SAUT DIGITAL

@sautdigital

Huu ni ukurasa rasmi wa SAUT Media (SAUT Digital na Radio SAUT FM Stereo)
Followers
2,265
Following
1
Account Insight
Score
28.74%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
2265:1
Weeks posts
leahmushi_ a proud alumna of @saut_mwanza is among the professionals representing Tanzanian excellence on the international stage through her work with the United Nations. Her journey reflects the power of education,confidence and determination nurtured within the walls of @saut_mwanza Your future can reach beyond borders too. KARIBU TULIJENGE JIJI LA MUNGU
198 9
4 hours ago
Badilisha mtazamo, jenga uwezo, na jiandae kwa mafanikio baada ya chuo!😊 Jumamosi hii hakikisha unafika chuoni, kujumuika pamoja na wanafunzi wenzako kupata maarifa kuhusu future yako baada ya kumaliza chuo. #YouthEmpowerment #FinancialLiteracy #Genemers #BenkiInayomwelewaMtanzania
58 1
2 days ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amevunja Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 14, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka, hatua hiyo imeanza rasmi kutekelezwa kuanzia tarehe hiyo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kuvunjwa kwa bodi hiyo ni sehemu ya maamuzi ya kawaida ya kiutawala yanayofanywa na mamlaka husika katika kuhakikisha taasisi za umma zinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Shaaban Kissu. #SAUTDIGITAL l #HABARI l #sautdigitalupdates l #RadioSAUTFm
9 0
3 days ago
For Abdallah Othamn,the journey began at @saut_mwanza a place where passion for media was transformed into professional excellence. Today,he continues that journey through @habaristartv delivering stories,presence and professionalism to audiences across the country. Behind every confident presenter is a foundation built through learning,practice and opportunity.That’s the experience students gain at @saut_mwanza
239 11
4 days ago
The Vice Chancellor of @saut_mwanza Prof.Juvenalis AsanteMungu yesterday visited the international students’ workshop involving students from Denmark reaffirming the university’s commitment to international partnerships,cultural exchange and quality education.
111 0
4 days ago
@oscarnickson20 a proud alumnus of @saut_mwanza once captured the hearts of football fans across Tanzania as one of the country’s most recognized sports broadcasters, famously known by many as “Mwamuzi wa Kati.” Today, he continues serving professionally as a Public Relations Officer at the Government Chemist Laboratory Authority, proving that communication skills can open doors far beyond the studio. At @saut_mwanza students are prepared to excel in media, communication, leadership, and every space where impactful voices are needed. Your journey to influence can begin here too. KARIBU TULIJENGE JIJI LA MUNGU ✝️
810 114
5 days ago
Kikundi cha wanafunzi wa shahada ya Uhandisi kutoka chuo cha @saut_mwanza kimeshiriki hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi washindi wa shindano la andiko la ubunifu wa kupunguza msongamano wa magari mjini “Wanafunzi Chemsha Bongo Challenge” iliyoanzishwa na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega. Chemsha Bongo hiyo ilianzishwa kama shindano kwa wanafunzi wa shahada za uhandisi katika vyuo vikuu nchini, kwa lengo la kuibua mawazo ya kutatua kero ya foleni nchini. Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo,Waziri Ulega alisema Wizara imeamua kuwashirikisha vijana katika kutafuta suluhisho za changamoto za usafiri mijini ili kuhamasisha matumizi ya maarifa ya darasani katika vitendo na kuongeza ushiriki wao katika maendeleo ya Taifa. Kikundi cha wanafunzi hao kutoka chuo cha @saut_mwanza ambao waliambatana pia na Rais wa serikali ya wanafunzi chuo cha @saut_mwanza ,Mh.Paul Kashinje ( @paulkashinje_ )
77 4
5 days ago
@maria_ukhotya a proud alumna of @saut_mwanza continues to make her mark in the media industry through @crownfmtz while inspiring many with her professionalism and creativity. Her journey recently earned national recognition after winning the @teyaawards as Young Author and Multimedia Creator of the Year. From talent discovery to industry impact this is the kind of greatness nurtured at @saut_mwanza . Dream big,sharpen your skills and let your voice reach beyond limits.
