BEATS AND BARS

@beatsandbars___

🎤 Underground stays alive here || HANDAKINI 📍 Hip-hop from the roots up - Swahili Lyrics Daily "Keeping the underground loud."
Followers
1,835
Following
400
Account Insight
Score
27.91%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
5:1
Weeks posts
Nyabinghi Daicon [@nyabinghi_daicon_unique ] ni moja kati ya Mc bora ambao wanawakilisha mkoa wa Mbeya vyema kwenye ramani ya Muziki wa Hip Hop kwa upande wa Underground. Mbeya ni moja kati ya mikoa ambayo imebarikiwa watu na wasanii ambao wanafanya vizuri sana upande wa Underground Hip Hop inchini Tanzania, nikukumbushe tu Dizasta Vina ni moja kati ya kichwa ambacho kimeendelea kusumbua upande wa Underground Hip Hop nchini na moja kwa moja ni chata kutoka mkoa wa Mbeya. Nyabinghi ni Mc mwenye uandishi wa kipekee sana linapokuja suala la mistari huwa ni msanii anaezingatia vina vizuri lakini pia haachi nguzo muhimu ambayo ni ujumbe. Nyabinghi ameendelea kufanya vizuri kwa kutoa ujumbe kupitia ngoma zake mbalimbali kama vile MIMI NI MUNGU, SHABIKI ambayo amempa shavu Shaulin Seneta [@shaulinsenetamwanazuoni ] na Freestyle mbalimbali ambazo amezitoa. Unaweza kwenda kwenye YouTube na kuandika Nyabinghi Daicon na uka subscribe, like, comment na ku-share muziku mzuri wa Hip Hop. ✍️🏽 @___.culture . . . . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #musicvideo
21 5
7 hours ago
Pages [@pages._ ] kupitia ukurasa wake wa instagram amethibitisha kuachia Album mpya inayokwenda kwa jina la OBSESSION. Pages amachia Album hiyo ambayo ina nyimbo kumi na tatu (13) huku akiwa ameshirikisha wasanii sita (6) ambao ni Mazimpaka Prime [@mazimpaka_prime ], Kelvin Tiba [@kelvintiba ], Rabia Damari [@Rabiadamari ], na Lacoste. Lakini pia kupitia artwork ya cover yake ametoa shootout kwa baadhi ya waandishi wa nyimbo hizo ambapo Fivara [@fivara ] pia amehusika kwenye Album hiyo kwa kuandika track number 5. Album hiyo inapatikana kwenye majukwaa yote ya kidigitali kama Spotify, Apple Music, Boomplay na Audiomack. Nenda ka-support muziki mzuri sasa. . . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #musicvideo
32 0
1 day ago
Bars kali sanana za moto kutoka kwa brother @mullaobo 🔥 Kalamu ya kitaa , kalamu ya uhalisia wa life la vijana This is real Hiphop Ungeipa ngapi 1–10? 💾 Save kama imekugusa Follow and share na wana @raplines._daily for daily bars and @beatsandbars___ for daily Hiphop updates Follow na kusubscribe kwa @mullaobo kupata ngoma kali Lyrical credits 🎙@mullaobo . . . #raplines . #bongohiphop #wasafi #bongo
774 27
1 day ago
Barkeliam [@barkeliam_ ] kupitia ukurasa wake wa instagram amethibitisha kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la TAP TAP. Barkeliam ameachia ngoma hiyo sambamba na video ambazo zote zinaendelea kufanya vizuri katika majukwaa ya kidigitali, mitandao ya kijamii, redio na vipindi mbalimbali vya televisheni. Hadi sasa video ya wimbo huo inaendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube ikiwa na watazamaji zaidi ya 2000. Kwa sasa ngoma hiyo inapatikana kwenye majukwa yote ya kidigitali kama vile YouTube, Spotify, Apple Music, Boomplay, Audiomack na mengine. Je, umeshaisikiliza ngoma hiyo, Ni mstari upi umeupenda kweny ngoma hiyo? Dondosha comment yako hapo chini 👇🏽 . . . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #music
61 1
2 days ago
Mex Cortez [@mex.tz ] kupitia ukurasa wake wa instagram ametangaza kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la KUUH. Mex Cortez hivi karibuni alifuta post zote kwenye ukurasa wake wa instagram na kuacha post moja ambayo ilikuwa ikionesha Kuna jambo ambalo linakuja hivi karibuni ambapo aliwaomba mashabiki zake like 3000 na comments 500 ili kuweza kutoa ngoma hiyo. Mex Cortez hivi karibuni amekuwa anafanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya kidigitali kifuatia mvutano wake baina ya msanii mwenzake wa Hip Hop Young Lunya. Je, unadhani ngoma hii ni muendelezo wa kile kilichokuwa kinaendelea? Dondosha comment yako hapo chini.
