bongo5.com

@bongofive

Tanzania’s #1 Plug! Your daily dose of News • Culture • Vibes
Posts
66.9k
Followers
2.8m
Following
1,417
Account Insight
Score
76.89%
Index
Health Rate
80%
Users Ratio
2012:1
Weeks posts
82.19
Vichwa vya habari magazeti ya leo May 18, 2026 Tanzania 🇹🇿, Kenya 🇰🇪 na Uganda 🇺🇬.
12 1
18 minutes ago
Binti (14) kidato cha kwanza mkazi wa Msangalale, Dodoma, anayefahamika kwa jina la Niache Nisome (sio jina lake halisi), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana usiku wa Jumapili Aprili 26, 2026, na baadaye kupatikana akiwa ametupwa kwenye korongo huku akiwa hana fahamu na kudaiwa kubakwa. Kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo, anadai alibakwa na watu wanne akiwemo baba yake mzazi. Inaelezwa kuwa siku ya tukio, majira ya usiku akiwa anatoka kunyoa akiwa na rafiki yake, gari jeusi lilisimama ghafla na watu waliokuwemo ndani yake kumlazimisha kuingia kabla ya kutokomea naye kusikojulikana. Rafiki aliyekuwa naye alitoa taarifa nyumbani, na juhudi za kumtafuta zilianza mara moja bila mafanikio. Inadaiwa kuwa majira ya saa nne usiku, familia ilifika Kituo cha Polisi kutoa taarifa ya kupotea kwa mtoto huyo. Majirani wa eneo hilo wamedai kusikia taarifa za kupotea kwake usiku huo na kushiriki katika jitihada za kumtafuta. Mama wa binti huyo, akiwa katika hali ya majonzi, amesema mtoto wake alimweleza kuwa aliwaona baadhi ya watu waliomshambulia, akiwemo baba yake mzazi ambaye alidai alimwambia: “Kwanini unachukua chuki ya Mama yako?” Mama huyo amesema hana mgogoro mkubwa na mzazi mwenzake isipokuwa changamoto za muda mrefu zinazohusiana na malezi ya mtoto huyo. Kwa upande wake, baba anayehusishwa na tuhuma hizo amekanusha kuhusika. Akizungumza na BongoFive, amesema madai hayo yanachochewa na mgogoro wa muda mrefu kati yake na mama wa mtoto huyo. Aidha, amedai kuwa kwa muda mrefu aliwahi kuomba kufanyika kwa vipimo vya DNA ili kuthibitisha uhusiano wake na mtoto huyo lakini hakupata ushirikiano. Mtuhumiwa huyo pia amesema kuwa siku ya tukio alikuwa Zanzibar kwa shughuli za kikazi na kisiasa, akieleza kuwa yeye ni kiongozi na mwanachama wa CCM. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kupokea taarifa ya tukio hilo na kusema uchunguzi bado unaendelea. Kama una tukio lolote la ukatili, mkasa wasiliana nasi kupitia 0716265838 Fuatilia mkasa mzima YouTube BongoFive Imeandaliwa na @yasiningitu
587 82
11 hours ago
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa msanii @mbosso_ amewaacha mashabiki zake na maswali mengi baada ya kupost picha yenye maandishi #ODB, huku O-May, D-June na B-July. Wengi wakifikiria huenda Mbosso ataachia Album tatu ndani ya hiyo miezi wengine wakishindwa kuelewa kabisa. Je, unahisi @mbosso_ anamaanisha nini kwenye hii Post??
673 7
11 hours ago
Rapa wa muziki wa Bongo Fleva @billnass ameachia Freestyle yake mpya ya Division One, Mpe maksi zako
1,084 63
12 hours ago
Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Klabu ya Manchester United pamoja na timu ya Taifa ya England, Rio Ferdinand, ameweka wazi kuwa atatembelea Tanzania Mei 19 hadi 22, 2026 kufuatia mwaliko wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda. Kupitia ujumbe wake, Rio amesema amefurahishwa na mazungumzo aliyofanya na Mhe. Makonda pamoja na viongozi wengine kuhusu fursa zilizopo Tanzania katika michezo, utalii na maendeleo ya vijana. Amesema ana hamu ya kujifunza zaidi kuhusu utamaduni wa Tanzania, kukutana na wananchi pamoja na kuona namna ambavyo ushirikiano wa michezo unaweza kufungua fursa mpya kwa vijana wa Kitanzania. Ziara hiyo inatarajiwa kuwa sehemu ya juhudi za kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia michezo, utalii na diplomasia ya kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
263 6
12 hours ago
Ameandika kuwa:- “ZUCHU MASTERCLASS 2026 Madarasa ya siku tatu ya kujiandaa na Industry ya Muziki .Hii ni kwa ajili ya kukuandaa wewe Mwanamuziki ,Dj ,Dancer ,Na manager kwa ajili ya Majukwaa na Industry kwa ujumla
233 10
12 hours ago
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwenye video inaonyesha dereva wa pikipiki (Bodaboda) akiwa njiani akakuta njia imezibwa kwa mbele na Mnyama ambaye ni Simba na kuamua kugeuza, Ingekukuta wewe ungekuwa katika hali gani??