713 50
7 days ago
Ni video iliyosambaa na kufuatiliwa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha mwanaume huyu wa Kiafrika nchini Tanzania akitumia meno yake kukwangua mti. Je, una ufahamu gani kuhusu kile anachokifanya mwanaume huyu na maana yake katika jamii au tamaduni husika? #SAUTDIGITAL l #HABARI l #sautdigitalupdates l #RadioSAUTFm
32 1
10 days ago
Klabu ya Azam FC inatarajiwa kuwa mgeni wa TRA United katika mchezo wa ligi utakaopigwa kesho Mei 8, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema kikosi chake kinapaswa kuwa imara kiufundi, kitaalam na kiakili ili kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu ugenini. “Kesho tunakwenda kukabiliana na mpinzani mzuri. Tunatakiwa tuwe wazuri kweli kitaalam, kiufundi na mara nyingi kiakili na kujaribu kuchukua pointi tatu hizi,” alisema Ibenge. Azam FC inaingia katika mchezo huo ikiwa na lengo la kuimarisha nafasi yake katika msimamo wa ligi, huku TRA United wakitarajiwa kutumia uwanja wao wa nyumbani kuwania matokeo chanya mbele ya mashabiki wao. #SAUTDIGITAL l #HABARI l #sautdigitalupdates l #RadioSAUTFm
7 0
10 days ago
Kocha Abdihamid Moalin na Kocha Patrick Mabedi wameanza rasmi majukumu ya kuinoa timu ya Young Africans SC, kufuatia mabadiliko yaliyofanywa katika benchi la ufundi la klabu hiyo. Mabadiliko hayo yanakuja baada ya uongozi wa Yanga SC kutangaza kumfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Pedro Gonçalves, kupitia taarifa iliyotolewa Mei 6, 2026. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, klabu ilimshukuru Gonçalves kwa mchango wake alioutoa wakati wa uongozi wake na kumtakia mafanikio katika majukumu yake yajayo. Katika hatua ya mpito, uongozi wa Yanga SC umewakabidhi majukumu Moalin na Mabedi hadi mwisho wa msimu, ambapo tayari wawili hao wameanza kazi kwa kuongoza mazoezi ya kikosi hicho Mei 7, 2026. Mashabiki wa Yanga SC sasa wanasubiri kuona mwelekeo mpya wa timu chini ya uongozi huo wa muda, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michezo ijayo ya Ligi Kuu. #SAUTDIGITAL l #HABARI l #sautdigitalupdates l #RadioSAUTFm
7 0
10 days ago
Klabu ya Simba SC imeendelea kuonyesha matokeo chanya ndani na nje ya uwanja baada hapo jana kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Baada ya ushindi huo, Simba SC imetangaza rasmi kuhamisha miechezo yake katika Uwanja wa KMC Complex unaomilikiwa na klabu ya KMC FC. Hatua hiyo inakuja katika mazingira ambayo uwanja huo pia hutumiwa na watani wao wa jadi, Young Africans SC, hali inayoongeza msisimko mpya kati ya vigogo hao wa soka la Tanzania. Kwa hatua hiyo, mashabiki wa soka wameitafsiri kwa utani kuwa baada ya “kupiga mwenye nyumba” kwa ushindi uwanjani, Simba sasa “wamehamia alikopanga Yanga,” wakirejea uwepo wa Yanga SC katika matumizi ya uwanja huo. Uhamiaji huo unatarajiwa kuongeza ushindani na mvutano wa kimichezo kati ya miamba hiyo miwili ya soka la Tanzania katika maandalizi ya mechi zijazo. #SAUTDIGITAL l #HABARI l #sautdigitalupdates l #RadioSAUTFm
8 0
10 days ago