15 0
2 days ago
Rapper ni mtu anayefanya rap tu, yani kuimba kwa mistari yenye vina na flow. Mwana hip hop ni mtu anayewakilisha utamaduni mzima wa hip hop, sio rap pekee. Anaweza kuwa rapper, lakini pia anaelewa na kuheshimu vitu kama: •Rap/MCing •DJing •Breakdance •Graffiti •Maarifa na maisha ya hip hop Kwa kifupi: Kila mwana hip hop anaweza kuwa rapper, lakini si kila rapper ni mwana hip hop.
78 9
3 days ago
Rapa wa kike Barbiemia [@its_barbiemia ] kupitia ukurasa wake wa instagram ametangaza ujio wa ngoma mpya hivi karibuni. Barbiemia ambae yupo chini ya Lebo ya IAM Music [@iam_music_co ] ambayo inasimamiwa na Country wizzy [@countrywizzy_tz ] ameendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya kidigitali ambapo kwa mara ya mwisho aliachia Extended Playlist yake inayokwenda kwa jina la LIFE OF BARBIE ambayo ilikuwa na nyimbo nne. Kwa sasa ametangaza ujio wa ngoma hiyo mpya. . . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #musicvideo
101 10
3 days ago
Jabir Saleh [@jabirsalehtherealest ] A.K.A Kuvichaka au Kuvifacts kupitia ukurasa wake wa instagram amethibitisha kuachana na redio ya Efm ambayo alikuwa akifanya kazi hapo. Jabir Saleh kupitia ukurasa wake amewashukuru Efm kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 ambapo amesema kipindi chote ambacho amekuwa Efm kimemfanya kuwa mtu bora zaidi ya alivokuwa. Kwa sasa Jabir Saleh amejiunga na redio ya Ufm kwenye kipindi cha Mtaa wa 107. . . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #musicvideo
289 18
4 days ago
Rapa Frida Amani [@fridaamaniofficial ] ambae pia ni mtangazaji wa Clouds fm kipindi cha Amplifier kupitia ukurasa wake wa instagram amethibitisha kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la CELEBRATE. Frida Amani ameachia ngoma hiyo ambayo inaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa yote ya kidigitali kama Spotify, iTunes, Boomplay na majukwaa mengine hadi sasa kwenye mtandao wa YouTube hadi sasa ngoma (video) hiyo inazaidi ya watazamani 4000. Je, umeshaisikiliza na kuitazama ngoma hiyo? Kama bado inapatikana kwenye majukwaa yote ya kidigitali. Kama umeshaisikiliza ngoma hiyo, mstari upi umeupenda? dondosha comment yako hapo chini 👇🏽 . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #musicvideo
31 4
4 days ago
🎵 UCHAMBUZI WA WIMBO “MUDA” Muda NI wimbo wa hip hop ulioimbwa na @kinyamistari , kupitia wimbo huu msanii ameupa Muda sifa za binadamu ili kuitahadharisha jamii katika Mambo muhimu. Kwa ujumla, Muda ni wimbo unaozungumzia uhalisia wa maisha kupitia kitu ambacho kila binadamu anakitumia kila siku lakini wengi hawakithamini — muda. Kinya Mistari ameufanya muda uwe kama binadamu mwenye uwezo wa kuzungumza, kutoa tahadhari, kujitetea na kueleza nafasi