URT Updates 🇹🇿

@urtupdates

Updates from the United Republic of Tanzania #URTUpdates
Followers
3,893
Following
591
Account Insight
Score
50.87%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
7:1
Weeks posts
Video Highlight: Ziara ya Waziri Mkuu-Kondoa
0 0
1 hour ago
▪️HONGERA RAIS DKT. MWINYI KWA UJENZI NA UKARABATI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA ; MWENYEKITI WA UCCM KAWAIDA Mwenyekiti wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM ndg. Mohamed Ali Kawaida (MCC) amempongeza Makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kutokana na Juhudi anazozifanya katika Kubotesha Miundombinu haswa upande wa barabara Mwenyekiti kawaida ameyasema Hayo katika tukio la Dkt. Mwinyi UVCCM Ushindi Party Tukio Lililojikita Katika Kusherehekea Utimilifu wa Miaka mitano ya maendeleo na Kuipokea miaka mingine mitano ya Kuleta maendeleo na ustawi wa mwananchi mmoja mmoja kupitia utekelezwaji wa ilani ya CCM 2025/2030 Dkt. Mwinyi UVCCM Ushindi Party Inafanyika Leo Tarehe 16 Mei 2026 Katika Ukumbi wa Chuo cha Umoja wa Vijana wa CCM Tunguu, Zanzibar
4 0
3 hours ago
SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KONDOA KWA KIWANGO CHA JUU Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata ya Mnenia, Wilaya ya Kondoa itaendelea kutekelezwa na kukamilika kwa kiwango cha juu, kufuatia dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati. Dkt. Mwigulu aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnenia wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kondoa. Amesema Serikali inatambua umuhimu wa miundombinu katika wilaya hiyo na imejipanga kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaohitajika. Aidha, ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara katika kata hiyo na maeneo mbalimbali ya wilaya, kuboresha huduma za afya pamoja na kutatua kero mbalimbali, ikiwemo zinazohusiana na maeneo ya uhifadhi. Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha dhamira kubwa ya kuleta maendeleo nchini kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa hospitali zaidi ya 100 katika maeneo mbalimbali nchini. “Kwa Afrika, si kila nchi imefikia hatua za maendeleo kama ilivyob Tanzania. Tumpongeze Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema Dkt. Mwigulu. Aidha, amesema Serikali imepokea hoja kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani iliyowasilishwa na Mbunge wa Kondoa, Mhe. Ashatu Kijaji na kwamba suala hilo litafanyiwa kazi. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imefanikiwa kukamilisha miradi mikubwa muhimu, ikiwemo mradi wa bwawa la kuzalisha umeme, na kwamba miradi mingine itaendelea kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameifanya Wilaya ya Kondoa kunufaika na maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi, hususan katika sekta za afya na elimu. Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameckj Nchemba, yupo katika ziara Wilayani Kondoa ambapo leo ametembelea Kata ya Mnenia, na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Msingi Amaali Kinale pamoja na kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa Puma uliopo wilayani humo.
4 0
3 hours ago
DKT. MWIGULU ASEMA BIMA YA AFYA KWA WOTE KUONDOA CHANGAMOTO ZA MATIBABU Waziri Mkuu, Dkt. @mwigulunchemba amesema utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote utaondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika kupata huduma za matibabu nchini. Amesema hayo leo Jumamosi, Mei 16, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kondoa Mjini katika Uwanja wa Puma mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi. Waziri Mkuu amesema kupitia mfumo huo wananchi hawatalazimika tena kutumia gharama kubwa katika hatua mbalimbali za matibabu ikiwemo kumuona daktari, vipimo pamoja na ununuzi wa dawa. “Kwa kuwa tunakwenda kwenye utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wote, baadhi ya haya mambo yaliyokuwa yanawasumbua wananchi yataenda kupata jawabu la kudumu,” amesema. Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya nchini kupitia ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati katika maeneo mbalimbali nchini. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameonya vitendo vya baadhi ya hospitali kuwaelekeza wananchi kununua dawa nje wakati Serikali ikipeleka fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa katika hospitali na vituo vya afya. “Haiwezekani taarifa zioneshe utoshelevu wa dawa ni zaidi ya asilimia 90 halafu kila mwananchi akienda hospitali anaambiwa akanunue dawa nje. Hapo lazima pana mchezo mchafu,” amesema. Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali imeelekeza waganga wakuu pamoja na watendaji wanaosimamia ununuzi wa dawa kuhakikisha dawa zinazonunuliwa zinaendana na mahitaji ya wananchi katika maeneo husika. “Nunuweni dawa kulingana na mahitaji ya eneo husika kwa sababu kila eneo lina aina ya dawa zinazotumika zaidi,” amesema. Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanza kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za dawa katika maeneo mbalimbali ili kubaini kiasi cha fedha kilichotolewa, dawa zilizonunuliwa pamoja na matumizi yake. “Nimetuma watu kufuatilia kila palipo na hospitali, fedha kiasi gani zimekwenda kwenye dawa, dawa kiasi gani zimenunuliwa na kiasi gani zimetumika,” amesema.
