Uanzishwaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani umetajwa kuwa miongoni mwa mikakati muhimu ya Serikali inayowasaidia wakulima kupata uhakika wa soko na bei nzuri za mazao yao.
Wakulima wa zao la kokoa katika Kijiji cha Mashewa, Kata ya Kisiwani wilayani Muheza mkoani Tanga, wamesema mfumo huo umekuwa mkombozi mkubwa kwao kutokana na kusaidia kuongeza thamani ya mazao yao na kupunguza unyonyaji kutoka kwa madalali.
Wamesema kupitia mfumo huo wameanza kupata matumaini ya kuongeza kipato na kuboresha maisha yao kutokana na kuuza mazao kwa bei yenye tija zaidi.
Aidha, wakulima hao wameiomba Serikali kuendelea kuimarisha mfumo huo pamoja na kutoa elimu zaidi kwa wakulima ili waweze kunufaika zaidi na fursa zilizopo katika sekta ya kilimo.
Endelea kuwa karibu na mitandao yetu ya @crowntvtz@crownfmtz na sikiliza 92.1 Mhz au Redio Box/ Garden na kutufuatilia live YOUTUBE channel ya CROWN MEDIA na CROWN TV Chaneli 415 Kwenye Kisimbuzi cha Azam (DISH)
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Mashindano ya msimu wa kumi yamehitimishwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, huku mshindi wa mbio ndefu za kilomita 42 akitokea nchini Kenya.
Mashindano hayo pia yameendelea kudhihirisha ubora wa wanariadha wa Kenya katika mbio mbalimbali, jambo linaloonekana kuwafanya wawe vinara wa kutumia fursa za mashindano ya riadha ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya washiriki waliozungumza baada ya kumalizika kwa mashindano hayo walieleza kufurahishwa na maandalizi ya mbio hizo, wakisema kuwa zimeendelea kuvutia washiriki wengi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Kenya.
Aidha, washiriki hao wamepongeza mafanikio ya wakisisitiza umuhimu wa kuyaendeleza na kuyaboresha zaidi mashindano hayo ili kuongeza mchango wake katika kukuza sekta ya michezo na utalii nchini.
Wakati baadhi ya watu wakitupa vifuu vya nazi mara baada ya kukuna nazi, kwa upande wa John John kutoka Tarafa ya Amani wilayani Muheza, Mkoa wa Tanga, ameona fursa tofauti kupitia mabaki hayo.
‎
‎Kupitia ubunifu wake, ameamua kutumia vifuu vya nazi kutengeneza mapambo na bidhaa mbalimbali za urembo, hatua inayomuwezesha kujipatia kipato huku akiielimisha jamii kuwa hata vitu vinavyoonekana kama uchafu vinaweza kuwa na thamani kubwa endapo vitatumika kwa ubunifu.
‎
‎Mngano Mngano na maelezo zaidi @officialmngano
Endelea kuwa karibu na mitandao yetu ya @crowntvtz@crownfmtz na sikiliza 92.1 Mhz au Redio Box/ Garden na kutufuatilia live YOUTUBE channel ya CROWN MEDIA na CROWN TV Chaneli 415 Kwenye Kisimbuzi cha Azam (DISH)
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inapanga kufanya maboresho katika mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuondoa changamoto zinazowakabili wakulima hususan gharama na usumbufu wa kufuata huduma za maghala yaliyo mbali na maeneo yao ya uzalishaji.
Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnenia, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma katika mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea malalamiko mbalimbali kuhusu utekelezaji wa mfumo huo na kwamba hatua zinaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha mfumo huo unawanufaisha wakulima kama ilivyokusudiwa.
“Maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ni wananchi wasiyafuate maghala, maghala yawafuate wananchi pale walipo,” amesema Waziri Mkuu.
Sikiliza CROWN FM kupitia 92.1 Mhz, Radio Box & Radio Garden tafuta CROWN FM. Tutazame Live kupitia YOUTUBE channel yetu CROWN MEDIA na CROWN TV kwenye Kisimbuzi cha Azam (DISH) ni chaneli namba 415.
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia amekuwa kiongozi ambaye anaonesha kwa vitendo utekelezaji wa yale, ambayo aliahidi na kuwataka viongozi wengine wa ngazi za chini pia kufuata hatua hizo.
Amesema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Dodoma akiwa anazungumza na Wananchi katika Wilaya ya Kondoa.
Sikiliza CROWN FM kupitia 92.1 Mhz, Radio Box & Radio Garden tafuta CROWN FM. Tutazame Live kupitia YOUTUBE channel yetu CROWN MEDIA na CROWN TV kwenye Kisimbuzi cha Azam (DISH) ni chaneli namba 415.
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Majibu ya @sophia_amelowa_official kuhusu kuwasiliana na Lamata ilinaweze kurejea kazini.
Full Interview ya #Sophia ndani ya BATANI na @edsonmaziwa kupitia CROWN TV inapatikana kwenye YouTube yetu ya CROWN MEDIA nenda sasa hivi kaitazame pamoja na vipindi vyetu mbalimbali.
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili mkoani Shinyanga imerejesha tumaini kwa Agatha Julius, mkazi wa kijiji cha Mseki kata ya Bulungwa halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga baada ya kunyang’anywa mirathi na ndugu wa mume wake.
