Tips za Michongo

@mchongo.tv

Ukurasa Rasmi wa Mchongo TV Kutoa Elimu na kuonyesha Fursa zilizopo kwenye Sekta ya Kilimo 🚜 Mifugo 🐄 na Uvuvi 🎣 Startimes no: 134 Azam TV(OC): 019
Followers
8,379
Following
355
Account Insight
Score
33.9%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
24:1
Weeks posts
Shukrani za dhati ziende kwa waandaaji wa kongamano hili muhimu; Piga Kitabu Unity kwa kushirikiana na Mchongo Television, Golden Star Consultant pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kwa kuandaa jukwaa lenye lengo la kuwawezesha na kuwaamsha vijana kuhusu fursa halisi za kiuchumi. Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, akiwakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, amewataka vijana kutumia kikamilifu majukwaa ya vijana kama nyenzo ya kujikwamua kiuchumi na kujiendeleza kimaisha. Amesisitiza kuwa majukwaa hayo yanatoa nafasi muhimu kwa vijana kupata elimu sahihi, kubadilishana uzoefu, kuunganishwa na wadau wa maendeleo, pamoja na kubuni na kutekeleza miradi ya kiuchumi, hususan katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi. Aidha, ameainisha kuwa Mkoa wa Morogoro, ukiwa ni mkoa wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania, una fursa lukuki za kiuchumi katika sekta hizo, na amewahimiza vijana kuzitambua, kuzitumia na kuzigeuza kuwa chanzo cha ajira na maendeleo yao binafsi pamoja na maendeleo ya jamii kwa ujumla. #Shukrani #PigaKitabuUnity #MchongoTV #GoldenStarConsultant #OfisiYaMkuuWaMkoaMorogoro #VijanaNaFursa #Morogoro #KilimoBiashara #Ufugaji #Uvuvi #AjiraKwaVijana #IGNITE2026 #Tanzania
58 2
3 months ago
WAZIRI MWENYE DHAMANA NA VIJANA AKIZUNGUMZA LIVE MJINI MOROGORO NA VIJANA ZAIDI YA 2000 TOKA VYUO 9 VYA MOROGORO. Kongamano la Vijana IGNITE limewakutanisha zaidi ya vijana 2,000 kutoka vyuo vikuu na vya kati kwa lengo la kuwapa elimu na uelewa mpana kuhusu namna ya kuchangamkia fursa zinazotokana na sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi kama nguzo muhimu za maendeleo na ajira. Wakati wa kongamano hilo, Waziri wa Vijana Dr. Joel Nanauka alizungumza kwa njia ya simu na kusisitiza umuhimu wa kuwapatia vijana elimu mapema kuhusu fursa zilizopo katika kilimo, ufugaji na uvuvi, akibainisha kuwa elimu hiyo hubadilisha mtazamo na kufungua milango ya ajira, ubunifu na maendeleo. Tunazishukuru kwa dhati taasisi zote, vyuo, wadau na wanafunzi walioshiriki na kufanikisha IGNITE. Huu ni mwanzo tu, kongamano hili litaendelea kufanyika katika maeneo mengine ili kuwafikia vijana wengi zaidi nchini. Kwa kupata tukio zima fuatilia Mchongo Television Azam other Chanel 019, StarTimes 134 , YouTube. #IGNITE #VijanaNaFursa #KilimoNiAjira #MchongoTV #SafariInaendelea
149 3
3 months ago
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Suleiman Masoud Makame amesema machinjio ya Kisakasaka yanakabiliwa na changamoto za miundombinu na huduma, hali inayohitaji maboresho ya haraka. Ameitaka Idara ya Mifugo kuandaa mkakati wa kuimarisha huduma, usafi na ufanisi wa uchinjaji huku akiwataka wananchi kuzingatia taratibu rasmi za afya na uchinjaji katika kipindi cha sikukuu.