yake katika maisha ya watu. Katika wimbo huu, muda umechorwa kama nguvu inayotawala mafanikio, kushindwa, majuto na maendeleo ya mwanadamu. Kinya anaonyesha kwamba muda hausimami, haumsubiri mtu na hauna upendeleo. Kila mtu anapewa muda, lakini tofauti ya waliofanikiwa na walioshindwa ni namna walivyoutumia. Wimbo unaonesha kuwa watu waliouheshimu muda walifanikiwa, huku walioupuuzia wakibaki na kilio na majuto. Ndiyo maana anasema waliomfuata walipata mafanikio, lakini waliodharau walitaka “kumzidi mbio” mwisho wakaanguka. Hapa anafundisha kwamba hakuna mtu anayeweza kuushinda muda; unaweza tu kwenda sambamba nao. Pia Kinya anakosoa tabia ya watu kupoteza muda huku wakijiona wana nafasi nyingi mbele yao. Mistari kama: “Unaevaa saa kama pambo unachekesha” inaonyesha namna baadhi ya watu wanavyoonekana kuthamini muda kwa nje, lakini matendo yao hayaonyeshi hivyo. Kwa upande mwingine, wimbo una tahadhari nzito kuhusu maisha. Muda unasema ukimpoteza ni hatari, kwa sababu hauwezi kurudishwa nyuma. Hii inaakisi ukweli kwamba fursa, ujana, nguvu na maisha yenyewe vina mipaka. Ukichelewa kufanya jambo muhimu leo, kesho inaweza isikukute na nafasi hiyo tena. Kinya Mistari pia ameonyesha ubora mkubwa wa kiuandishi kwa kutumia personification — yaani kuupa muda tabia za kibinadamu. Mbinu hii imeufanya ujumbe uwe mzito zaidi na rahisi kumgusa msikilizaji moja kwa moja. Kwa ujumla, Muda ni wimbo wa mafundisho unaowakumbusha watu kuwa maisha hayaharibiwi na kukosa uwezo pekee, bali mara nyingi huharibiwa na kuchezea muda. Ni wimbo unaosisitiza nidhamu, uwajibikaji, kufanya maamuzi mapema na kutambua kuwa muda ndio mali pekee ambayo ikiondoka hairudi tena. Je unamaoni gani na Pia umejifunza nini katika wimbo huu?
9 5
5 days ago
Nacha [@nacha_ousam ] ambae ni mkali wa Spoken Word Poetry kwa upande wa Tanzania kupitia ukurasa wake wa instagram amethibitisha kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la I'M FINE. Nacha ameachia ngoma hiyo siku ya Jana na hadi sasa inaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya kidigitali ambapo kwenye jukwaa la YouTube tayari ngoma hiyo ina zaidi ya watazamaji 20000 na kwa sasa ipo top 20 YouTube trending. Je, umeshaisikiliza ngoma hiyo? Dondosha mstari ambao umeukubali kwenye ngoma hiyo👇🏽 . . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #musicvideo
19 4
5 days ago
Dr. Chemical [@dr.chemical_tz ] kupitia interview ambayo amefanya na redio ya Wasafi Fm na kupitia interview hiyo ameeleza maoni yake juu ya game ya muziki wa Hip Hop kwa upande wa wanawake kipindi yupo masomoni. Je, wewe una maoni gani kuhusu hilo? Dondosha comment yako hapo chini 👇🏽 . . . . . #BeatsAndBars #tamaduni #hiphopmisingi #tanzania #musicvideo
6 0
5 days ago