Sikiliza CROWN FM kupitia 92.1 Mhz, Radio Box & Radio Garden tafuta CROWN FM. Tutazame Live kupitia YOUTUBE channel yetu CROWN MEDIA na CROWN TV kwenye Kisimbuzi cha Azam (DISH) ni chaneli namba 415.
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Afisa ardhi Mteule wa Mkoa wa Dodoma Bw. Letare Shoo amesema kwa siku 15 za utekelezaji wa awamu ya pili ya kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Mkoa wa Dodoma, Idara ya ardhi kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria imepokea jumla ya kero 887 za wananchi wenye changamoto za ardhi katika Mkoa huo, wananchi wakimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kampeni hiyo ambayo imeondoa michakato mirefu na gharama kubwa katika kutafuta suluhu mbalimbali za migogoro hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Mei 16, 2026, Bw. Shoo amebainisha kuwa kupitia mashirikiano ya Idara ya ardhi Mkoa wa Dodoma na Wizara ya Katiba na sheria, tayari pia wanashughulikia migogoro mingine 62 iliyosalia, wakidhamiria kuikamilisha kwa siku za karibuni.
Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya Mama Samia umemuwezesha pia mwananchi kupata elimu mbalimbali kuhusu masuala ya ardhi ikiwemo uhamishaji wa umiliki wa vipande vya ardhi huku pia banda hilo likitoa hati za ardhi ndani ya siku moja ambapo kwa siku 15 za utekelezaji wa Kampeni hiyo Mkoani Dodoma, Jumla ya hatimiliki 130 zimetolewa kwa wananchi waliokuwa na nyaraka zote za kuthibitisha uhalali wa umiliki wa ardhi husika.
Kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria kwa awamu ya pili ilianza Mei Mosi 2026 katika Mikoa ya Dodoma na Shinyanga, lengo kubwa likiwa ni kutafuta usuluhishi nje ya mahakama katika migogoro mbalimbali ya kisheria pamoja na kutoa elimu ya sheria mbalimbali, kampeni ikiasisiwa na kufadhiliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kutolewa bure kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kupewa wakili pale shauri lako litakapokuwa linalazimika kwenda Mahakamani.
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Mbunge wa Viti Maalumu, Vyuo na Vyuo Vikuu Tanzania, Regina Malima amewataka wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ukerewe kujiepusha na mambo yanayoweza kuharibu mustakabali wa maisha yao, akisisitiza kuwa hatma ya maisha yao ipo mikononi mwao.
Amesema ni muhimu kwa wahitimu hao kuwa na maadili mema, heshima na kutoacha ndoto zao kufifia kutokana na changamoto mbalimbali, akibainisha kuwa silaha muhimu ya mafanikio ni nidhamu, uaminifu, bidii, ujasiri na kumcha Mungu.
Aidha , Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukerewe, Rebecca Lyanga amesema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 699 inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa walimu wa masomo ya Kiswahili, Historia na Kiingereza kwa kidato cha kwanza hadi cha sita, pamoja na upungufu wa maabara ya fizikia na uzio wa usalama kwa wanafunzi na walimu
Endelea kuwa karibu na mitandao yetu ya @crowntvtz@crownfmtz na sikiliza 92.1 Mhz au Redio Box/ Garden na kutufuatilia live YOUTUBE channel ya CROWN MEDIA na CROWN TV Chaneli 415 Kwenye Kisimbuzi cha Azam (DISH)
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Tanzania pamoja na Urusi zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, kilimo, uwekezaji na usafirishaji ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa mataifa hayo mawili.
Makubaliano hayo yamefikiwa katika Kikao cha Tatu cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Biashara na Uchumi kilichofanyika jijini Arusha.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo amesema ushirikiano huo utafungua masoko mapya ya mazao ya kilimo, kuvutia wawekezaji na kuongeza kasi ya biashara kati ya Tanzania na Urusi.
Aidha, mataifa hayo mawili yamekubaliana pia kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Urusi ili kuimarisha mahusiano ya biashara, utalii na uwekezaji.
Pia, pande hizo zimejadili uwezekano wa kuanzishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Urusi ili kurahisisha biashara na usafiri.
Endelea kuwa karibu na mitandao yetu ya @crowntvtz@crownfmtz na sikiliza 92.1 Mhz au Redio Box/ Garden na kutufuatilia live YOUTUBE channel ya CROWN MEDIA na CROWN TV Chaneli 415 Kwenye Kisimbuzi cha Azam (DISH)
#CrownMedia #HapaNiNyumbani #TupoMwakaWaMbele
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Gairo limepongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wa kuwawezesha walimu wa masomo ya amali kwenda nchini India kwa mafunzo maalumu yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufundisha kwa vitendo na kuwaandaa wanafunzi kujiajiri.
Wilaya ya Gairo ni miongoni mwa wanufaika wa mpango huo ambapo walimu sita wamepata nafasi ya kushiriki mafunzo ya siku 30 nchini India, yaliyojikita katika kuwaongezea ujuzi utakaosaidia kuwahimiza vijana kuendana na mahitaji ya soko la ajira pamoja na mabadiliko ya teknolojia duniani.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Sharifa Nabalang'anya amesema halmashauri itaendelea kuwafuatilia na kuwapa ushirikiano walimu hao baada ya kurejea nchini ili kuhakikisha maarifa waliyojifunza yanakuwa na matokeo chanya kwa vijana na jamii kwa ujumla.