4 0
9 hours ago
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imepokea ugeni kutoka Chuo Kikuu cha Cornell cha nchini Marekani pamoja na Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya kilimo cha muhogo nchini. Ziara hiyo iliyofanyika Mei 14, 2026 katika Makao Makuu ya TARI jijini Dodoma, imelenga kujionea mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa Muhogo Bora unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya TARI, Chuo Kikuu cha Cornell na IITA. Mradi huo unaotekelezwa katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Singida na Rukwa, unalenga kuhamasisha matumizi ya mbegu bora za muhogo zinazostahimili magonjwa ya virusi, kuongeza uzalishaji pamoja na kuinua kipato cha wakulima wadogo. Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Thomas Bwana amesema taasisi hiyo itaendelea kuwekeza katika tafiti za kisasa na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa urahisi na kwa wakati. Kwa upande wake, Mwakilishi wa IITA na Mtaalamu Mshauri wa Mifumo ya Mbegu, Dkt. Kiddo Julius Mtunda, amesema kupitia mradi huo jumla ya mbegu mama vipande milioni 1.9 vya muhogo vimegawiwa kwa kushirikiana na TARI. Akitoa maelezo wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa TARI Makutopora, Mtafiti Isack Teya, alisema kituo hicho kinaendelea kufanya tafiti za aina mbalimbali za zabibu zinazolimwa nchini pamoja na matumizi yake, huku akibainisha kuwa kituo hicho pia kinazalisha mvinyo bora kupitia shughuli za usindikaji zinazofanyika katika kiwanda kilichopo kituoni hapo. By: @rachelfestus5 Source: TARI Tanzania
3 0
11 hours ago
Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi limeendelea kufungua milango ya ushirikiano wa kiuchumi kwa kuibua fursa mpya za uwekezaji katika sekta ya kilimo, hususan tasnia ya mbolea na maeneo mengine. Jukwaa hilo lililofanyika katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha limewakutanisha wadau kutoka sekta za umma na binafsi kutoka Tanzania na Urusi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili. Akizungumza katika jukwaa hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amesema mbolea ni nyenzo muhimu katika kukuza sekta ya kilimo na kuongeza tija ya uzalishaji, hivyo ipo haja ya kuwekeza zaidi katika tasnia hiyo ili kuimarisha usalama wa chakula nchini. Amesema hayo wakati wa majadiliano yaliyowakutanisha wadau mbalimbali wa biashara na uwekezaji kutoka Tanzania na Urusi kwa lengo la kuibua fursa mpya za ushirikiano katika sekta mbalimbali za uchumi zenye mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa. Aidha, jukwaa hilo limejikita katika kujadili maeneo ya kimkakati ikiwemo kilimo, madini, viwanda, nishati, teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na elimu ya ufundi, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wenye tija na kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Katika hatua nyingine, watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) walishiriki na kufuatilia kwa karibu mijadala kuhusu fursa za ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi, hususan katika sekta ya kilimo na pembejeo za kilimo, hatua inayotarajiwa kuongeza uwekezaji na kuimarisha maendeleo ya tasnia ya mbolea nchini. By: @rachelfestus5 Source: TFRA
2 0
12 hours ago
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeendelea kuonesha mafanikio makubwa katika kuimarisha sekta za uzalishaji nchini baada ya kutoa gawio la shilingi Bilioni 8.38 kwa Serikali kwa mwaka ulioishia Desemba 31, 2025. Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 50 ikilinganishwa na gawio la shilingi Bilioni 5.58 lililotolewa mwaka 2024, hatua inayodhihirisha ukuaji na uimara wa Benki hiyo katika kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini. Serikali imeendelea kuiamini TADB kama benki ya kimkakati, ambapo hadi sasa imewekeza jumla ya shilingi Bilioni 452.37 kama mtaji kwa ajili ya kuendeleza shughuli zake. Katika mwaka 2025, TADB imefanikiwa kufikia mafanikio mbalimbali ikiwemo: 🟢 Thamani ya mali za Benki kukua kwa asilimia 41 hadi kufikia shilingi Trilioni 1.3. 🟢 Kitabu cha mikopo kuongezeka kwa asilimia 51 na kufikia shilingi Bilioni 806.75 kutoka Bilioni 534.16 mwaka uliopita. 🟢 Faida baada ya kodi kuongezeka kwa asilimia 50 hadi kufikia shilingi Bilioni 27.94. 🟢 Kufunguliwa kwa ofisi mpya tatu katika mikoa ya Kigoma, Kagera na Ruvuma kwa lengo la kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi. TADB inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuimarisha usalama wa chakula nchini pamoja na kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuhamasisha kilimo cha kibiashara badala ya kilimo cha kujikimu. By: @rachelfestus5 Source: TADB
