Oscar Nickson Nkembo

@oscarnickson20

Professional Journalist PRO Mkemia Mkuu wa Serikali Former Sports Caster RFA /Azam TV /TBC /BongoFM BBC Swahili/ RFI Swahili
Followers
49.2k
Following
1,413
Account Insight
Score
40.88%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
35:1
Weeks posts
Ndugu Zangu naijua vizuri sana hiyo klabu , Yanga inaviongozi wanaoweza Kudanganya Umma bila kuogopa kabisa nawaambia, miaka mitatu iliyopita Yanga waliwadanganya watanzania kupitia Ukurasa wao rasmi wa Instagram wakasema Yanga TV sasa ni channel rasmi ndani ya Kisimbuzi cha Azam TV, Sasa sitashangaa kama Na Hilo la Uwanja likawa kama la Yanga TV kuonekana Azam TV mpaka leo sijawahi kuipata kwenye kisimbuzi cha Azam Hizi klabu Zetu zinaongozwa na wahuni wahuni miaka nenda miaka rudi hizo za Viwanja ni hadithi za Abunuasi na hazijaanza leo.
743 183
1 day ago
Katika soka la ushindani, hisia huwa sehemu ya mchezo. Furaha, hasira, presha, matumaini na maumivu ya kupoteza ni vitu vinavyoandamana na timu, viongozi, wachezaji na mashabiki. Lakini kadri ushindani unavyokuwa mkubwa, ndivyo namna ya kuutafsiri ushindani huo inavyokuwa muhimu zaidi kwa hadhi ya klabu kubwa kama Simba SC na Young Africans SC. Kwa miaka ya hivi karibuni, Simba imekuwa ikipewa hadhi ya timu yenye uwekezaji mkubwa, kikosi bora na malengo makubwa ya kimataifa. Lakini pamoja na ubora huo, ukweli mmoja umeendelea kuonekana wazi; Yanga ndiyo timu ambayo imekuwa ikiwasumbua zaidi kisaikolojia na kimatokeo ndani ya ligi. Hali hiyo imeanza kujenga kile kinachoweza kuitwa “ugonjwa wa matamanio” ndani ya Simba — hali ya kutamani zaidi mpinzani aanguke kuliko wao wenyewe kushinda vita yao uwanjani. Jana wengi waliona namna baadhi ya viongozi, wachezaji na mashabiki wa Simba walivyokuwa wakifuatilia kwa karibu mchezo wa Yanga dhidi ya Dodoma Jiji FC na namna walivyofurahia matokeo mabaya kwa Yanga. Kimsingi hilo ni jambo la kawaida katika ushindani wa soka. Hakuna timu inayopenda kuona mpinzani wake wa karibu akishinda kila siku. Lakini swali kubwa linabaki kuwa; je, furaha ya mpinzani kupoteza ndiyo iwe msingi wa matumaini ya ubingwa kwa klabu kubwa kama Simba? Timu yenye mentality ya ubingwa hupambana kuchukua kombe kwa nguvu zake yenyewe. Haisubiri msaada wa timu nyingine. Ubingwa mkubwa hujengwa kwa kuifunga Yanga moja kwa moja, kushinda mechi zako muhimu, kuwa na consistency na kuonyesha nguvu ndani ya uwanja. Ndiyo maana mara nyingi mashabiki wa soka wanaheshimu zaidi timu inayochukua ubingwa kwa dominance kuliko ile inayosubiri mpinzani ajiharibie. Kitendo cha Simba kufurahia sana matokeo mabaya ya Yanga kinatoa picha moja muhimu sana kwa jamii ya soka; kwamba Yanga kwa sasa ndiyo kipimo kikubwa cha mafanikio au maumivu ndani ya Simba. Hii ni dalili ya namna ushindani huo ulivyoingia mpaka kwenye saikolojia ya klabu. Badala ya Simba kuonekana kama timu inayotengeneza njia yake ya ushindi, wakati mwingine inaonekana kama timu inayopima furaha yake kwa kuangalia hali ya Yanga.
