Dr. Abdulmajid Nsekela

@amnsekela

Son, Husband, Dad Group CEO & MD @crdbbankplc | Chairman @ushirika_tcdc | Chairman @bodi_ya_chai | Former Chairman @tba_forbankers
Followers
84.9k
Following
525
Account Insight
Score
63.03%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
162:1
Weeks posts
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela (@amnsekela ) akizungumza na #Cloudsmediagroup kuhusiana na safari pamoja na mafanikio ya Mkutano Mkuu wa 31 wa Wanahisa wa CRDB BANK. Mkurugenzi Dr. @amnsekela alisema Benki ya CRDB itaendelea kuwekeza katika teknolojia, ujumuishaji wa kifedha na huduma zinazounganisha uzoefu wa kidijitali na huduma za ana kwa ana ili kuongeza ushindani, kuboresha uzoefu wa wateja na kujenga thamani endelevu kwa wadau wake. Zaidi isogeleee kurasa ya CloudsMF na Clouds Tv kwa video. #AGM2026
230 5
10 hours ago
CEO to CEO moment with Mr. Abdul Majid Nsekela. Some leaders don’t just lead institutions, they shape the way you think about vision, resilience, and legacy. From him, I continue to learn that strength in leadership is built through consistency, patience, and the courage to keep moving forward even when the journey is demanding. Grateful for this moment at the CRDB Bank AGM. Inspired, humbled, and more focused on the bigger vision. CRDB ni mimi. CRDB ni wewe. CRDB ni sisi sote. #infocusstudiotz #livestreamkingstz #crdbbank #crdbnisisisote #ceolife
1,124 32
11 hours ago
✅ Wanahisa wamepitisha Ripoti ya Wakurugenzi pamoja na Taarifa za Hesabu Zilizokaguliwa kwa mwaka 2025. ✅ Wanahisa wameidhinisha pendekezo la gawio la Shilingi 90 kwa kila hisa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 38 ikilinganishwa na Shilingi 65 zilizotolewa mwaka jana. ✅ Wanahisa wamepitisha azimio la kuiteua Kampuni ya Ukaguzi wa Hesabu ya nje ya PWC kuwa wakaguzi wa Benki kwa mwaka 2026. #CRDBBank #AGM2026
357 4
12 hours ago
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema mwaka 2025 Benki hiyo iliendelea kuimarisha nafasi yake kama taasisi kubwa zaidi ya kifedha nchini kupitia ukuaji mkubwa wa biashara, ubunifu wa kidijitali na upanuzi wa huduma zake kikanda. Akiwasilisha taarifa yake, Dkt. Nsekela (@amnsekela ) alisema jumla ya mali za Benki ziliongezeka kwa asilimia 33.6 hadi kufikia Shilingi trilioni 22.3, huku mikopo na advances zikifikia Shilingi trilioni 13.7, hatua aliyosema inaonyesha uwezo wa Benki kuendelea kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali za uchumi. Alisema Benki itaendelea kuwekeza katika teknolojia, ujumuishaji wa kifedha na huduma zinazounganisha uzoefu wa kidijitali na huduma za ana kwa ana ili kuongeza ushindani, kuboresha uzoefu wa wateja na kujenga thamani endelevu kwa wadau wake. #AGM2026
989 18
14 hours ago
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema mwaka 2025 Benki hiyo iliendelea kuonyesha nguvu ya mkakati wake wa kidijitali na ujumuishi wa kifedha kupitia ongezeko kubwa la wateja na matumizi ya huduma za kisasa za kifedha. Dkt. Nsekela alisema Benki ilifikia wateja milioni 7.2 kupitia mtandao wa mpana zaidi wa huduma nchini Tanzani, Burundi, DR Congo, pamoja na Ofisi ya Uwakilishi ya Dubai. Aidha, amesema kuwa mageuzi ya mfumo yamesaidia kuongeza ufanisi katika mtandao wa utoaji huduma wa Benki. Benki ya CRDB inaongoza kwa mtandao wa matawi zaidi ya 261, ATM 732, CRDB Wakala 38,883 pamoja na vituo vya malipo na manunuzi 6,607, hatua iliyosaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha nchini na katika masoko tunayoyahudumia. Alisema mafanikio hayo yanaonyesha namna Benki ya CRDB inavyoendelea kujenga uzoefu bora kwa wateja kupitia teknolojia, huduma za kifedha jumuishi huku ikiendeleza dhamira yake ya kubadilisha maisha na kukuza maendeleo ya uchumi. #AGM2026
