🔵ARUSHA-TANZANIA
*RC MAKALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA UCHUMI NA MAENDELEO WA URUSI*
- *_RC Makalla akaribisha watalii na wawekezaji kutoka Urusi kuwekeza katika sekta ya utalii_*
- *_Wapendekeza ushirikiano wa Mkoa wa Arusha na Mkoa mmoja wa Urusi_*
- *_Waziri Reshetnikov avutiwa na ukarimu wa watanzania, Amani na utunzaji wa vivutio vya utalii_*
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumamosi Mei 16, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Serikali ya Shirikisho la Urusi ulioongozwa na Waziri wa maendeleo ya uchumi Mhe. Maxim Gennadyevich Reshetnikov akiwakaribisha watalii na wawekezaji kutoka Nchini Urusi kuja kutalii na kuwekeza katika sekta ya utalii Mkoani Arusha.
Katika mazungumzo ya Viongozi hao yaliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Arusha, Viongozi hao pia wamejadiliana na kupendekeza ushirikiano wa Mkoa wa Arusha na Mkoa mmoja wa Urusi ili kushirikiana katika sekta mbalimbali za maendeleo pamoja na kubadilishana uzoefu ili kunufaisha pande hizo mbili kwa maslahi ya maendeleo na ustawi wa wananchi wa Mkoa wa Arusha na Mkoa utakaochaguliwa kutoka Nchini Urusi.
Kwa upande wake Mhe. Reshetnikov amemshukuru Mhe. Makalla kwaniaba ya serikali ya Tanzania kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na ujumbe wake tangu alipofika Mkoani Arusha jana Mei 15, 2026, akionesha pia kuvutiwa na ukarimu wa Watanzania, amani iliyopo Nchini pamoja na utunzaji mkubwa wa Vivutio vya utalii vilivyopo Mkoani Arusha.
Katika kikao hicho Mhe. Makalla ameshiriki pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Toba Alnason Nguvila na Maaafisa wa taasisi za serikali zilizopo Mkoani Arusha huku upande wa Waziri Reshetnikov akiambatana na Balozi wa Urusi Nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetisyan na Maafisa wengine kutoka serikali ya Urusi, Mhe. Reshetnikov akitembelea na kutalii pia kwenye hifadhi ya Taifa ya Arusha jana Ijumaa akiambatana na ujumbe wake.
🔵ARUSHA-TANZANIA
Miss Grand Arusha, Prisca Lyimo, amepokelewa kwa shangwe na nderemo na wakazi wa Jiji la Arusha wakiwemo madereva bodaboda, vijana na wananchi mbalimbali, katika mapokezi yaliyojaa hamasa kubwa na furaha, kabla ya kuwasili katika ofisi za serikali kwa ajili ya kuendelea na ratiba rasmi ya ziara yake.
Mapokezi hayo yameonesha uzalendo na mshikamano wa wananchi wa Arusha, ambapo Prisca Lyimo alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi waliojitokeza kumlaki kabla ya kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Baada ya mapokezi ya wananchi, Miss Grand Arusha aliwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambako alipokelewa rasmi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Dkt. Jacob Julius Rombo pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Akizungumza katika mapokezi hayo, Dkt. Rombo amesema mashindano ya urembo yamekuwa chachu ya kuwawezesha mabinti wengi kujipatia kipato, kukuza vipaji vyao na kuwaepusha kujiingiza katika vitendo visivyofaa katika jamii.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika kuwawezesha vijana kupitia sera, taasisi na programu mbalimbali za maendeleo.
🔵ARUSHA-TANZANIA
Mapema Leo May 15 ,Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Dkt. Jacob Julius Rombo, amempokea Miss Grand Arusha, Prisca Lyimo @prisca__lyimo ofisini kwake.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Dkt. Rombo amesema uwepo wa mashindano ya urembo umefungua fursa kwa mabinti wengi nchini kujipatia kipato pamoja na kuwaepusha kujiingiza katika mambo yasiyofaa katika jamii.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutambua mchango wa vijana katika maendeleo ya taifa kwa kuunda na kuimarisha wizara pamoja na taasisi zinazowalenga vijana, ikiwemo Ofisi ya Rais inayoshughulikia maendeleo ya vijana chini ya Mhe. Joel Nanauka.