3 0
4 hours ago
The Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Hon. Ambassador Mahmoud Thabit Kombo (MP), participated in the Third Session of the Tanzania–Russia Joint Commission on Economic, Trade and Technical Cooperation held in Arusha, reaffirming the enduring bilateral relations and shared commitment of the two nations to deepening strategic partnership, expanding trade and investment opportunities, and strengthening economic diplomacy for mutual prosperity.
3 0
5 hours ago
On the sidelines of the Joint Parliamentary Assembly meetings between the OACPS Africa Region and the European Parliament, the Tanzanian delegation held discussions with several Members of the European Parliament, including Hon. Ms. Hilde Vautmans, Co-President of the OACPS–EU Joint Parliamentary Assembly. The discussions focused on issues of mutual interest within the framework of cooperation between Tanzania and the European Union at bilateral, regional, and international levels.
0 0
6 hours ago
Waziri Mkuu Mhe, Dkt. @mwigulunchemba akizungumza na mtoto mwenye ulemavu wa viungo, Raudhwat Abeid katika viwanja vya Puma Kondoa, mkoani Dodoma leo tarehe 16 Mei, 2026. @samia_suluhu_hassan @owm_tz @ashatukijaji
6 1
6 hours ago
TANZANIA YAIPONGEZA NORWAY KWA MAADHIMISHO YA SIKU YA KATIBA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Norway katika maeneo ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi, nishati jadidifu, kilimo himilivu na maendeleo endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Mhe. Masauni amesema hayo Mei 15, 2026 jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 212 ya Siku ya Katiba ya Norway maarufu kama Syttende Mai, ambapo aliipongeza Serikali na wananchi wa Norway kwa kuendelea kudumisha misingi ya uhuru, demokrasia na mshikamano. Amesema Tanzania inathamini uhusiano wa kihistoria wa zaidi ya miaka 60 na Norway uliyojengwa katika misingi ya urafiki, mshikamano na ushirikiano wa maendeleo, huku akibainisha kuwa hadi Desemba 2025, Mamlaka ya Uwekezaji na Kanda Maalum za Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ilisajili miradi 46 ya uwekezaji kutoka Norway yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 323 na kuzalisha ajira zaidi ya 4,400 nchini. Aidha, Mhe. Masauni ameipongeza Norway kwa mchango wake katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi duniani pamoja na kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika kuimarisha mifumo ya uhifadhi wa mazingira, ikiwemo Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).
3 0
6 hours ago
Minister Ndejembi Chairs Special Session on Nuclear Energy Development Plan The Minister for Energy, Hon. Deogratius Ndejembi, has chaired a special high-level meeting to review proposals for the development of nuclear power generation as part of the Government’s broader strategy to expand electricity production and ensure reliable energy supply for national development. During the session, it was noted that several preparatory steps are already underway, including the drafting of a national nuclear energy roadmap and ongoing collaboration with the International Atomic Energy Agency. The initiative is expected to be implemented over a six to seven-year period through phased stages encompassing national readiness assessments, legal and regulatory preparations, and the establishment of infrastructure for nuclear-based electricity generation. The meeting was held today, May 16, 2026, at the Ministry’s Sub-Office in Dar es Salaam and was attended by the Permanent Secretary responsible for Electricity and Renewable Energy at the Ministry of Energy, Engineer Felchesmi Mramba; the Commissioner for Electricity and Renewable Energy, Engineer Innocent Luoga; the Managing Director of Tanzania Electric Supply Company Limited, Mr. Lazaro Twange; alongside other technical experts from the Ministry.
1 0
6 hours ago
Members of Parliament from the National Assembly of the Democratic Republic of the Congo (DRC) have visited the Mtumba Government City in Tanzania’s capital, Dodoma, to observe the area’s urban planning framework and inspect the site allocated for the DRC Embassy. Leading the delegation, Hon. Prof. Willy Buhini, a Member of the National Assembly of the DRC, expressed appreciation to the Government of Tanzania for allocating the embassy plot and pledged to advise the DRC Government to take full advantage of the opportunity by commencing development of the site. The Government of Tanzania has allocated 75 plots within Mtumba Government City for diplomatic missions and international organizations represented in the country. The Embassy of Uganda is the first to establish its offices in the area, while the embassies of Burundi and Ethiopia are currently in the early stages of development.
