Wasafi_digital

@wasafitv_digital

@wcb_wasafi is a full_service management, Music, Publishing and Entertainment Company founded by @diamondplatnumz
Followers
5,595
Following
25
Account Insight
Score
32.3%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
224:1
Weeks posts
WASAFI MEDIA TUMEDHAMIRIA KUKUPA KILICHO BORA 📻 📺 Ofisi zetu za Wasafi Media sasa zimepata muonekano mpya wa kisasa unaoendana na maendeleo ya teknolojia na ubunifu wa tasnia ya burudani. Muundo wa ofisi umeboreshwa kwa mtindo wa kisasa (modern media workspace) wenye mazingira yanayochochea ubunifu, ushirikiano na uzalishaji bora wa maudhui. Studio za kurekodia vipindi vya Radio, Televisheni na Digital zimewekewa vifaa vya kisasa vya sauti na picha, pamoja na mapambo ya kuvutia yanayoakisi utambulisho wa brand yetu. Pia kuna maeneo maalum ya mikutano, editing, na ubunifu wa maudhui (creative rooms) kwa ajili ya waandishi, watangazaji, wazalishaji wa vipindi Pamoja na Matukio. Muonekano huu mpya unaonyesha dhamira yetu ya kuendelea kuwa media ya kisasa, yenye ubunifu na inayotoa maudhui bora ya aina zote. ✨ Kwa kifupi: Muonekano mpya wa ofisi zetu ni ishara ya maendeleo, ubunifu na kujipanga kutoa huduma bora zaidi katika tasnia ya media na burudani. #MchezoUmebadilikaa, #theworldisyours
9 0
1 month ago
"Studio Za Wasafi Ni Level Za Dunia Na Sio Afrika" Live On @wasafifm & @wasafitv | Youtube - Wasafi Media
12 0
1 month ago
Mhe. Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, leo ameungana na maelfu ya wakimbiaji kushiriki kwenye @yastanzania_ Kili International Half Marathon 2026 iliyofanyika mkoani Kilimanjaro Region. Ushiriki wake umeonesha dhamira ya Serikali kuhamasisha michezo, afya na mshikamano wa jamii kupitia matukio makubwa ya kimataifa kama haya. 🏃‍♂️🇹🇿 #YASKiliInternationalHalfMarathon2026 #kilimanjaro
3 0
1 month ago
MAAGIZO YA RAIS MWINYI KWA JESHI LA POLISI - SHEREHE ZA SIKUKUU YA EID FITRI ZANZIBAR Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amelitaka Jeshi la Polisi kusimamia na kuhakikisha usalama na amani vinaimarishwa katika viwanja vya sikukuu, pamoja na kusisitiza usimamizi madhubuti wa sheria za usalama barabarani ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu kwa amani na utulivu. Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 21 Machi 2026, katika Baraza la Eid el-Fitri lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Polisi, Ziwani, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amefafanua kuwa ili kuwa na jamii yenye ustawi bora, ni vema utaratibu huo ukaendelezwa kwani kwa kiasi kikubwa umewasaidia watu wa makundi maalumu, wakiwemo mayatima, wajane na mafakiri, kupata futari na kutekeleza ibada ya funga kikamilifu. Aidha, Alhaj Dkt. Mwinyi amesema waumini wa dini ya Kiislamu wana wajibu mkubwa wa kutekeleza na kuendeleza mambo yote ya kheri yaliyokuwa yakifanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ikiwemo kumcha Mwenyezi Mungu kwa bidii, kwani yanaongeza upendo, umoja na mshikamano. Aidha amewanasihi waumini wa dini ya Kiislamu na jamii kwa ujumla kuendeleza utaratibu mzuri wa kuwasaidia na kuwahurumia watu wasio na uwezo kwa kuzingatia mahitaji yao maalumu. Kwa upande wa suala la Hijjah, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zinazosafirisha mahujaji kupitia Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana ili kuhakikisha Waislamu wanaokwenda kutekeleza ibada ya Hijjah wanaongezeka. Aidha, ameeleza kuwa Serikali inaendelea na utaratibu wa kukamilisha kuanzishwa kwa mfuko maalum wa Hijjah. Baraza la Eid limehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mama Mariam Mwinyi, viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu, Balozi Seif Ali Iddi, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zuberi Ali Maulid, pamoja na viongozi wa dini, masheikh na waumini mbalimbali. cc: @rashidbattashy #wasafidigita
5 0
1 month ago
