INTERVIEW SAFI SANA NA BALOZI WA URUSI NCHINI TANZANIA!
——
BALOZI WA URUSI AELEZA USHIRIKIANO UNAOKUA KATI YA TANZANIA NA URUSI
Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, ameeleza kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi unaendelea kupanuka katika nyanja za biashara, uwekezaji, nishati, elimu na utalii.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum na @djsma255 , Avetisyan alisema Kamisheni ya Kiserikali ya Biashara na Mahusiano ya Kiuchumi tayari imefanya mikutano miwili yenye mafanikio jijini Dar es Salaam na St. Petersburg, ambapo zaidi ya wajumbe 50 wa Kitanzania — viongozi na wafanyabiashara — walishiriki na kuunganishwa na wenzao wa Urusi.
Balozi alibainisha pia maendeleo makubwa katika sekta ya nishati, akitaja uzinduzi wa kituo cha kuchakata madini ya nyuklia mkoani Ruvuma na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano na shirika la Rosatom.
Mradi huo utasaidia uhamisho wa teknolojia, ajira mpya, na mafunzo ya Watanzania nchini Urusi. Aidha, makampuni ya Urusi yanahusisha pia miradi ya uwajibikaji wa kijamii kama kuchimba visima, kusaidia shule na hospitali.
Katika sekta ya utalii, Avetisyan alisema kundi la waendeshaji wa biashara ya utalii kutoka Urusi linatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ziara ya wiki moja kutembelea hifadhi na Zanzibar, hatua itakayoongeza idadi ya watalii wa Kirusi.
Pia alihimiza Watanzania kuigundua Urusi kama kituo cha utalii na kuongeza kuwa idadi ya watalii ikiongezeka, safari za moja kwa moja kati ya nchi hizo zinaweza kurejeshwa.
Akihitimisha, Balozi alionyesha matumaini kuwa miradi mipya itaongezeka zaidi na ushirikiano utaendelea kukua.
Watu wema ni riziki kama riziki nyingine muombe mungu akupatie watu kama hao na akuepushe na watu wabaya @djsma255
Full interview ipo kwenye YouTube channel ya #96link
#96link
#tunakuunganisha