Katika hatua nyingine, Dkt. Rombo alimpongeza Prisca Lyimo kwa hatua aliyofikia na kumkaribisha Wilaya ya Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Joseph Mkude.
Kwa upande wake, Miss Grand Arusha, Prisca Lyimo, alishukuru kwa mapokezi hayo na kuishukuru serikali kwa kutambua mchango wa vijana katika Taifa na kuahidii kuendelea kuitangaza Arusha pamoja na kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiletea maendeleo.
🔵ARUSHA-TANZANIA
Ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii nchini kote ,Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Dkt. Jacob Rombo amwataka wananchi kuunga mkono juhudi za ukusanywaji wa mapato kwa kulipa kodi ili kufikia lengo la kuimarisha huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Hospitali ya Ngazi Wilaya Kaloleni jijini Arusha Dkt.Rombo amesema ni vyema kuunga mkono zoezi la ulipaji kodi kwani jambo hilo ndio chachu ya upatikanaji wa huduma bora ikiwemo za Afya.
🔵ARUSHA -TANZANIA
Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Dkt Jacob Julius Rombo amewataka wajawazito wote kuhakikisha wanahudhuria kliniki na kufika kwenye vituo vya afya mara kwa mara katika kipindi chote cha ujauzito hadi kujifungua kwa usalama.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya Kaloleni jijini Arusha Dkt. Rombo amesema hatua hiyo itasaidia kulinda afya ya mama na mtoto pamoja na kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa ujauzito na kujifungua.
@ikulu_mawasiliano
🔵ARUSHA-TANZANIA
ARUSHA, TANZANIA
DKT JACOB JULIUS ROMBO AZINDUA RASMI HOSPITALI YA
KALOLENI NGAZI YA WILAYA.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Dkt Jacob Julius Rombo leo amezindua rasmi Hospitali ya Kaloleni ngazi ya wilaya jijini Arusha kufuatia Kituo cha Afya Kaloleni kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ngazi ya wilaya kupitia maboresho makubwa yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na mamia ya wananchi, viongozi mbalimbali pamoja na wataalamu wa afya waliojitokeza kushuhudia hatua hiyo muhimu katika kuboresha huduma za afya ndani ya Jiji la Arusha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt Rombo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha amesema Serikali imeendelea kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na za kisasa karibu na maeneo yao.
Amesema kupandishwa hadhi kwa Kituo cha Afya Kaloleni na kuwa Hospitali ya Wilaya kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu pamoja na kupunguza changamoto kwa wananchi waliokuwa wakilazimika kufuata huduma mbali na
maeneo yao.
Aidha amewapongeza wataalamu wa afya kwa juhudi
wanazoendelea kuzifanya katika kuwahudumia wananchi huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma kwa maslahi ya wananchi.
Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo wakisema ni mafanikio makubwa kwa sekta ya afya
@ikulu_mawasiliano
🔵ARUSHA-TANZANIA
Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Dkt Jacob Julius Rombo leo amezindua rasmi Hospitali ya Kaloleni ngazi ya wilaya jijini Arusha kufuatia Kituo cha Afya Kaloleni kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ngazi ya wilaya kupitia maboresho makubwa yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na mamia ya wananchi, viongozi mbalimbali pamoja na wataalamu wa afya waliojotokeza kushuhudia hatua hiyo muhimu katika kuboresha huduma za afya ndani ya Jiji la Arusha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt Rombo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha amesema Serikali imeendelea kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na za kisasa karibu na maeneo yao.
