GRATEFUL BEYOND WORDS 🙏🏿
Kualikwa kama mmoja wa wageni rasmi kwenye TUNAWEZA AWARDS ilikuwa heshima kubwa—lakini kupokea tuzo ya heshima kama kioo cha jamii ni jambo ninalolichukua kwa unyenyekevu na uwajibikaji mkubwa.
Hii si tu tuzo… ni ukumbusho kwamba kile tunachofanya kina impact, kinaonekana, na kinaweza kugusa maisha ya wengine.
Asanteni sana waandaaji kwa heshima hii, na hongera kwa kila mshindi na aliyeteuliwa—kila mmoja wenu ni ushuhuda kwamba tunaweza kweli 💫
Rai yangu kwa vijana, hasa nyie Gen Z msisite msiogope kuanza, usikate tamaa, msihofu kuwa tofauti, wala msiruhusu tamaa izime ndoto yenu.
Wekeni uthubutu, na tembeeni kwa ujasiri katika kila mnachokifanya.
Tambueni kwamba mara nyingi kile kinachokutofautisha ndicho kinachokupa mwanga wa kung’aa mbele ya ulimwengu. Upekee wenu si udhaifu ni nguvu yenu ya asili.
Kwa washindi wa leo hongereni sana kwa mafanikio haya. Endeleeni kung’ara, lakini kumbukeni: ukuu wa kweli haupimwi kwa kufika kileleni peke yako, bali kwa wangapi umeinua njiani.
Kwa waandaaji pongezi za dhati kwa kujenga jukwaa lenye maana na athari chanya. Hili si tukio tu; ni mbegu ya urithi unaoendelea kuzaa matunda.
Asanteni sana kwa kunialika ni heshima ya pekee kuwa pamoja nanyi leo.
The journey continues… with purpose, passion, and responsibility.
🗣️ Hon.
@binamubananga
🎥 ©️
@msangi.images
Thanks Miss :
@meet_bether
My Beautiful Dress 👗 Design by :
@otson_legendary_design
Model : Miriam Odemba C.E.O
@sautiyamitindo
@odembamodelmanagement
#MiriamOdemba #KiooChaJamii #SautiYaMitindo #TunawezaAwards #Gratitude Impact Inspiration LegacyInTheMaking