617 41
14 hours ago
Bruno Fernandes tayari ameifikia rekodi iliyowekwa na mkongwe Thierry Henry (Arsenal) kwa kufikisha pasi za mwisho 20 msimu wa 2002-2003 pamoja na Kelvin De Bryune (Man City) nae akiwa amefikisha pasi za mwisho 20 katika msimu 2019-2020. Ikumbukwe Bruno Fernandes yupo kwenye kinyang’anyiro cha kupata tuzo ya mchezaji bora, hii rekodi ya kufikisha pasi za mwisho 20 haijawahi kuvunjwa bali imefikiwa na wachezaji wawili nje ya Henry wa Arsenal ni De Bryune pamoja na Bruno Fernandes. Hii rekodi inampa nguvu mno Bruno kwenye kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza Henry na De Bryune katika misimu husika walishinda hiyo tuzo baada ya kufikisha rekodi hiyo, lakini mambo hayakwenda sawa kwa Mesut Ozil alikuwa kinara wa pasi za mwisho akifikisha pasi 19 katika msimu wa 2015/2016 lakini alikosa hiyo tuzo. Tuzo hii mara nyingi wanaangalia na jumla umehusika vipi na magoli nje ya pasi za mwisho pia wanaangalia mchango wako kwenye timu na timu yako kwa ujumla imeshika nafasi ya ngapi katika msimu husika mchezaji akionekana kwenye vigezo vingi vya usaidizi wa timu ndio hupewa tuzo hizo. Je, unaiona tuzo hiyo msimu huu ikienda kwa Bruno Fernandes wa Man Utd?? @vunjabeibet
558 2
14 hours ago
Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amewahimiza wananchi kuendelea kuiombea Tanzania ili amani, umoja na mshikamano wa kitaifa viendelee kuimarika sambamba na nchi kuendelea kupiga hatua za maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Amesema hayo leo Jumapili, Mei 17, 2026 aliposhiriki ibada katika (KKKT) Usharika wa Kondoa Mjini, Jimbo la Kondoa, Dayosisi ya Dodoma. Ibada hiyo iliongozwa na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, pamoja na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kondoa Mjini na Mkuu wa Jimbo la Kondoa KKKT, . Waziri Mkuu amesema anaendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini akitambua mchango wake katika kujenga jamii yenye maadili, umoja na maendeleo. “Ujumbe wake kwa wananchi wa Kondoa ni kwamba tuendelee kuiombea nchi yetu ili iendelee kuwa ya amani na kuendelea kupiga hatua za maendeleo,” amesema. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ikiwemo ujenzi wa daraja la kuingia Kondoa Mjini pamoja na daraja la barabara ya kuelekea Hanang. “Tumebeba jambo la daraja la kuingia hapa Kondoa Mjini, hilo tutaanza nalo. Lakini la pili ni daraja la kuelekea Hanang ambalo na lenyewe kero yake ni kubwa sana,” amesema. Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea na maandalizi ya utekelezaji wa mfumo wa elimu ya lazima wa miaka 10 unaotarajiwa kuanza mwaka 2028. “Hatutakuwa na jambo linaloitwa mtoto amemaliza darasa la saba. Tunaenda kuondoa mfumo wa kuishia darasa la saba ili elimu ya lazima iwe miaka 10,” amesema. Amesema utekelezaji wa mfumo huo unahitaji ushiriki na hamasa kutoka kwa Watanzania wote kutokana na umuhimu wa mabadiliko hayo katika sekta ya elimu nchini. Kwa upande wake, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini. “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu , kwa ushirikiano na sisi watu wa imani na viongozi wa dini,” amesema. Aidha, amesema kanisa linaendelea kumuombea Waziri Mkuu pamoja na viongozi wa Serikali ili waendelee kulitumikia taifa kwa hekima na uadilifu.
47 2
16 hours ago
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amesema mchezaji na Nahodha wa zamani wa Klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Rio Ferdinand anatarajiwa kuja kutembelea nchini tarehe 19, Mei 2026. Makonda amesema hayo Mei 16, 2026 wakati wa hafla ya chakula cha jioni ya Mkutano wa mwaka wa 31 wa wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Arusha. Ameeleza kuwa, hatua hiyo inalenga kufungua milango ya Tanzania na kuwa kivutio kwa wageni wengi wa mataifa mbalimbali kufika na kuleta manufaa. Aidha, Makonda amebainisha kuwa, kupitia Wizara hiyo vijana watanufaika na ajira na kuongeza uchumi kupitia vipaji vyao.
357 27
16 hours ago
Kiungo wa Singida Black Stars, Khalid Aucho ataikosa mechi ijayo ya NBC PL dhidi ya Yanga kutokana na kadi nyekundu aliyoonyeshwa jana kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la CRDB. Yanga itawakaribisha Singida Mei 22 ndani ya KMC Complex.
759 33
18 hours ago
Wengi tumeona mapokezi ya Album tatu Mpya za Drake (Iceman, Habibti na Maid of Honour1 zimepokelewa kwa ukuwa zaidi tunaweza kusema Drake ni Goat kutokana na Consistency yake, Streaming namba zake zinatishia Dunia kwa hivi sasa, hits zake haziishi na hata Album alizoziachia 2026 tunaweza kusema Drake hakuna wa kumfikia kwa sasa kwenye mafanikio ya kibiashara kwa Marapper Duniani. Wengi wanasema Kendrick Lamar anashika Crown hasa baada ya Beef ya 2024. “Not like Us” ilikuwa tishio sana na hata baada ya miaka miwili bado ilikuwa na Impact, Kendrick alichukuliwa kama yeye ndio mfalme kwa wakati huo lakini hii album ya Drake imekuja kubadili upepo wa watu. Wengine wanasema kuwa J Cole kama moja ya Marapper wenye nguvu sana kwa hifi sasa. Tunaweza kusema Drake ni Mfalme wa Numbers, hit songs, kibiashara na mwendelezo mzuri kwenye Hip Hop huku Kendrick Lamar akiwa Mfalme kwenye kudumisha Utamaduni halisi wa Hip Hop. Je, wewe unaona kwa sasa Duniani nani ni Mfalme wa Hip Hop kati ya Drake, Kendrick Lamar na J Cole??
362 27
19 hours ago