvements, hicho ndicho nilichokifanya hapa
Nimeamua kuweka malengo yangu open kabisa kwasababu nimeamua kuitumia kama sehemu ya accountability system niliyojiwekea ambayo hii itanisaidia control quality na consistency ya kila ninachodhamiria kufanya
Kama ambavyo nimeshare resolutions zangu, nitakuwa nikishare progress ya growth ups,downs, niliyojifunza, na yote nitakayo ya experience kwenye hii safari
Since ni mara ya kwanza nafanya hiki najua kuna vitu havitaenda kama vilivyopangwa, najua kutakuwa na setbacks za hapa na pale lakini niko tayari kukabiliana na chochote ambacho nitakutana nacho mbele
Kama ambavyo itakuwa mara ya kwanza kwangu kukutana na changamoto hizo na vivo hivyo hata hizo changamoto zenyewe zitakuwa zimekutana na mimi kwa mara ya kwanza ,
So it's kind like we all enters the game with equal chances, I'm new to them and they're new to me,the more they figure me out I will be figuring them out, so they better be prepared
Najua haitakuwa rahisi, lakini nina uhakika itakuwa safari ya ukuaji yenye excitement nyingi
Exciting part is the only reason I need for now and it's more than enough for me
So, I'll take the shot.
Let's get started.
#WatchMe
Kwa miaka ambayo Ruge aliianza kuitumikia Tanzania alitumia platform na uwezo na mapenzi yake yote kutuunganisha watanzania kwenye utambulisho wake wetu wa pamoja
"UTANZANIA"
Alifanya hivyo kupitia majukwa ya Clouds, Fursa,THT, Tanzania All Stars nk
RUGE aliiishi akiamini umoja wetu ndio silaha yetu kubwa, aliiishi akiamini tanapaswa kuishi kwa kupeana tafu sisi kwa sisi aliamini nguvu yetu ikiungana inaweza kuleta matokeo makubwa mno kwetu binafsi na kwa taifa zima
Ruge anabaki kwenye vitabu vya historia ya Tanzania kama Mzalendo na mtu ambae aliiishi kujenga Tanzania Bora
Tanzania Bora ni kitu kilichomnyima usingizi
Ruge aliiona Tanzania kama kisiwa cha fursa ambacho kila mmoja wetu anaweza kufanikiwa bila kumshusha mwingine, aliishi akiwatengeneza watanzania wengi kuwa ngazi za watu wengine kupanda kuyafuata mafanikio yao
7 bila yeye lakini Bado tunaendelea kuadhimisha na kusherekea maisha yake
Tupendane, Tuheshimiane, Tujaliane, Nchi hii ni yetu sote, ni wajibu wetu kuipenda, kuilinda na kuijenga
Live Long #RugeBadoAnaishi
🫡
Sio dhambi kuikumbusha Serikali majukumu yake.
Kuna maswala madogo madogo ambayo tunayachulia poa lkn yanaweza kuwa na impact kubwa kwa taifa mfano hili la vipaji,Burudan na Michezo
Ili sekta yoyote ikue lazima ifanyiwe uwekezaji na usimamizi wa kimkakati
Tunatamani Taifa star ifuzu kombe la Dunia na AFCON, lakini hakuna mkakati na usimamizi wa kuhakikisha lengo hilo lnatimia
Bonus na hamasa na haviwezi kutufanya tuwe bora uwanjani,Kamwe.
