Mbeya Fm 89.3 MHz

@mbeyacityfm

Habari Za Ndani | Burudani | Michezo | Vipindi Maalum. 89.3 MHz | Mbeya | Njombe | Iringa | Songwe | Sumbawanga. #matangazo Piga +255 745 327 319.
Followers
11.4k
Following
61
Account Insight
Score
35.14%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
188:1
Weeks posts
content creator na mhamasishaji kwa njia ya mitandaoni @chiefgodlove_billionaire leo amepokea gari zake nchini Kenya baada ya kusafirishwa hapo jana kutokea Tanzania. Kupitia ukurasa wake wa Instagram @chiefgodlove_billionaire ameeleza kuwa sababu ya kusafirisha gari zake hadi kenya ni kwaajili ya kuziosha na kuzifanyia matengenezo. @chiefgodlove_billionaire amesisitiza kuwa hakuna mnyakyusa mshamba wala hakuna mtoto wa kimaskini aliezaliwa kwenye familia ya kimaskini anayeweza kupata hela zikapotea kilahisi. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
7,878 449
4 months ago
Ingawa mara nyingi harusi ni tukio linalofurahiwa na kusherehekewa, hali imekuwa tofauti kwa Zainab Kombo, aliyefanya sherehe baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mume wake. Hatua ya Zainab imeibua mitazamo tofauti kutoka kwa wadau wa maadili, wataalamu wa sosholojia, viongozi wa kiroho na Serikali, baadhi wakimuunga mkono, huku wengine wakimpinga. Viongozi wa dini wao wanasema sherehe za talaka zinapaswa kupingwa kwa sababu hazitoi mfano mwema kwa jamii na zinavunja heshima iliyopewa taasisi ya ndoa. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima, anasema hata kwake tukio hilo limekuwa jambo geni. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
16.5k 688
4 months ago
Frida Kajala Masanja '@kajalafrida ' ameonekana kuufurahia wimbo wa #FURAHA akiwa kwenye show ya Mpenzi wake wa zamani Fleva Rajab Abdul Kahali ‘@harmonize_tz ’ Zanzibar, ambako Harmonize alikuwa akifanya show. Frida Kajala Masanja '@kajalafrida ' aliambatana marafiki zake ikiwemo #Lamata lakini pia matukio kadha wa kadha yaliendelea ndani ya show hiyo. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
5,354 43
4 months ago
Umoja wa Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania (UWAKTA) umesema utaendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa amani ili kuendelea kudumisha mshikamano ulioasisiwa na waasisi wa Taifa. Akizungumza Mei 10, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa UWAKTA, Msemaji wa umoja huo, Sheikh Said Kinyogoli, amesema ni Jukumu la Wahadhiri wote kutoa elimu kwa Watanzania juu ya maoni na mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Uchunguzi kuwa ni kitu kizuri na yakifanyiwa kazi nchi itakuwa salama "Kila wahadhiri wote waliotoka katika kona mbalimbali za nchi yetu hii ya Tanzania, wao wanaondoka hapa wakiwa wamelibeba jukumu la kuhakikisha kwenye maeneo yao, kitu cha kwanza ni kuihubiri amani ya nchi yetu. Kitu cha kwanza ni kuihubiri amani ya nchi yetu. Lakini kingine, ni kuwapa elimu Watanzania juu ya maoni, mapendekezo yaliyotolewa na tume ya uchunguzi, kwamba Watanzania mapendekezo haya ni kitu kizuri na inshallah Mwenyezi Mungu akijalia yakifanyiwa kazi tutakwenda kuwa salama na nchi yetu itaendelea kuwa kisiwa cha amani" 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
0 0
1 day ago
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akizungumza katika mahojiano na Bongo FM Mei 15, 2026, Msigwa alifafanua kuwa namna wananchi wanavyotii sheria ni kipimo cha wazi cha kuridhishwa na uongozi na mwelekeo wa nchi. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
0 1
1 day ago
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imepanga ifikapo mwaka 2030, iwe imesajili vikundi na kampuni 20,000 za vijana ziingie katika mfumo wa manunuzi. Amesema uamuzi huo, unalenga kuzifanya kampuni na vikundi hivyo, viwe sehemu ya wanufaika wa zabuni zinazotangazwa na Serikali. Nanauka ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Mei 16, 2026 alipozungumza wakati wa Kongamano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu lililokuwa na kaulimbiu ya Never Again. Amesema Sheria ya Manunuzi ya Umma, inataka taasisi za Serikali kutenga asilimia 30 ya manunuzi yake kutoka katika makundi ya wanawake, watu wenye ulemavu, wazee na vijana. “Katika hiyo asilimia 30, asilimia 10 inatakiwa iende kwa vijana. Tafsiri yake, katika mwaka wa fedha uliopita asilimia 30 ya manunuzi yaliyokuwa yanatakiwa kutengwa ni zaidi ya Sh30 trilioni, katika hiyo maana yake kuna takriban Sh3 trilioni kwa vijana,” amesema. Kwa bahati mbaya, amesema katika mfumo wa manunuzi kuna kampuni chache za vijana zilizosajiliwa kwa ajili ya kuomba zabuni, ndiyo maana Serikali inataka kuhakikisha inasajili kampuni za kundi hilo ili wanufaike kiuchumi. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
2 0
1 day ago
Akizungumza leo Mei 16, 2026, Katika Mjadala wa kitaifa kuhusu mwelekeo na khatima ya Tanzania, uliokusanya makada na viongozi wa chama hicho, wasomi, wanadiplomasia na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo ngazi ya Taifa, Othman Masoud amesema licha ya kuwepo uhuru wa kuzungumza bado watu wanapewa vitisho wanapozungumzia Bungeni Matukio ya Uchaguzi Mkuu 2025. "Badala ya kuzifuta machozi familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na mauaji ya mwaka 2025, imetia pilipili kwenye kidonda. Huu ni ukweli. Sasa ajabu kubwa zaidi ya nchi yetu, kuna watu wanataka hata haya yasizungumzwe Leo kuna watu ambao wanatishwa kwa yale wanayoyasema bungeni kuhusiana na yaliyotokea kwenye uchaguzi"- Amesema Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Othamn Masoud. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
0 0
1 day ago
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, wakati wa mahojiano na Bongo FM Mei 15, 2026. Amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru inayojiongoza kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni zake, na haitakubali kuendeshwa au kupangiwa namna ya kufanya mambo yake na wanaharakati. "Tanzania sio nchi ambayo inatakiwa iamuliwe na mwanaharakati namna ya kuendesha mambo yake.
