Kwenye forex trading industry kuna taarifa nyingi zisizo sahihi sana, na mara nyingi hizi huwafanya beginners kuchukua muda mrefu sana kujifunza na kuelewa trading vizuri.
Wewe unahisi beginners wengi wanakosea wapi kwenye forex trading...?
Huu ni ujumbe kwako kijana mwenzangu. Najua kuna muda unakata tamaa na mambo yanaenda tofauti kabisa na ulivyotarajia. Najua bado hujakata tamaa kabisa, ila kuna kipindi unashindwa kuona ni wapi utatokea kutokana na ugumu wa hali ilivyo sasa.
Siandiki haya kwa lengo la kumtia moyo kila mtu anayesoma. Ila kuna usiku mmoja utakaa peke yako kabisa, brother/sister. Marafiki zako na hata watu wako wa karibu watakua mbali na wewe. Na siku hiyo, wewe mwenyewe ndiyo utakua muamuzi wa mwisho wa maisha yako na mapito yako.
Kwa sasa nipo kwenye phase ya maisha ambayo ni ngumu sana kumuelezea mtu. Kuna muda hata sijui kama nimefanikiwa au bado natafuta njia ya mafanikio. Unakaa unajiuliza kwanini umechelewa sana, wakati ulioanza nao harakati za maisha tayari wapo mbali. Ila nao pia wanapambana na mapito yao kwa namna tofauti.
Lakini huwa nakaa na kujiambia kuwa hizi ni phases za maisha. Hakuna siku utakaa na kusema kila kitu kimekaa sawa asilimia mia moja. Mara nyingi ukihisi mambo yanaanza kwenda sawa, ndiyo kazi ngumu zaidi ya ku-maintain hiyo phase inaanza. Waliopitia hizo hatua ndiyo wanajua uzito wake.
Kwa sisi vijana ambao bado tupo chini, ni kawaida kuwa na kiu, mawazo na stress za kujiuliza,
-Kwanini sipati hela?
-Kwanini mambo yanazidi kuwa magumu?
-Kwanini mpenzi wangu hanielewi tena?
-Kwanini hata nyumbani hawaonekani kunielewa? N.K
Lakini hayo yote yasiwe sababu ya kusimama katikati ya giza na kuanza kurusha mawe ovyo. Maisha yana vipindi vyake.
Nimewahi kupitia vipindi vigumu sana vya maisha, na naamini vipindi hivyo hujirudia haijalishi upo hatua gani. Ila tofauti inakuja kwenye namna unavyobeba hali zako, namna unavyopambana nazo, na namna unavyoendelea kufanyia kazi vision yako hata ukiwa huoni matokeo kwa haraka.
Kadri muda unavyoenda, vision inaanza kuwa clear zaidi. Unaanza kuona solutions nyingi ambazo zamani hukua hata unazifikiria.
Najua upo kwenye kipindi kigumu kwa sasa, usijione umepotea. Inawezekana hii ni sehemu ya safari inayokujenga kuwa mtu mwingine kabisa mbele ya maisha.
Forex ni moja ya ujuzi mgumu sana kuumaster.
Nimelishuhudia hilo katika safari yangu yote ya trading.
Inahitaji kudhibiti mambo ambayo yanatokana na hisia za ndani,
kama vile:
• Emotional control
• Proper risk management
• Patience
• Consistency
Tatizo ni kwamba wengi huingia bila maandalizi ya haya yote.
Ndiyo maana wengi huishia njiani, wakitafuta wa kumlaumu:
“Mtu fulani kanifelisha”
“Watu hawatusaidii”
Lakini ukweli unabaki palepale,
Kiwango kikubwa cha kushindwa hakimaanishi Forex si halali, bali kinaonyesha ugumu wake.
Kama unaingia Forex, ingia kwa lengo la kujifunza skill.
Kwa sababu ukianza kukimbiza pesa kabla ya maarifa,
unajiweka kwenye nafasi ya kupotoshwa kirahisi.
Kila mtu akitangaza “service” fulani, unajikuta unakimbilia.
Na mwisho wa siku, unageuka kuwa mtazamaji wa wengine wakifanikiwa.
Maisha huwa yanatufundisha kwa njia ambazo hatutarajii.
Wakati mwingine si mafanikio yanayotujenga, bali ni makosa na majuto tunayopitia njiani. Lakini, hakuna mtu anayekua bila kupitia maamuzi magumu aliyoweza kuyabadilisha kua matokeo yenye positive impact kwake na familia yake.
Kuna kipindi unafanya kitu ukijiamini kabisa, unaamini uko sahihi, lakini muda unavyoenda ndipo unaanza kuona ulipokosea. Hapo ndipo akili inaanza kufanya kazi tofauti.
Unaanza kuelewa vitu kwa undani zaidi, unajifunza kuvumilia, na zaidi ya yote, unajifunza kujithamini. Tofauti na hapo kuna pressure kubwa sana ndani inayoweza kukuangusha vibaya, na kukutoa kwenye malengo mazuri.