Tunatamanii watanzania washinde medali za dhahabu Olympic lkn hakuna mkakati wowote strong wa kuwaandaa vijana ili wakashinde hizo medali
Bahati mbaya tunaogopa kusema haya,
Ni mambo ambayo yanayowezekana, Kiptchonge hakuzaliwa mwanariadha alitengenezwa,Mbape hakuzaliwa mchezaji ni zao la mradi wa Serikali
Sisi Bado tunaamini Taifa stars inaweza kufuzu world cup na AFCON kwa hamasa na bonus
Haya tuendeleee na hamasa Niko pale nimekaa 😃
Tunatamani wasanii wetu washinde Grammy lakini kujenga Arena hatutaki
Haya tuendeleee kuota,sema tukiona kichaka tustuke
Ni kweli Serikali haiwezi kutufanyia kila kitu,lakini inaweza kufanya vitu vingi kwa ufanisi na kwa ukubwa,ni swala la kuamua tu
Duniani kote uwezo wa mtu binafsi uko limited, lkn uwezo wa Serikali ni limitless, swala la kujenga Arena au ku sponsor sports and talent centers za kukuza na kulea vipaji kwa Serikali ni rahisi mno, nchi nyingi duniani zinafanya hivi Spain, UK, France,Brazil, German,Morocco, SA,Egypt, Tunisia, Rwanda,Kenya nk
Kama taifa kuna vitu tunachukulia poa lakini vinaweza kuwa na faida kubwa sana kwenye taifa letu
Kupitia vipaji Kuna urahisi wa kulijenga na kulitangaza taifa kimataifa,Vipaji havina mipaka
Simbu anaweza kung'aa Olympic lkn akiweka rekodi sio yake ni ya Taifa zima
Imagine tukiwa na Sammata wengi na tukawa na uwezo wa kufuzu kombe la Dunia, taifa litakuwa na exposure kiasi gani
Imagine Trace Awards ingefanyika "Tanzanite Arena" , au "Kilimanjaro Arena" impact yake ingekuwaje
Just Imagine, hizi ni logic za kawaida kabisa.
Kwa taarifa tu, kiliachotokea Trace award sio fedheha kwa wasanii peke yao ni doa na fedha kubwa kwa taifa zima
Narudia Tena Kuikumbusha Serikali majukumu yake sio dhambi.
#NakupendaTanzania
Tufanyiane yote lakini tusisahau sisi sote ni watanzania, hii nchi ni yetu sote, tunaishi sisi leo, vizazi vyetu vitafuata kesho
Chochote utakachokifanya Leo kitaamua kizazi changu na chako kiishije kesho, tukiishi kwa ubinafsi na uonevu vizazi vinavyokuja baada yetu vitarithi mtindo huo huo, nchi itageuka kuwa ya visasi vizazi hadi vizazi
Tuishi kwa mfano wa JPM ambae mpaka Leo kizazi chake kina uhakika wa kuishi kwa kupendwa na watanzania wengi kama si wote (ukiwatoa wale wabinafsi)
Tuishi tukijua fika hatuishi kwasababu yetu bali tunaishi kuandaa maisha ya watakaofuata baada yetu
Kuna watu Leo wanaona aibu hata kupost picha ya JPM kwasababu nafsi zitawasuta kwasababu kwa unafiki na ubinafsi wao walikuwa wakimpinga utawala wake
Kuna wale ambao Leo nafsi zao zinawauma kuona JPM anasemwa kwa mazuri ya kila aina, wanaumia kwasababu wanajua wakiondika Leo hawako kwenye nafasi ya kusemwa kwa mazuri kwasababu walichagua kuishi maisha yao kibinafsi, wameishi wakinyonya na kuwakandamiza wengi kwa maslahi yao wachache
Kuna wale waliopost Leo kinafki tu lakini deep down wanajijua kabisa hawana sifa za kupost picha au chochote kinachomuhusu JPM, kwa ubinafsi na uonevu wao
