Tanzania Railways Corporation

@tzrailways

Official account for Tanzania Railways Corporation | Ukurasa rasmi wa Shirika la Reli Tanzania Toll Free 0800110042 Bofya kukata Tiketi za SGR👇
Followers
121k
Following
209
Account Insight
Score
64.42%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
578:1
Weeks posts
427 42
1 month ago
Why pay more when you can travel better? SGR offers comfort, speed, and affordable fares. Choose smart. Choose SGR ______________________________________________________________ Kwa nini ulipe zaidi wakati unaweza kusafiri kwa ubora zaidi? SGR inakupa safari yenye faraja, kasi na nauli nafuu. Chagua kwa busara. Chagua SGR.
678 33
3 months ago
Tiketi ya treni sasa iko mkononi mwako. Android na iOS, pakua sasa, safiri kwa urahisi. ---------------------------------------------------------------- Train tickets are now in your hands. Android & iOS, download now and travel with ease.
114 8
1 month ago
Kiongozi wa madhehebu ya Dawoodi Bohora duniani, Dr. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb, amesafiri kwa treni ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Morogoro akiambatana na viongozi na waumini zaidi ya 70 kutembelea waumini walioko Mkoani Morogoro. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya wiki mbili ambapo kabla ya kuwasili Dar es Salaam amewatembelea pia waumini walioko Moshi, mkoani kilimanjaro na Simanjiro mkoani Manyara
4,334 17
13 hours ago
HEKARI 25 ZAFUNGUA NJIA UJENZI WA KAMBI YA MKANDARASI KIPANDE CHA SABA Wananchi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wajitokeza kushiriki zoezi la utwaaji wa ardhi ili kupisha ujenzi wa kambi ya mkandarasi Mradi wa Kimkakati wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha saba kutoka Uvinza hadi Malagarasi. Zoezi hilo ambalo limesimamiwa na timu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanyika katika shule ya msingi ya Mumnyika iliyopo kata ya Luhita wilayani Kasulu ambapo jumla ya takribani hekari ishirini na tano (25) zimetwaliwa kwa wananchi hao. Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele alisema zoezi hilo limefanyika kwa kufuata taratibu za kisheria na kwa ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na wananchi wa maeneo husika na alieleza kuwa lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha utekelezaji wa mradi unaendelea bila vikwazo huku haki na taratibu za ulipaji fidia zikizingatiwa ipasavyo.
34 0
1 day ago
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaujulisha umma kuwa tangazo linalosambaa mitandaoni kuhusu nafasi za ajira katika treni za SGR kwa mwaka 2026 , si la kweli, ni uzushi na halijatolewa na TRC. TRC halitumii mawakala binafsi, namba za simu za watu binafsi, wala kuomba fedha au malipo yoyote katika mchakato wa ajira. Wananchi wanatahadharishwa kutowasiliana na namba zilizopo kwenye tangazo hilo, kutotuma taarifa binafsi, na kutofanya malipo ya aina yoyote. Taarifa rasmi za ajira na matangazo ya TRC hutolewa kupitia tovuti na kurasa rasmi za TRC pamoja na njia rasmi za Serikali. TAFADHALI PUUZA TANGAZO HILI, NI FAKE NEWS.
81 5
2 days ago
Hatua kubwa kwa Taifa letu! TRC sasa inasimama yenyewe! Ni fahari kubwa kuona Shirika la Reli Tanzania (TRC) likifikia hatua ya kulipa mishahara kwa 100% kutokana na mapato yake ya ndani bila ruzuku ya Serikali. Huu ni ushahidi wa utendaji bora na mapinduzi ya kweli ya kiuchumi. #nusumudakotekote #kasiyenyebarakazamama
0 0
3 days ago
TRC INAENDELEA NA UJENZI #nusumudakotekote #kasiyenyebarakazamama
0 0
3 days ago
22 0
3 days ago
UJENZI WA SGR UKIKAMILIKA UTALETA MAPATO SERIKALINI KUPITIA MAKAA YA MAWE
68 1
3 days ago
32 0
3 days ago
30 1
3 days ago