Ni heshima kubwa kwangu pamoja na warembo wenzangu wa Miss Grand kupata mwaliko wa kuhudhuria Bunge la Tanzania, ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda
@baba_keagan , aliwasilisha bajeti ya wizara yake.
Uzoefu huu umeniacha na matarajio makubwa kuona juhudi zaidi zikiwekwa katika kuwawezesha vijana kupitia sanaa, michezo na tasnia ya urembo. Ninaamini kuna nafasi kubwa ya kufungua fursa zaidi kwa vijana kukuza vipaji vyao, ubunifu wao na kufikia ndoto zao kwa kiwango cha juu zaidi.
Pia nashukuru kupata nafasi ya kukutana na viongozi na wadau mbalimbali akiwemo Mhe. Gerson Msigwa
@gersonmsigwa , Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mhe. Hamis Mwinjuma (Mwanafa) , Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Bw. Alphonce Simbu
@simbualphonce , mwanariadha bingwa wa dunia 2025 ; pamoja na Bw. Redemptus Caesar
@officialcza , mtaalamu wa media na maendeleo ya biashara. Kila mmoja wao ni msukumo mkubwa kwa vijana kama sisi.
Ninabaki na imani kuwa mustakabali wa vijana wa Tanzania unaendelea kung’aa zaidi kila siku 🇹🇿✨
#missgranduniversity #youthinaction #creativeindustry