Wote tutakufa lakini majina ya wachache walioishi kwa hofu ya mungu watakumbukwa na majina yao yatatajwa kwa heshima daima
Kama JPM alivyosema kwa kinywa chake mwenyewe "Ipo siku mtanikimbuka tena mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya" leo taifa zima linamkumbuka na linataja na kuimba majina yake kwa upendo na heshima kubwa sana
Chuma , Bulldozer, Jasiri, Mzalendo, Mwanamapinduzi, Rais Wa Wanyonge, Mtanzania Wa Kweli, Mpemda Haki na majina mengi ya kishujaaa
Licha ya kuimba majina yake lakini Tunapaswa kukumbuka kuwa Bado anatudai, anatudai kuipenda, kuitetea na kujenga Tanzania Bora , anatudai kuendeleza undugu wetu, anatudai kuishi kama binadamu na si kama wanyama wasio na utu
Kwa heshima kubwa Endelea kupumzika kwa amani #JPM5
MARCH BRAIN FOOD READING : 4 Books 1. Never Split The Difference by Chris Voss 2.Talk Like TED By Carmine Gallo 3. Pitch Anything By Oren Klaff 4. Obstacle In The Way By Ryan Holiday WATCHING : 21 videos 1. DOAC 2. Front Raw Seat 3. Vinh Giang 4. The MIT Monk
#LearnConnectExecute
My February Recap
✅ 2 Books • You Become What You Think By Subham K. Singh • The Power Of Your Subconscious Mind J. Murphy
✅ 1000+ Minutes YouTube Videos • Ruge Archive • The MIT Monk
✅ RUGE ARCHIVES + RUGE 7 Post
✅ Started WL Project Execution (Hili nitaeleza kwenye post zijazo)
✅ #NilinyooshaLove @damdam_marathon
✅ Attended @fikrazinduka Event
✅ 30+ hrs of reflection + 28 days of Journaling
✅ 20+ New Connections
✅ 12 Days of intense physical exercise
SPECIAL THANKS:
February nimefanikisha yote hayo lakini Kuna wengi ambao waliwezesha kwa namna moja ama nyingine,nachukua nafasi hii kuwapa maaua yao
@remmymbowa_@marcel__kitabu@praf.paparaz@henry_mwinuka_esq@djsma255@skytanzania@katunzi_tza
Na kipekeee kabisa shukrani kwa brother @Soudybrown mazungumzo ya tarehe 13 Feb yalikuwa noma sana niliokota madini mengi sana sana , shukran sana brother 🙏🏿
Na bila kuwasahau wengine wote ambao kwa namna moja ama nyingine tuli cross path Mwezi February
Thank You All 🙏🏿🫡
MY MARCH RESOLUTION
☑️ 2-3 Books
☑️ 10+ YouTuber Videos and Podcasts
☑️ Attend as Many events as available and possible
☑️ 31 Days Journaling
☑️ 20 days of intense physical exercise
☑️ Final Preparation to launch WL officially
☑️ 3 Days of Reset (Total Rest and Reset)
☑️ 3 -5 Social Media Post excluding this
March resolution sio constant itabafilika kulingana na uhitaji na circumstances zitakazojitokeza
Shukrani kwa kuendelea kufuatilia safari yangu ya
#LearnConnectExecute
Leo imetimia miaka 7 tangu tuanze kusherehekea maisha ya Ruge Mutahaba, Jasiri Muongoza Njia, Scofield, Mastermind,
Licha ya Miaka mingi kupita, maumivu Bado ni mabichi as if ilikuwa Jana tu,
Ilikuwa ndoto kwangu kukutana nae siku moja lakini ndoto haikuweza kuwa kweli, lakini maisha yanasonga, binafsi naendelea kutumia maisha yake kama shule na ninaendelea kufanya kuwa Mwalimu kwangu kwasababu naamini Nina mengi sana ya kujifunza