10 0
1 day ago
Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) inaendelea kuimarisha uwezo wa watumishi wake kupitia mafunzo maalum yanayolenga utekelezaji bora wa sheria, kanuni na mifumo ya udhibiti wa biashara ya nafaka na mazao mengine nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika usimamizi wa masoko ya ndani na nje ya nchi, kuzingatia sheria na taratibu za biashara za kitaifa na kimataifa,kuimarisha uwezeshaji wa biashara na masoko pamoja na Uzingatiaji wa viwango vya masoko ya kikanda na kimataifa. Programu hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Kilimo wa mwaka 2050 (AMP 2050) unaolenga kuimarisha taasisi, mifumo ya biashara ya mazao na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini. Mafunzo hayo yamefadhiliwa na AGRA Africa kwa kushirikiana na Agricultural Transformation Office Tanzania (ATO Tanzania). By: @rachelfestus5 Source: COPRA
13 0
1 day ago
Tanzania yazidi kufungua milango ya biashara ya mazao ya kilimo katika soko la China Kupitia mchakato wa usajili wa GACC, Tanzania inaendelea kuimarisha biashara ya mazao ya kilimo nje ya nchi kwa kuongeza utayari wa usafirishaji na ushindani wa kimataifa kwa kampuni za ndani kupata fursa ya kuuza bidhaa katika soko la China. Mazao yaliyopo kwenye fursa hiyo kwa sasa ni pamoja na: ✅ Parachichi ✅ Ufuta ✅ Kahawa ✅ Korosho ✅ Soya ✅ Kakao ✅ Mihogo ✅ Karafuu pamoja na bidhaa zitokanazo na pamba na alizeti. Wadau wa sekta ya kilimo na wauzaji nje wanahimizwa kutumia fursa hii kupanua soko la bidhaa za Tanzania nchini China. Toll Free: 0733 800 200 Maombi mapya yatumiwe kupitia: [[email protected]](mailto:[email protected]) By: @rachelfestus5 Source: COPRA
8 0
1 day ago
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wananchi wa mkoa huo kujiunga kwa wingi katika vyama vya ushirika. Akizungumza Mei 14, 2026 katika ufunguzi wa Jukwaa la Tano la Wadau wa Maendeleo ya Ushirika mkoani humo, amesema vyama vya ushirika vinapaswa kuongeza matumizi ya TEHAMA ili kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia. Mhe. Babu pia ameahidi kuendelea kusimamia, kuongoza na kulinda mali za ushirika huku akisisitiza mshikamano kwa wanaushirika na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo. By: @rachelfestus5 Source: Tume ya Maendeleo ya Ushirika
1 0
1 day ago
Akizungumza kuhusu maendeleo ya kilimo cha miwa, Godfrey Madega amesema wanaendelea kuwa karibu na wakulima kwa kuwapa elimu na ushauri ili kuongeza uzalishaji wa miwa bora yenye tija kwa wakulima na Kiwanda cha Mkulazi. By: @rachelfestus5 Source: Mkulazi Sugar
2 0
1 day ago
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele, leo Mei 15, 2026 jijini Dodoma amekutana na ujumbe kutoka Umoja wa Afrika uliowasili nchini kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa mifugo. Ujumbe huo umefanya tathmini hususan kwenye chanjo ya kudhibiti ugonjwa wa sotoka kwa mbuzi na kondoo. By: @rachelfestus5 Source: Wizara ya Mifugo na Uvuvi
1 0
1 day ago
Wakulima katika Halmashauri za Chamwino, Kondoa, Chemba na Kongwa wamepatiwa elimu ya uzalishaji wa Alizeti kwa kutumia kanuni bora za kilimo kupitia mashamba darasa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wenye tija. Mafunzo hayo yametolewa na wataalam wa Wizara ya Kilimo kupitia Mradi wa Kuwezesha Upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo Tanzania (TAISP) tarehe 11 hadi 14 Mei 2026, mkoani Dodoma ambapo pia wataalam kutoa walikagua maendeleo ya mashamba darasa yaliyoandaliwa na vikundi mbalimbali katika kata na vijiji vya Halmashauri hizo. Ufuatiliaji huo ulilenga kuona namna wakulima wanavyoshiriki kwa vitendo katika mafunzo ya kilimo cha Alizeti kwa kutumia mbinu bora za kilimo. Jumla ya vikundi vya wakulima 32 vyenye jumla ya wakulima 729 kwenye Halmashauri zilizotembelewa vimenufaika na mafunzo ya kilimo cha Alizeti kwa kutumia kanuni bora za kilimo kupitia mashamba darasa yaliyoanzishwa. Akizungumza kuhusu manufaa ya mashamba darasa, mkulima Bw. Idi Omary Nchongoli kutoka kijiji cha Kinyasi, kitongoji cha Kinyasi-Kati, Halmashauri ya Chemba amesema kuwa wakulima wamepata elimu zaidi kuhusu kilimo cha Alizeti kwa kutumia kanuni bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
11 0
1 day ago