LETSPRAYGLOBAL

@letsprayglobal_

🙏 LET’S PRAY GLOBAL A global prayer & worship movement Calling this generation back to God 🔥 Prayer • Worship • Revival 🌍 Impacting nations
Followers
56.2k
Following
327
Account Insight
Score
41.4%
Index
Health Rate
%
Users Ratio
172:1
Weeks posts
Week hii Mungu yupo pamoja nawe. Usiogope wala kufadhaika kwa sababu ya yale unayopitia. Mungu akufanyie wepesi wa kupata majibu ya maombi yako. Amen
114 35
1 month ago
Sikiliza ujumbe kutoka kwa Binti huyu Hakika Utajifunza Jambo #globalgospelimpact #gospeltothenations #fyp #fypage
1,299 49
9 hours ago
Sikiliza ujumbe kutoka kwa pastor @pastor_roseshaboka Hakika urajifunza Jambo #globalgospelimpact #gospeltothenations #fyp #fypage
3,291 198
10 days ago
VANESSA MDEE AJA NA WIMBO WA KUMTUKUZA MUNGU “HOW GREAT THOU ART” 🙏🎶 Aliyekuwa nyota mkubwa wa muziki wa secular nchini Tanzania, Vanessa Mdee ameendelea kuonesha mwelekeo wake mpya wa kumtumikia Mungu baada ya kuachia rasmi toleo maalumu la wimbo wa injili “How Great Thou Art” — unaojulikana kwa Kiswahili kama “Bwana Mungu Nashangaa Kabisa.” ✨ Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vanessa Mdee aliandika ujumbe wenye kugusa wengi akisema: “Let every thing that hath breath praise the LORD. Praise ye the LORD.” — Zaburi 150:6 🙏 Katika ujumbe huo, Vanessa pia aliwataka mashabiki wake kuusikiliza wimbo huo mpya kwa kuandika: “STREAM NOW — HOW GREAT THOU ART.” Kazi hiyo imeandaliwa na wataalamu kutoka Tanzania ambapo Producer alikuwa @nasamwa , huku kazi ya Mixing & Mastering ikifanywa na @mitchell_mike_jr kupitia @mixline_studio . Pia sauti za nyuma (BGV’s) zimehusisha @dr_victoria_joseph pamoja na @neema_balige . 🇹🇿🎹 Hatua hiyo ya Vanessa Mdee imeendelea kuwagusa wengi mitandaoni huku mashabiki wake wakieleza namna anavyozidi kuweka wazi safari yake mpya ya kumwimbia Mungu na kueneza ujumbe wa imani kupitia muziki wa injili. ❤️🙏 #globalgospelimpact #gospeltothenations #fyp #tanzania #eastafrica
1,171 20
10 days ago
FILAMU YA “MONICA” YA UCHE MONTANA YATIKISA AFRIKA KWA VIEWS NYINGI 🎬🔥 Filamu mpya ya Uche Montana yenye jina la Monica imeendelea kushika chati barani Afrika baada ya kuvutia idadi kubwa ya watazamaji na kuwa moja ya filamu zinazozungumziwa zaidi mitandaoni kwa sasa. 🎥🌍 Filamu hiyo imepokea mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa filamu za Kiafrika kutokana na simulizi lake lenye hisia kali, mafunzo ya maisha pamoja na uigizaji uliowagusa wengi. “Monica” inasimulia maisha ya mwanamke anayepitia changamoto nzito za mapenzi, maumivu ya usaliti, vita vya ndani, pamoja na safari ya kutafuta thamani yake halisi katika maisha. Kadri simulizi linavyoendelea, watazamaji hushuhudia namna maamuzi, upendo na majeraha ya zamani yanavyoweza kubadilisha kabisa maisha ya mtu. Mbali na burudani, wengi wameeleza kuwa filamu hiyo imebeba ujumbe mzito kuhusu: * Kujithamini * Kusamehe * Kuvumilia changamoto * Na umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi katika mahusiano Mitandaoni, mashabiki wengi wameendelea kushiriki maoni yao wakisema filamu hiyo imewafundisha mengi kuhusu maisha ya kweli na mahusiano ya kisasa. Swali kubwa ambalo wengi wanaendelea kujiuliza ni: 🗣️ “Wewe umejifunza nini kupitia filamu ya Monica?” Kupanda kwa kasi kwa views za filamu hiyo kunaonesha namna kazi za filamu za Kiafrika zinavyoendelea kukua na kugusa mioyo ya watu wengi duniani. 🎬🔥 #fyp #gospeltothenations #globalgospelimpact #tanzania #fypシ
0 46
10 days ago
Sikiliza ujumbe kutoka kwa pastor @christinemlingi Hakika urajifunza Jambo #globalgospelimpact #gospeltothenations #fyp #fypage
795 23
11 days ago
Sikiliza ujumbe huu from @mwl_emilian_katubayemo #globalgospelimpact #fyp #gospeltothenations #eastafrica #fypă‚·
0 39
11 days ago