Majuto si ishara ya kushindwa kwa ninavyojua, maana hata Leo ninajutia muda mwingi niliochezea bila kubadilika, kwa sasa ninaelewa ni sehemu ya mchakato wa kukua, kwasababu nilipo Leo, Jana nilikua sehemu mbaya zaidi psychologically.
Majuto yanatufanya kuwa makini zaidi, kuwa na subira, na kufanya maamuzi bora zaidi siku zijazo. Bila zile moments za kujilaumu, huwezi kufika kwenye level ya kujielewa vizuri.
“Majuto ni mjukuu” hii ni methali tumekua tukiisikia mara kwa mara, ilinijia sana akilini kipindi nimeanza kupingana na wazazi ili nifuate plan zangu, baada ya mambo kuyumba nilijihisi pengine ni laana, lakin hadi nilipoanza kuona sehem niliyochagua ni sahihi na inanibadilisha kunifanya kua bora zaidi, ilihitaji mchakato wa muda kidogo na kujitoa kwa moyo wote kimya kimya.
Kwa hiyo kama unapitia kipindi ambacho unajilaumu au unajutia baadhi ya maamuzi yako, jua tu uko kwenye hatua ya kubadilika. Usikimbie hiyo hali, ipokee, jifunze, halafu songa mbele ukiwa na akili mpya.
Maisha hayahitaji ukamilifu, yanahitaji mtu anayeweza kujifunza kutokana na kila alichopitia na kuamua kuwa bora zaidi kesho.
Wanasema “Maisha huwa yanahitaji some few regrets alafu unaanza kutumia akili.”
Ukiona ninatabasamu, ujue tu niko sawa na nina amani moyoni.
Ukiona ninazungumza na watu, elewa tu nina uwezo wa kuongea na yeyote, siku yoyote.
Ukiona nimenyamaza, ujue kuna mambo nimeyapa muda, nayatafakari kwa kina zaidi.
Ukiniuliza kitu nikakosa majibu, tambua tu muda huo sina jibu, lakini nikibaki peke yangu, nitalitafuta hadi nilipate.
Nikikujibu haraka bila hata kufikiria sana, ujue hilo ni eneo nililolizoea nina uzoefu nalo wa muda mrefu.
Nikikudharau, hata wale muhimu kwenye circle yangu watakutenga.
Lakini nikikupokea, basi ujue umepewa nafasi na circle yangu yote itakusikiliza.
Mimi bado ni mwanafunzi wa wengi,
Lakini nimezungukwa na watu ambao hawapendi nishindwe kwenye mitihani ya maisha.
Ukiniona nakosea ukaniweka sawa, nitakuheshimu bila kificho, sipendi unafiki.
Kuna muda hata mimi napunguza kasi kwenye maisha, au naonekana mvivu kwa sababu fulani,
Lakini linapokuja suala la kujaribu na kuleta matokeo popote, huwa nafanya kazi kweli, na huwa nadeliver.
Nina mengi ya kujifunza kutoka kwako,
Na nina sababu ya kumheshimu kila mtu ninayekutana naye.
Katika kujenga mfumo imara na sustainable trading environment,
hatuishii kwenye strategy na execution pekee - tunajenga pia departments zinazohakikisha consistency na longevity,
Ndani ya system yetu kuna department muhimu sana – Risk Management Department,
Hii ndiyo department inayohakikisha capital inalindwa, risk inadhibitiwa, na kila trader anafuata mfumo sahihi wa execution bila kuathiriwa na emotions,
Inasimamia risk exposure, discipline, na overall trading behavior ya floor nzima,
Kuanzia kusimamia mchakato wa tracking ya data, hadi kuandaa reports za kila siku na kila wiki kuhusu risk management ya kila trader,
Hii inarahisisha mentors kufanya sessions zenye direction sahihi, kutoa usimamizi wa karibu, na kusaidia traders kuboresha performance yao kulingana na risk management data halisi,
Let’s experience professional side of trading
Juzi nilipita sehemu ya jilan kwenye mitaa ninayokaa, nikawa nadambua kachori buana.
Faza mmoja, akasogea na wenzake wakawa wanachakata pweza na mchuzi wake. Yule faza alikuwa anawapigisha story wenzake, akiwambia plan zake. Plan ambazo, ukimuangalia, hazionekani zenye kuendana na hali yake ya sasa 😑.
Ni ndoto ambazo, sisi vijana wenye miaka 20, ndio tunazifukuzia. Lakini faza bado anazifikiria na anataka kuzitimiza.
Alisema kuhusu miamala iliyokatiza mikononi mwake kwa kipindi chote cha maisha yake, ila akaishia kushindwa kufanikisha baadhi ya malengo yake. Nilijikuta nikiwaza kitu akilini 😁.