Kama alivyotutaka tusilie bali tusherekee maisha yake, Mimi huwa nasherekea kwa kurudi kwenye archive zake kuchota madini
#Ruge7 ni mambo 7 ambayo nimejifunza kutoka kwenye Legacy yake,natumaini na wewe una la kujifunza hapo
Endelea kupumzika kwa amani #JasiriMuongozaNjia
#Ruge7
📌
14/02/2026
Jana nilishiriki Dam Dam Marathon kwa mara ya kwanza tangu imeanzishwa mwaka 2021
2022-2025 nilikuwa na nafasi na uwezo wa kushiriki lakini nilikuwa nikikwepa kushiriki kutokana na uzembe na ule woga wa kuhisi kuwa kushiriki Dam Dam Marathon sio vitu vyangu, au Dam Dam Marathon sio sehemu yangu ni sehemu ya watu flani flani na kwamba sistahili kuwepo kule,
Hayo mawazo yamekuwa yakinirudisha nyuma mno
Lakini leo ninafuraha kwasababu ninaamini maisha yangu hayatakuwa the same baada ya kushiriki Dam Dam Marathon
Shukran brothers, @remmymbowa_@marcel__kitabu@praf.paparaz@johnjakson_tz kwa kuninyooshea, nime experience na kujifunza mengi sana.🙏🏿
Na tukio langu bora Dam Dam ni kuzungumza na brother @JohnJackson_tz , ulikuwa wakati mzuri sana kuzungumza nae tumezungumza vitu vingi sana kuhusu kazi na maisha kiujumla JJ yeye ananyoosha kupitia WhatsPopN ya XXL , Ghetto Podcast na Drip check
Kitu special kuhusu tukio hili la kuzungumza na brother JJ ni kwamba, kwanza ni mtu mpya ambae sikuwahi kuzungumza nae kabla japo nilikuwa namuona,Kumfahamu na Kumfuatilia kama brother na Role Model kwangu na kwa vijana wengi sana, kilichokuwa kinamisi siku zote ni mimi kuanzisha conversation in which Leo kimetokea, na brother JJ was very humble and receptive
Na matokeo ya mazungumzo yetu nimemuomba nihudhurie set ya @ghettopodcasttz , amenyoosha na siku moja nitamjoin set na nina hakika nitajifunza mambo mengi zaidi
Thanks brothers kwa kuniyoshea
TAKE.
Sehemu ambayo unahisi sio sehemu yako au unahisi woga kwenda ndo sehemu unayopaswa kwenda na ndio funguo ya kukufungua kwenye minyororo ya kujifungia ndani
Binafsi Leo nimefanikiwa kufungua mnyororo ambao ulikuwa nizuia nisi show up
DAM DAM yangu ya kwanza kushiriki imenikutanisha na watu wengi wapya zaidi ya nilio Network nao for the whole past year,
Kama nilivyo ahidi nitaendelea kwenda kokote penye connection na maarifa,
Maeneo uncomfortable kwangu ndo maeneo ambayo yametengenezwa kwajili yangu so, lazima niyatumie vizuri kukua kimaarifa na kijamii
"One moment can change a day,one day can change a life, One life can change a world - Buddha
Dam Dam Marathon was that One Moment for me
January 8 nilianza ku document maisha yangu ya kila siku
• Kila detail bila kuacha kitu
Kiukweli ni kitu ambacho kimenifanya nigundue na kujifunza vitu vingi sana ambavyo vilikuwa vinaendelea kwenye maisha yangu ambavyo vingine vilikuwa vina cost future ya yangu bila hata mimi mwenyewe kujua.