Amesema kupandishwa hadhi kwa Kituo cha Afya Kaloleni na kuwa Hospitali ya Wilaya kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu pamoja na kupunguza changamoto kwa wananchi waliokuwa wakilazimika kufuata huduma mbali na maeneo yao.
Aidha amewapongeza wataalamu wa afya kwa juhudi wanazoendelea kuzifanya katika kuwahudumia wananchi huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma kwa maslahi ya wananchi.
Wananchi waliojotokeza katika hafla hiyo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo wakisema ni mafanikio makubwa kwa sekta ya afya katika Jiji la Arusha.
@samia_suluhu_hassan@owm_tz@tamisemi@wizara_afyatz@gersonmsigwa
🔵ARUSHA-TANZANIA
WANANCHI WAMIMINIKA KATIKA UZINDUZI WA KAMBI YA MATIBABU BURE KALOLENI
Mamia ya wananchi wamejitokeza katika kituo cha afya kaloleni kilichopandishwa hadhi kuwa Hospitali yngazi ya Wilaya jijini Arusha kushiriki hafla ya uzinduzi wa kambi maalum ya matibabu bure ya siku mbili inayofanyika hospitalini hapo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Dkt Jacob Julius Rombo anayemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Hafla hiyo imekusanya wananchi, viongozi pamoja na wataalamu wa afya huku lengo kuu likiwa ni kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi.
Kambi hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya nchini, ambapo Hospitali ya Kaloleni imeendelea kunufaika na maboresho makubwa baada ya kupandishwa hadhi kutoka kituo cha afya na kuwa Hospitali ya Wilaya.
Wananchi waliojitokeza wameonekana kuwa na hamasa kubwa ya kupata huduma mbalimbali za afya zitakazotolewa bure katika kipindi chote cha siku mbili za kambi hiyo.
@ikulu_mawasiliano
Arusha, I’m coming home! 👑
I’m Prisca Lymo, your newly crowned Miss Grand Arusha 2026. For the first time since the crown was placed on my head, I’m heading back to the city that raised me — not just as Prisca, but as your Queen, ready to carry Arusha’s name with pride to Miss Grand Tanzania.
This homecoming is for YOU. For every dreamer in Arusha who dares to believe big. Let’s celebrate together!
Join me:
📍 Arusha Airport
📅 15th May 2026
⏰ 1:00 PM
Come with your energy, your flags, and your love. Let’s make Arusha proud together.
#MissGrandArusha2026 #TheCrownReturnsHome #ArushaPride #RoadToMissGrandTanzania
See you at the airport, Arusha!
Special Thanks
@makuyuniwildlifepark@tawa_tanzania@kiliseasons@dc_wilaya_arusha
🔵ARUSHA-TANZANIA
Leo may 12 katibu tawala wilaya ya Arusha dkt. Jacob Rombo kwaniaba ya Katibu Tawala wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Mkude amehudhuria mkutano wa kilele siku ya maadhimisho ya wa uguzi duniani ambapo mgeni rasmi katika mkutano huo ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejenti ya Utumishi wa Umma Mhe.Regina Qwaray Ndege uliofanyika kitaifa Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC.
Akizungumza katika mkutano huo akitoa salamu za Mkoa na Wilaya Dkt. Rombo mewataka watumishi kumtanguliza mungu katika kazi zao ili kuleta matokeo chanya katika kazi zao ambapo amefafanua ni faraja kwa mtumishi endapo mgonjwa amerejea kwenye hali yake ya kawaida na si vinginevyo akiwasisitiza kufanya kazi kwa moyo,bila kusita,kuogopa na kuona haya pamoja na kumtegemea mungu.
Mwisho akizungumzia ahadi za Katibu Tawala wa mkoa kwa Wauguzi ikiwemo kutembelea vivutio vya Utalii Arusha ,Dkt. Rombo pia ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia utekelezwaji wa zoezi la Nyama choma kama lilivyoelkezwa na Katibu tawala Mkoa kwa wauguzi hao.
@ikulu_mawasiliano