151 2
14 hours ago
Benki ya CRDB imeendelea kuimarisha nafasi yake kama kinara wa sekta ya fedha nchini kwa kuongoza katika viashiria vikuu vya soko ikiwamo amana kwa asilimia 27, mikopo kwa asilimia 30, mali kwa asilimia 28 pamoja na faida baada ya kodi kwa asilimia 32, mafanikio yanayoonyesha nguvu ya biashara, imani ya wateja na uimara wa mkakati wa Benki hiyo sokoni. Akiwasilisha taarifa yake katika Mkutano Mkuu wa 31 wa Wanahisa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema Benki itaendelea kuwekeza kimkakati katika teknolojia, ubunifu wa kidijitali pamoja na mifumo ya kisasa ya utoaji huduma ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji, kuboresha uzoefu wa wateja na kuharakisha ukuaji wa biashara. Aidha, amesema Benki ya CRDB itaendelea kupanua uwepo wake katika masoko ya kikanda na kimataifa sambamba na kuimarisha nafasi yake kama taasisi kubwa zaidi ya kifedha Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku ikiendelea kujenga thamani endelevu kwa wanahisa na kuchochea ukuaji wa uchumi. #CRDBBank #AGM2026
88 0
14 hours ago
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema mwaka 2025 Benki hiyo iliendelea kuonyesha nguvu ya mkakati wake wa kidijitali na ujumuishi wa kifedha kupitia ongezeko kubwa la wateja na matumizi ya huduma za kisasa za kifedha. Dkt. Nsekela alisema Benki ilifikia wateja milioni 7.2 kupitia mtandao wa mpana zaidi wa huduma nchini Tanzani, Burundi, DR Congo, pamoja na Ofisi ya Uwakilishi ya Dubai. Aidha, amesema kuwa mageuzi ya mfumo yamesaidia kuongeza ufanisi katika mtandao wa utoaji huduma wa Benki. Benki ya CRDB inaongoza kwa mtandao wa matawi zaidi ya 261, ATM 732, CRDB Wakala 38,883 pamoja na vituo vya malipo na manunuzi 6,607, hatua iliyosaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha nchini na katika masoko tunayoyahudumia. Alisema mafanikio hayo yanaonyesha namna Benki ya CRDB inavyoendelea kujenga uzoefu bora kwa wateja kupitia teknolojia, huduma za kifedha jumuishi huku ikiendeleza dhamira yake ya kubadilisha maisha na kukuza maendeleo ya uchumi. #CRDBBank #AGM2026
97 2
15 hours ago
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema mwaka 2025 Benki hiyo iliendelea kuimarisha nafasi yake kama taasisi kubwa zaidi ya kifedha nchini kupitia ukuaji mkubwa wa biashara, ubunifu wa kidijitali na upanuzi wa huduma zake kikanda. Akiwasilisha taarifa yake, Dkt. Nsekela alisema jumla ya mali za Benki ziliongezeka kwa asilimia 33.6 hadi kufikia Shilingi trilioni 22.3, huku mikopo na advances zikifikia Shilingi trilioni 13.7, hatua aliyosema inaonyesha uwezo wa Benki kuendelea kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali za uchumi. Alisema Benki itaendelea kuwekeza katika teknolojia, ujumuishaji wa kifedha na huduma zinazounganisha uzoefu wa kidijitali na huduma za ana kwa ana ili kuongeza ushindani, kuboresha uzoefu wa wateja na kujenga thamani endelevu kwa wadau wake. #CRDBBank #AGM2026