39 6
3 days ago
#TBT ROCK FM RADIO MBEYA @emmanueljohn1030
154 45
3 days ago
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo Nidhamu na tabia njema inajengwa kutoka nyumbani , Ukilea Jambazi nyumbani kuna siku litakuvamia tu, Huyu Diarra alitukana watu wakasema ni upambaniaji wa timu sio utovu wa nidhamu huyu huyu anaonesha kuwadharau Waamuzi wetu Yanga ikasema ni kuipigania Timu Kiko wapi? Jana Timu inamuhitaji kwa sababu ya Makosa ya Captain yaliyoruhusu bao la Kwanza Yeye akaamua Kujivunja, anajiona mkubwa kuliko Yanga na hilo wamelisababisha Yanga wenyewe, hiyo sio Nature ya Yanga wamewahi fukuzu Timu nzima haya Diarra Be Carefull Ushauri kwa Yanga. Kwa sasa Hamna Golikipa bora zaidi ya Diarra, tulieni amalizie Ligi kisha zisetiwe Standards nzuri za kudhibiti nidhamu za wachezaji, acheni tabia za kukumbatia tabia mbaya, mchezaji akifanya ujinga adhabu zianzie ndani ya Club itasaidia kuonesha hakuna mkubwa kuliko Yanga Video ni Mali ya @chrisskakwaya
70 9
3 days ago
“Kuna Timu zinajifanya Timu kubwa ila sio Timu Kubwa, Timu kubwa inapaswa kuendeshwa katika hali ya usafi, umeshawahi kuona Timu kubwa mchezaji anadai ada ya uhamisho? umewahi kusikia Mamelodi Mchezaji anadai? Nyie sio Timu Kubwa , Timu nyingine inaendeshwa kama amacha ndio hii unasikia kocha anaongoza ligi kwa pointi tano anafukuzwa ndio hii Mungu anawaadhibu, naweza sema Azam ndiyo Timu kubwa huwezi sikia imepelekwa FIFA eti mchezaji anadai asa ya usajili” Mwinyi Zahera kocha wa Zamani wa Yanga akizungumza na @davidkampista ndani ya @cloudsfmtz
801 59
4 days ago
Kocha wa Zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema Timu hiyo ilifanyamakosa makubwa kumfuta kazi kocha wake Pedro akiwa anaongoza ligi bila kupoteza mchezo wowote “Maisha ni malipo kila kitu unatenda utalipa, ubaya ni deni utalipa, nakwambia hakukuwa na sababu ya kumfukuza kocha Pedro, kwenye mkataba wanataka ubebe upigwa ufuzu ligi ya mabingwa hamna sehemu wanaandika ucheze vizuri sana wanataka matokeo, yule kocha wamemfanyia kitu kibaya kumfukuzu kazi bila kosa lolote ule ubaya ni deni wamelipa leo” Mwinyi Zahera Aidha Zahera ameongeza kuwa Kama walimfukuza kocha kiwa kileleni bila kupoteza mchezo basi wanapaswa kumfukuza aliyepoteza mchezo mmoja ndani ya mechi mbili kwani kufunga mabao matatu ameonesha udhaifu mkubwa wa kimbinu Chanzo : Mahojiano na @davidkampista @cloudsfmtz @oscarnickson20 @oscarnickson20
151 7
4 days ago
Mchezaji wa Daraja la Kawaida Sana , ukweli ni kwamba jamaa anakosa sana nafasi ila hatuambiani ukweli, angetumia walau Nafasi mbili tu yangetokea yaliotokea? Yanga acheni utani niliwaambia hamna Streka mkanitukana haya Kiko Wapi ?? Mtu anakosa kila nafasi ?? namheshimu na Nampenda Dube but hana Quality ya kucheza Yanga.
102 23
4 days ago
Nani anakubaliana na @yurah_himidi ?? anasema yeye ni Mwananchi na Matokeo haya ni mazuri??
112 6
4 days ago
ALAN OKELLO AMEFUNGA BAO HARAMU ALIKUWA AMEOTEA HAPA MWAMUZI AMEWABEBA YANGA HIVYO BASI TUKITOA BAO HILI HARAMU NGOMA HII ILIPASWA KUWA DODOMA 3 YANGA 1 Video Mali ya Azam TV
57 2
4 days ago
Sisi haoo Dodoma Jiji FC What a day , Historia imeandikwa @dodomajijifootballclub Video Mali ya @azamtvtz
352 6
4 days ago
SISI HAO WAKULIMA WA ZABIBU @dodomajijifootballclub ⚽️⚽️⚽️
117 11
4 days ago
Siku mbaya sana kwa Captain ni ngumu kumtetea ila ndiyo hivyo siku mbaya kazini.
37 1
4 days ago