Kupitia journaling:-
Nimegundua nina muda mwingi sana (24 hrs is a lot kwa kweli), Lakini kwa bahati mbaya sikuwa nautumia vizuri,baada ya kuanza ku journal nimegundua kuwa ni muda ambao kama nikiutumia inavyopaswa ninaweza kufanya chochote, Tena bila presha
Masaa 24 niliyonayo sasa ni the same na niliyokuwa nao mwanzo lakini kwasababu matumizi yake kwa sasa yako controlled & tracked kila sekunde kwenye maisha yangu ina matter
Siku zote bila kujua muda wako unatumika kwenye nini exactly inakuwa ngumu ku control au ku track, lakini baada ya kuanza ku journal nimejua exactly muda wangu mwingi ulikuwa unapotelea wapi na kuanzia hapo nikaanza kufanya time allocationa na improvement to make sure every ticking second inaongeza kitu kwenye maisha yangu
Mfano, niligundua muda wangu mwingi ninautumia social media ku doomscroll kwenye vitu ambavyo havikuwa na msingi so nikafix kuanzia hapo kutoka kutumia zaidi ya masaa 6 social media mpaka kuwa na limit ya Max Saa moja kwa siku na ku allocate muda mwingine kwenye vitu vya muhimu zaidi kama kusikiliza podcast, Kufanya research,Kuandaa contents,Kufanya reflections nk
Lakini pia kuna vitu nilikuwa nafanya bila kufikiria athari ambazo zitatokea kwenye maisha yangu in a long run,nilikuwa nachukulia mambo poa lakini Baada ya kuanza kutrack kila kitu ninachokifanya kwenye siku kina matter, coz najua kuna sehemu tu either kitanipa advantage au kunipa disadvantage
So journaling imenifanya niwe na control kamili maisha yangu, inanilazimisha kuwa makini ku prioritize vitu na ku virtualize aftermath ya vitu hata kabla sijavifanya ili kuepuka kufanya makosa mengi ambayo yanaweza kunicost mbeleni
So with just Journaling I regain full control of my life
Bila shaka hata wewe unatamani kuwa na control kamili ya maisha yako,
Anza kujournal sasa, Utajifunza vitu vingi zaidi kupitia safari hiyo
#LearnToEarn
#LearnConnectExecute
• 600+ Min's of brain feeding
•1,800 Mins of Reflection (Journaling) Next Post
Kwenye macho yako inaweza kuonekana ni archivement kidogo,lakini kwangu naona ukubwa wa namna ambavyo nimefanikiwa kushift mindset yangu
Kwangu hilo lina matter zaidi.
Progress ninayo Iona ni matokeo kuamua kuchukua hatua za makusudi kabisa, ndio maana sijali sana kuhusu perfect ninachokizingatia zaidi ni progress
Nmekuwa niki plan na ku strategize vitu for more than 3 years lakini sikuwahi kumove an inch,lakini kwa actions za mwezi mmoja tu naanza kuona progress
That's a huge WIN to me
James clear anasema "We don't rise at the level of the goal, We fall at the level of the system"
I had goals, I didn't have system to archive them, and that changed this month, this year ambapo nilia amua kuchukua hatua, and here we are naanza kushare progress zangu kama ambavyo nili ahidi kwenye post zilizopita
#JanuaryLearnRecap
In January nimetumia dakika 740 + sawa na masaa 12 kuangalia podcasts, na kusoma kitabu cha #AtomicHabit by James clear
Licha ya ubize wa njaanuary, nimefanikiwa ku archive hayo,sio kikubwa sana lakini it means a lot to me, kwasababu I know how hard it was, lakini Bado sijaridhika, I demand more from myself
Na ili ku improve zaidi, ninaji challenge ku triple what I have archived in January,this month I will do even better
Lengo kubwa ni kujifunza na ku improve kwa kufanya ndio Sababu nina share slides hapa ili hata wewe ambae unanifuatilie uweze kujifunza kitu
Ninaendelea kiyasaka maarifa kadri nitakavyo weza, pa kuweka muda nitaweka, pakuweka pesa nitaweka, pa kuuliza nitauliza, pa kuomba guidance nitaomba, I have nothing to lose, I have much to gain
My next pick from my booklist is "The Power of Your subconscious Mind" By Joseph Murphy
Hiki kitabu nina story nacho, ninakisoma huku nikiwa guilty, siku moja nita simulia hiyo story, kuna kitu utajifunza kama ambavyo mimi nimejifunza tena the hardway
Ninaendelea kujifunza, Kufanya na ku Improve
Bila shaka hata wewe January yako haikupotea hivi hivi, unaweza kushare kwenye comment vitu gani umeviarchive ili na sisi tujifunze
Endelea kuwa karibu na @learnwithsako tujifunze zaidi
#LearnConnectExecute