DHARURA KUBWA!
Tunayo furaha kubwa kuwataarifu kwamba filamu fupi yetu, Dharura, imechaguliwa rasmi kushiriki katika Tamasha la Filamu la Lift-Off Sessions, jukwaa la kimataifa linalowaunganisha watengenezaji wa filamu kutoka duniani kote.
Lift-Off Sessions si maonesho ya kawaida wala tamasha la kawaida. Ni platform maalum yanayowahamasisha watengenezaji wa filamu kushirikiana, kujifunza na kuunga mkono kazi za wenzao.
Kama washiriki, filamu yetu itaoneshwa kwa hadhira ya kimataifa na pia tutakuwa na nafasi ya kushindania tuzo zitakazosaidia kukuza safari yetu ya filamu.
Hii ni hatua kubwa sana kwetu!
#LiftOffSessions #FilmSelected #Notepad #AfricanCinema #GlobalStage