174 1
15 hours ago
Sehemu ya hotuba ya CEO wa @crdbbankplc Dr. @amnsekela Mei 15, 2026 kwenye Siku ya Uwekezaji kwa Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha Umejifunza nini? #sokonifix #entrepreneurship
820 15
1 day ago
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema benk imeamua kuhamasisha vijana kuwekeza katika hisa kama mkakati wa kujenga kizazi chenye uwezo wa kumiliki mitaji, kushiriki katika ukuaji wa taasisi za ndani na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika uchumi rasmi. Dkt. Nsekela alisema Benki ya CRDB imeona mwamko mkubwa wa vijana katika masuala ya fedha, teknolojia, biashara na uwekezaji, hali inayodhihirisha uwepo wa kizazi chenye uelewa mkubwa wa fursa za masoko ya mitaji na uwekezaji wa muda mrefu. Alisema vijana hawapaswi kubaki kuwa watumiaji wa huduma za kifedha pekee bali washiriki wa moja kwa moja katika umiliki wa taasisi na kampuni zinazochochea uchumi wa Taifa. Aidha, alisema Benki ya CRDB inaendelea kuwekeza katika ubunifu wa kidijitali unaowawezesha vijana kuwekeza na kusimamia uwekezaji wao kwa urahisi kupitia SimBanking App, hatua inayolenga kufanya huduma za uwekezaji zipatikane kwa urahisi zaidi, kuongeza ushiriki wa vijana katika masoko ya mitaji na kujenga utamaduni wa uwekezaji wa kisasa unaoendana na kasi ya teknolojia. #CRDBBank #AGM2026
249 4
1 day ago
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema thamani ya uwekezaji katika Benki hiyo imeendelea kukua kwa kasi sambamba na mafanikio ya taasisi hiyo ndani na nje ya Tanzania. Dkt. Nsekela alisema ndani ya miaka saba iliyopita faida ya Benki ya CRDB imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 1000 hadi kufikia Shilingi bilioni 725 mwaka 2025, huku thamani ya hisa ikipanda kutoka chini ya Shilingi 100 mwaka 2018 hadi zaidi ya Shilingi 2,800 kwa sasa. Alisema mafanikio hayo ni ushahidi kuwa uwekezaji wa muda mrefu una uwezo mkubwa wa kujenga thamani kwa wawekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji na biashara. #CRDBBank #AGM2026
161 2
1 day ago
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema Benki hiyo imeendelea kuwa mstari wa mbele kuwawezesha vijana kupitia huduma za kifedha, elimu ya fedha, ubunifu na uwekezaji katika masoko ya mitaji. Akizungumza katika Semina ya Wanahisa iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC), Dkt. Nsekela alisema Benki kupitia kitengo chake cha huduma kwa vijana ‘Youth Banking’ imebuni huduma mbalimbali zinazowawezesha vijana kufikia ndoto zao kuanzia utunzaji wa akiba, uwezeshaji kupitia mikopo, pamoja na huduma za kidijitali maalum kwa vijana. Aidha, alisema kupitia taasisi yake CRDB Bank Foundation na programu ya IMBEJU, Benki ya CRDB tayari imetoa uwezeshaji waa zaidi ya Shilingi bilioni 20 kwa zaidi ya biashara changa 5,800 tokea kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 2023. Dkt. Nsekela amebainisha kuwa Benki ya CRDB imewekeza katika ubunifu wa huduma za vijana katika kila hatua za maisha yao kuanzia wanapokuwa shuleni, vyuoni, n ahata pale wanapoanzisha biashara na kuwa wajasiriamali. “Benki yetu inaamini vijana ni Taifa leo na wanapaswa kuwezesha kushiriki kikamilifu kuijenga leo na kesho yao,” aliongezea. #CRDBBank #AGM2026
194 3
1 day ago