Siku yangu ya kuzaliwa imenikumbusha kuwa kuchelewa si kushindwa. Mungu bado yupo kazini juu ya maisha yangu. Umuhimu wa maisha haupimwi kwa idadi ya miaka, bali kwa kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.
Kuna nyakati nilitamani kufanya mengi, lakini muda na mazingira vilionekana kunitupa mkono. Hata hivyo leo, katika siku yangu ya kuzaliwa, nachagua kuamini kwamba bado Mungu hajamaliza nami. Kama ilivyoandikwa katika Yeremia 29:11, Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
Leo najitakia neema ya kuanza upya, nguvu ya kusimama tena, na imani ya kuendelea kusubiri wakati sahihi wa Mungu. Kwa maana Mhubiri 3:11 inasema, Amefanya kila kitu kuwa kizuri kwa wakati wake.
Naamini bado kuna milango itafunguka, ndoto zitatimia, na yale niliyowahi kuyaombea kwa machozi yatageuka kuwa ushuhuda. Warumi 8:28 inasema, Katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema.
Happy Birthday to me. Mwaka huu mpya wa maisha yangu naubeba kwa imani, matumaini, na uhakika kwamba Mungu bado anaandika Historia nzuri ya maisha yangu. 🎂
@sutiyangu