RAIS MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI BANDARI JUMUISHI YA MANGAPWANI - “SINA EID HAPA KAZI TU” Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa ujenzi wa Bandari ya Kisasa Jumuishi ya Mangapwani unatarajiwa kuchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa Zanzibar. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo katika eneo la Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Amesema kuwa miongoni mwa mambo yanayokwaza kukua kwa uchumi wa Zanzibar ni kutokuwepo kwa bandari kubwa ya kisasa, hali inayosababisha mrundikano wa makontena katika Bandari ya Malindi ambayo kwa sasa imezidiwa na mahitaji ya huduma. Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Khalid Salum, amesema kuwa mradi huo wa kimkakati utaibua fursa nyingi za ajira kwa vijana, hususan wa maeneo ya jirani. Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Ali Said Bakari, amesema kuwa mradi huo utagharimu dola za Marekani milioni 300. Ameongeza kuwa katika hatua ya kwanza, bandari hiyo itaweza kushusha na kupakia zaidi ya makontena laki mbili kwa mwaka huku mipango ikiwa ni kufikia makontena milioni moja Bandari Jumuishi ya Mangapwani inatajwa kuwa ndio bandari ya kwanza kwa ukubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambayo itazingatia mahitaji yote ya bandarini cc: @rashidbattashy
3 0
1 month ago
Eti Ni Nini Kimemfanya SEMAJI Kuwa “HAPPY” HIvi 😅?? #happyhappyhappy
5 0
1 month ago
🎬: Behind The Scene "Happy" Music Video Je, Sehemu Gani Ya Video Hii Imekukosha Zaidi ⁉️ 🎥: @platnumzgallery
6 0
1 month ago
RAIS SAMIA KUSHIRIKI KILI MARATHON 2027, MSHINDI KUZAWADIWA MILIONI 100 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano ya Kilimanjaro International Marathon 2027. Makonda amesema hayo leo, Machi 22, 2026 wakati akizindua mbio hizo, jijini Arusha na kueleza kuwa zawadi kwa washindi itakuwa zaidi ya shilingi milioni 100. Ameyataja mashindano hayo kuwa ni ya kipekee yenye hadhi kubwa Afrika, yakivutia washiriki kutoka mataifa mbalimbali na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta ya utalii nchini. Vilevile, ameeleza kuwa mashindano hayo yameendelea kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi, kuanzia wafugaji, wafanyabiashara hadi sekta ya huduma za malazi huku akitoa wito kwa mabalozi wa Tanzania kushiriki kikamilifu kuitangaza ikiwa ni mkakati wa kuongeza ushiriki wa kimataifa na kukuza mchango wa michezo katika uchumi wa nchi.
1 0
1 month ago
#BrandNew📺: @diamondplatnumz 🦁 - Happy 🔥 Great visuals and great vibe!💯 Je, Umeitazama Mara Ngapi ⁉️ #AfricaIsWatching #wasafidigital
4 0
1 month ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuimarishwa kwa Akiba ya Kimkakati ya Hifadhi ya Mafuta (National Strategic Petroleum Reserves), ili kuongeza uwezo wa nchi kukabiliana na misukosuko ya soko la dunia. Aidha, amesisitiza kuimarishwa kwa mifumo ya kisasa ya ufuatiliaji wa shehena za mafuta kuanzia bandarini hadi hatua za usambazaji, kwa lengo la kuweka uwazi na kulinda mapato ya Taifa. Mradi wa Matanki ya Kupokea na Kusambaza Mafuta unatekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa gharama ya Shilingi bilioni 701.8. Hadi sasa, utekelezaji umefikia asilimia 41 na jumla ya Shilingi bilioni 117.1 zimelipwa kwa mkandarasi na mshauri wa mradi. Mradi ulianza mwezi Agosti, 2024 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2027. Utakapokamilika, utakuwa na matanki 15 yenye uwezo wa jumla ya mita za ujazo 378,000 ikijumuisha dizeli (162,000), petroli (135,000) na mafuta ya ndege - Jet A1 (81,000), Kukamilika kwa mradi huu kutaongeza uwezo wa jumla wa kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam kutoka mita za ujazo 1,051,888.52 hadi 1,429,888.52, sawa na ongezeko la asilimia 35.9, hatua itakayoongeza upatikanaji wa nishati hiyo na utulivu wa bei ya mafuta nchini. #wasafidigital
0 0
2 months ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Kikombo, mkoani Dodoma leo tarehe 24 Februari, 2026. #wasafidigital
3 0
2 months ago
Mbunge wa Kigoma Mjini @officialbabalevo , akizungumzia changamoto ya wananchi kushindwa kupata vitambulisho vya NIDA, amemuomba Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, kusaidia kuanzishwa kwa dawati maalum litakalopita katika kila kata ya Kigoma Mjini kwa ajili ya kuhakiki na kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho hivyo. Baba Levo amesema iwapo hakutakuwa na bajeti ya kuanzisha dawati hilo, yupo tayari kuuza magari yake mawili ili kupata fedha za kuwalipa watendaji watakaosimamia zoezi hilo. Ameeleza kwa uchungu kuwa wananchi wengi wa Kigoma Mjini wanakosa fursa mbalimbali za ajira, mikopo na huduma za kijamii kutokana na kutokuwa na vitambulisho vya NIDA, na hivyo kuathiri maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla. #wasafidigital
7 0
2 months ago