0 0
1 day ago
Elia Shula M/kiti wa kikundi cha Igale Vijana ame sema mafunzo ya ujasiriamali yame wapa manufaa makubwa kwenye kundi lao. Baadhi ya miradi walio anzisha baada ya mafunzo ni cpu mradi unao fanya kazi ya kuosha na kuchambua kahawa pia wameanzisha kukopesha mbolea. Mbali ya hiyo miradi pia M/kiti wa kikundi ame sema moja ya mradi wanao taka kuanzisha tena ni uchimbaji wa visima vitakavyo wasaidia wana kijiji wa Igale. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
0 0
1 day ago
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amemwagiza kupiga marufuku mikataba ya kinyonyaji kwa madereva bodaboda. Ametaka makundi hayo ya vijana kuhakikisha wanarasimishwa kwa kupewa vyeti vya kuzaliwa ili viwawezeshe kupata namba za utambulisho wa uraia na vigezo vingine vya kukopesheka. Msando ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Mei 16, 2026 alipozungumza wakati wa Kongamano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu lililokuwa na kaulimbiu ya Never Again. Amerejea muundo wa mikataba ya madereva wa bodaboda, akisema inawalazimu kurejesha Sh6 milioni, katika pikipiki inayonunuliwa kwa Sh3 milioni. Msando, amesema ukubwa huo wa marejesho na unyonyaji wa mikataba ndiyo inayowafanya madereva bodaboda kuendesha mwendokasi ili wawahi kuwasilisha rejesho la Sh13,000 kwa siku kwa mabosi wao. 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #mbeya
0 0
1 day ago
Mwanasiasa na mbunge wa zamani wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekia Wenje amesema vijana wana wajibu wa kulinda nchi bila kujali itikadi za vyama vya siasa. Amesema hayo leo , Jumamosi Mei 16,2026 katika kongamano la wanafunzi wa vyuo lenye kauli mbiu 'never again' tuipende, tuitunze , tuilinde nchi yetu' lililofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na TAHLISO mkoani hapa. Wenje amesema kwa takwimu zilizopo vijana nd ndio wengi na mchango mkubwa katika Taifa na ndio watu wanaouweza kuamua hatima ya nchi. " Kuna tofauti kati ya Serikali na Taifa Kuna tofauti kati ya nchi na Serikali, duniani hapa Serikali zinapita, chukua mfano Marekani kuna wakati Democratic kinaongoza, wakati mwingine Republican, lakini msingi lazima Taifa libaki," amesema Wenje 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
0 0
1 day ago
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema yaliyotokea Oktoba 29, 2025 hayakuwa mambo ya kawaida na hayafanani na Taifa la Tanzania. Kwa sababu ya uhalisia huo, Profesa Kabudi, amesema ni vema kama Taifa kukubaliana kwamba yasitokee tena ‘Never Again’ kauli ambayo imetumika na mataifa mbalimbali yalipokumbwa na mambo yasiyo ya kawaida. Profesa Kabudi, ameeleza hayo jijini Dar es Salaam leo, Mei 16, 2026 alipozungumza katika moja ya majopo wakati wa Kongamano la Vijana lililobeba ujumbe wa ‘Never Again’ inayomaanisha yasitokee tena “Zipo nchi, zilikumbwa na misukosuko, tufani na baadaye zikasema never again what happened yesterday. Mmechukua kaulimbiu inayoashiria kwamba kuna lililotokea si la kawaida, halifanani na nchi yetu na limetutikisa,” amesema. Aidha, Profesa Kabudi amesema chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ndipo mipango mingi iliyopangwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imetekelezwa ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JHPP). 📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku! 📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu. #mbeyacityfm #mbeya #Mbeya
0 1
1 day ago