Mzalendo Halisi

@zack__255

Critical Thinker |
Followers
7,511
Following
7,433
Account Insight
Score
33.46%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
1:1
Weeks posts
▪️Baraza la Mawaziri la EAC kukutana kwa Dharura jijini Arusha Maandalizi ya Mkutano wa 60 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Mei 2026, yameanza rasmi kupitia vikao vya ngazi ya wataalamu vinavyoendelea kuanzia tarehe 18 hadi 20 Mei 2026 katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha. Kikao hicho cha wataalamu kimepokea na kujadilia taarifa ya Kamati ya Fedha na Utawala kuhusu masuala ya fedha ya Jumuiya, na rasimu ya bajeti ya Sekretarieti ya EAC pamoja na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Mapendekezo yatakayopitishwa katika ngazi hiyo yatawasilishwa kwa Makatibu Wakuu watakaokutana tarehe 21 Mei, 2026 kabla ya kuwasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 22 Mei, 2026. Vilevile, mkutano huo wa siku tano kuanzia tarehe 18 hadi 22 Mei, 2026 unalenga kuweka mikakati ya pamoja ya utekelezaji wa maelekezo na maamuzi yaliyotolewa na Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi za EAC, hususan katika maeneo ya mipango na fedha Baraza la Mawaziri la EAC ni chombo kikuu cha maamuzi na kusimamia shughuli za Jumuiya, katika hatua hii ya maandalizi ya bajeti, Baraza hilo lina jukumu la kupokea, kuchambua, kufanya marekebisho na kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Sekretarieti ya EAC kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa rasmi. Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unajumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ukionaongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka.
1 0
53 minutes ago
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (MB), ashiriki Kikao cha 31 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13, Mei 18, 2026 Jijini Dodoma.
1 0
1 hour ago
Waziri wa Kilimo Mhe, Daniel Chongolo ashiriki Kikao cha 31 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13, Mei 18, 2026 Jijini Dodoma.
5 0
1 hour ago
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo (Mb), akishiriki Kikao cha 31 cha mkutano wa Tatu wa Bunge la 13, Mei 18, 2026 Jijini Dodoma.
5 0
1 hour ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Miradi wa Benki hiyo, Kanda ya Afrika, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe Bw. Firas Raad mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2026.
3 0
1 hour ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Miradi ya Benki hiyo, Kanda ya Afrika, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2026.
4 0
1 hour ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2026. Bw. Belete ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Miradi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, alifika Ikulu kwa ajili ya kumuaga Mhe. Rais Dkt. Samia mara baada ya kuhudumu katika nafasi yake ya awali kwa kipindi cha miaka minne. Pia aliambatana na mrithi wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe Bw. Firas Raad.
8 0
1 hour ago
5 0
1 hour ago
▪️Ndejembi Aongoza Ujumbe wa Tanzania Maandalizi ya Mkutano wa Nishati ya Nyuklia Afrika Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Mei 18, 2026 ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha maandalizi ya ushiriki wa Mkutano wa Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA) unaofanyika jijini Kigali, Rwanda kuanzia Mei 18-21, 2026. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Kigali na kuhudhuriwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Omar, Naibu Waziri wa Maji na Madini wa Zanzibar, Mhe. Seif Pandu, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Felchesmi Mramba pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja wataalamu kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC). Mkutano wa NEISA unawakutanisha viongozi wa serikali, wataalamu wa sekta ya nishati, wawekezaji na wadau mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika na duniani kwa lengo la kujadili ubunifu, uwekezaji na matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
2 0
1 hour ago
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, akizungumza na Ndg. Mursali Mustafa Issa ambaye ni mlemavu wa viungo katika Uwanja wa shule ya msingi Kambi ya Nyasa, Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma tarehe 17 Mei, 2026, baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya hiyo.
1 0
2 hours ago
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Najma Murtaza Giga akiongoza kikao cha 31 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13, katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, leo Mei 18, 2026. Translate
2 0
2 hours ago
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe, wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbambwe, Bw. Nathan Belete baada ya kumaliza muda wake, iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam.
2 0
2 hours ago