5 0
7 hours ago
TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM Na Neema Mbuja na Kassim Nyaki, Dodoma Imeelezwa kuwa Tanzania ni miongoni kwa nchi za awali katika bara la Afrika zilizopewa hadhi ya kimataifa ya Kijiopaki na UNESCO kutokana na mchango mkubwa kupitia Jiopaki ya Ngorongoro Lengai iliyopelekea Serikali kujenga makumbusho ya kisasa ya jiopaki (Urithi Geopark Museum) iliyojengwa na serikali wilaya ya Karatu Mkoani Arusha na kuzinduliwa mwaka 2025. Akiwaslisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii Bungeni Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema makumbusho hayo ni sehemu ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai ambayo imejengwa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu sayansi ya miamba, volkano, na historia ya mazingira, na ni ya pekee katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Amesema kupitia makumbusho hayo Watalii na wadau wanaotembelea jengo hilo wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo muonekano wa dunia miaka mingi iliyopita na ilivyo sasa, maumbile asilia yanayopatikana katika ukanda wa bonde la ufa, kujionea mwamba wenye umri wa miaka milioni tatu iliyopita unaopatikana hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai, sambamba kujifunza tamaduni za makabila ya Wahadzabe, Wairaq, Wadatoga na Wamasai pamoja, kupima uwezo wa kutambua sauti za wanyamapori, kushindana mbio kwa kutumia baiskeli na wanyamapori ndani ya makumbusho na mengine mengi. Makumbusho hii inayosimamia na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa sehemu ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) lenye hadhi tatu zinazotambulika na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (@unesco ) ambapo hadhi hizo ni Eneo la Hifadhi ya Mazingira na Binadamu (Man and Biosphere Reserve 1981), Eneo la Urithi Mchanganyiko wa Asili na Kitamaduni (Mixed World Heritage 2010) na hadhi ya tatu Eneo la Hifadhi ya Jiopaki ya Ngorongoro-Lengai @visitngorongoro
7 0
8 hours ago
DKT. SAMIA AENDELEA KUWEKEZA ELIMU YA UFUNDI NCHINI Waziri Mkuu, Dkt. @mwigulunchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu kupitia ujenzi wa shule za amali na ufundi nchini kote ili kuwawezesha vijana kupata elimu yenye ujuzi na kujitegemea. Amesema hayo leo Jumamosi, Mei 16, 2026 alipokuwa akikagua ujenzi wa Shule ya Ufundi ya Amali Kingale, Halmashauri ya Mji wa Kondoa mkoani Dodoma. Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha miaka minne hadi mitano, Serikali imejenga shule za amali 103 nchini kote ambapo shule 29 kati ya hizo ni za uhandisi, hatua ambayo amesema ni mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu ya ufundi nchini. “Tangu uhuru tulikuwa na shule tano tu za ufundi, lakini Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miaka yake minne hadi mitano amejenga shule 103 za amali, ishirini na tisa zikiwa za uhandisi. Hili ni jambo kubwa sana,” amesema. Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kujenga shule hizo kwa nchi nzima kwa wakati mmoja ili kila mkoa unufaike na fursa hiyo ya elimu ya ufundi. “Alisema kila mkoa upate awamu ya kwanza na watoto waanze kusoma, na baada ya hapo itakuja awamu ya pili ya kumalizia,” amesema. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuajiri walimu wa sekta za elimu na afya ambapo ndani ya siku 100 pekee walimu 7,000 waliajiriwa wengi wao wakiwa wa masomo ya sayansi. Pia, Waziri Mkuu amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kunufaika na mpango wa Samia Scholarship unaowawezesha wanafunzi wanaofanya vizuri kupata ufadhili wa masomo ndani na nje ya nchi. “Ukifanya vizuri sana unapewa Samia Scholarship, huo sio mkopo unapewa fedha ya ufadhili wa kusoma na unachagua chuo chochote duniani,” amesema. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Saidi Majaliwa amesema shule hiyo ilipokea zaidi ya shilingi milioni 544.2 kupitia Programu ya Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Amesema mradi huo umehusisha ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa, matundu 10 ya vyoo, jengo la TEHAMA, jengo la utawala, maktaba, majengo mawili ya maabara pamoja na nyumba ya mwalimu. Aidha,
14 1
8 hours ago