NEEMA ILIYOSHINDA HUKUMU: SOMO KUTOKA MAISHA YA TINAH MARKO Katika jamii nyingi, pale kijana au binti anapokosea—hasa kwenye mambo nyeti kama kupata mtoto kabla ya wakati—hukumu huwa ya haraka kuliko huruma. Hivi ndivyo ilivyotokea kwa msichana mmoja aitwaye Tinah Marko. Baada ya kupata mtoto kabla ya wakati uliotarajiwa na jamii, Tinah alikumbana na changamoto kubwa. Wazazi wake walimgeuka, na baba yake alimfukuza nyumbani. Badala ya kupewa nafasi ya kurekebisha maisha yake, alijikuta akihukumiwa na kuachwa peke yake katika kipindi kigumu zaidi cha maisha yake. Lakini katikati ya maumivu hayo, neema ya Mungu ilijidhihirisha kwa namna ya ajabu. Wakati watu walimwona kama aliyeshindwa, Mungu alimwona kama anayehitaji kurejeshwa. Pale ambapo jamii ilifunga milango, Mungu alifungua njia. Tinah hakubaki pale alipoanguka—kwa msaada wa neema ya Mungu, alianza safari ya kuinuka tena. Kisa hiki kinatukumbusha ujumbe muhimu sana wa kiroho: Yesu anatuonya katika Injili ya Mathayo 7:1-2: “Msihukumu, msije mkahukumiwa…” Na pia katika Waraka kwa Wagalatia 6:1 tunaambiwa: “Mtu akipatikana na kosa lolote, mrejezeni kwa roho ya upole.” Haya si maneno tu—ni mwongozo wa maisha. Swali la msingi linabaki: Je, tunakuwa chombo cha hukumu au cha urejesho? Tofauti ya dhambi haimpi mtu mamlaka ya kuhukumu wengine. Badala yake, tunaitwa kuomba, kusimama pamoja na wanaopitia changamoto, na kuonyesha upendo wa Kristo kwa vitendo. Kisa cha Tinah Marko ni ushuhuda hai kwamba neema ya Mungu ni kubwa kuliko makosa ya mwanadamu. Ni ukumbusho kwamba kila mtu anastahili nafasi ya pili—na mara nyingi, mtu anayehitaji zaidi upendo, ndiye anayehukumiwa zaidi. Tuchague kuwa sehemu ya suluhisho, si chanzo cha maumivu. Tuchague kuwa sauti ya faraja, si ya hukumu. Na juu ya yote—tuwape watu neema, kama ambavyo Mungu ametupa sisi. Follow us @tinah_kanel @rooted_and_rising_in_christ @marco_raphel @gospelnationstv Kama umejifunza kitu follow us! #globalgospelimpact #fyp #fypage
24.4k 683
17 days ago
WATU 22 WAOKOKA Kupitia huduma ya uinjilisti wa mtaa kwa mtaa, pamoja na juhudi za kumtangaza Kristo hata ndani ya daladala, Pastor Lenhard ameendelea kugusa maisha ya watu wengi kwa nguvu ya Injili. Katika mwendelezo wa huduma hii, jumla ya watu 146 walipata nafasi ya kusikia Injili ya Yesu Kristo, na kati yao 22 walifanya uamuzi wa kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Aidha, kulikuwa na ushuhuda wa uponyaji kwa baadhi ya walioguswa na nguvu ya Mungu wakati wa huduma hiyo. Hii ni ishara wazi kuwa Injili inaendelea kuleta matumaini, mabadiliko na uzima mpya popote inapohubiriwa. @pastorlenhardkyamba @pastorlenhardkyamba Follow us for more evangelical News @gospelnationstv #fyp #fypage #globalgospelimpact #tanzania #eastafrica
1,116 40
19 days ago
Kuna mengi ya kujifunza Hapa Sikiliza na follow us @gospelnationstv #fyp #globalgospelimpact #eastafrica
3,364 249
20 days ago
🙏 Maombi ya Shukrani: Baba wa mbinguni, nakushukuru kwa zawadi ya siku hii. Asante kwa ulinzi wako, kwa pumzi ya uhai, na kwa baraka zako zilizoonekana na zisizoonekana. Umenisitiri, umeniongoza, na umenipa neema ya kuvuka kila hatua ya leo. Ninakukabidhi usiku wa leo mikononi mwako—ulinde mawazo yetu, miili yetu, na nyumba zetu. Utujalie pumziko lenye amani, tukapate kuamka salama kesho kwa nguvu mpya. Ubariki kazi za mikono yetu, zikazae matunda mema na kuleta mafanikio. Ninakabidhi kesho yangu mikononi mwako, ukatangulie mbele yangu katika kila jambo. Katika jina la Yesu, Amina. 📖 Mstari wa Kusimamia: “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” — 1 Wathesalonike 5:18 Follow @gospeltothenationstz @gospelnationstv @letsprayglobal_ @realministerangela #gospeltothenationsz #globalgospelimpact #eastafrica #gospeltothenations
0 17
20 days ago
Sikiliza kwa makini ujumbe huu From @pastorlenhardkyamba Follow @gospelnationstv #globalgospelimpact #gospeltothenationsz #gospel_talk
0 14
20 days ago