Nikaanza kufikiria, “🤔kama huyu faza amekuwa akipanga hivi kwa miaka 20+ iliyopita, hiyo miamala yote aliyokuwa nayo, alitumia kufanya nini sasa?” Pale pale ikanipelekea kurequest report ya transaction zangu za NMB… duh!! Question marks zilianza kuja kichwani mwangu. Nikajipigia hesabu, nikajiuliza: “Ina maana mimi pia, ikiwa sitachukua hatua sasa, nitakuwa bado nikifukuzia ndoto zangu baada ya miaka 20 ijayo?” Hii ilikuwa hofu kidogo, ndoto zikiwa zinaonekana kuwa mbali.
Kuna kale ka msemo, “Ah, MUNGU NDIO ANAPANGA YOTE 😅.”
Nilipokuwa nataka kuondoka, nikamsikia yule faza akiwaaga marafiki zake,
“Ah, wajomba ngoja niwahi home nikaangalie Tamthiliya ya Otomani.” 😅
Sikujali sana, Ila Niliwahi pita mgahawa mmoja sinza, nikaona heading ya jina hilo kwenye tamthiliya moja iliyotafsiliwa kwa Kiswahili. Nikawaza tu, Labda ndoto zake zimechelewa kufanikiwa si kwa sababu hakujituma, bali kwa sababu ya vitu alivyokuwa amevipa kipaumbele.
Anaonekana sio mtu mwenye maisha magumu, lakini bado anawaza kujenga. Fikilia 50+ bado anazifikiria ndoto zake, akitaka kuwa na gari nzuri, nyumba nzuri n.k.
Plan ambazo sisi madogo tunapaswa kuzifikiria sana pengine.
kiukweli sio kosa kwake kuendelea kuziweka kwenye target zake. Lakini nilichopata pale ni somo zuri kwangu, ndoto hazina umri. Mtu akiwa na miaka 50, au zaidi, bado anaweza kuwa na ndoto na kuzipigania. Sometimes, tatizo ni mfumo wa maisha aliyokuwa nao kufikia hapo.
Unajua… kuna kipindi nilikuwa naishi maisha ya kujifariji sana.
Nilikuwa najua kabisa ndani yangu kuna kitu kikubwa zaidi naweza kufanya, lakini nilikuwa nakisukuma mbele kila siku. Nilijiambia bado kuna muda, nilijiambia nitaanza kesho, wiki ijayo, au nikijipanga vizuri zaidi. Lakini sikuwa hata najipanga nilikuwa naahirisha maisha yangu mwenyewe.
Na matokeo yake hayakuja ghafla… yalikuja polepole.
Nilianza kuhisi kama kuna kitu kinakosekana. Niko busy, nafanya mambo yangu, na hata watu wanaweza kuona kama nasonga mbele., lakini ndani kabisa nilikuwa najua sipo pale napaswa kuwa. Kuna ile sauti ya ndani ilikuwa inaninyima amani ikiniambia, “Cheleo unazingua… unaweza zaidi ya hapa?.”
Na kadri muda ulivyokuwa unapita, ndivyo nilivyoanza kujilaumu. Unaanza kujiuliza maswali mazito “Ingekuwaje kama ningechukua hatua mapema?”, “Kwa nini nilikubali kubaki sehemu ambayo hainijengi?”, “Kwa nini niliogopa sana kuanza?”
Kitu kibaya zaidi ni haya majuto hayapigi kelele ili watu wasikie wakusaidie, yanakaa kimya ndani yako, lakini yanakula confidence yako polepole. Unaanza hata kujiona wa kawaida tu, wakati ukweli unajua kabisa wewe si wa kawaida.
Nimewahi kufika point nikajikuta nimechoka, si kwa sababu nimefanya kazi sana, bali kwa sababu nimekuwa nikikimbia kile nilichopaswa kufanya.
Na hapo ndipo nilipogundua kitu,
kupuuza kile kinachokutoa ubora wako siyo tu unajinyima mafanikio., unajinyima amani na unatengeneza hofu ambayo kuitibu ni ngumu.
Kwa sababu hakuna kitu kinachoumiza kama kujua una uwezo, lakini hauutumi.
Sasa hivi najitahidi kubadilisha hilo. Si kwamba hofu imeisha, bado ipo. Lakini nimeacha kusubiri nijisikie tayari. Nimeanza kufanya vitu hata nikiwa Nina ogopa au hata nikiwa sina uhakika wote.
Kwa sababu nimeelewa kitu kimoja muhimu sana,
maisha hayanisubiri nipate ujasiri, yanaendelea tu kusonga mbele.
Na sitaki kufika sehemu ambapo nitatazama nyuma na kusema, “Ningejaribu tu…” 😔
Welcome to the professional side of trading.
Trading sio tu chart na entries… ni mazingira, nidhamu, na watu unaokaa nao kila siku.
Intelligence Floor ni mahali ambapo traders wanakutana kujifunza, kuchambua masoko, na kukua pamoja kama professionals.
welcome @intelligencefloor
No one has ever succeeded without experiencing failure. Failure teaches lessons that success often cannot.
HRM @intelligencefloor
Cc. @baraka_photography