MBEYA GAMING TOURNAMENT IMERUDI RASMI.
Tarehe 6 na 7 mwezi wa sita, Mbeya itakuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya E-Sports pamoja na burudani kupitia Swahili Culture. Wachezaji kutoka maeneo mbalimbali watakutana katika ushindani mkubwa wa gaming wenye kiwango cha juu.
ZAWADI ZA WASHINDI:
Mshindi wa Kwanza β 300,000 TSH
Mshindi wa Pili β 100,000 TSH
Mshindi wa Tatu β 50,000 TSH
TAREHE 6 MWEZI WA SITA
Mbeya Gaming Tournament itaanza rasmi ndani ya Press Lounge ambapo kutakuwa na michezo ya awali, usajili wa mwisho pamoja na ushindani wa gamers kutoka maeneo mbalimbali ya Mbeya.
TAREHE 7 MWEZI WA SITA
Event itaendelea rasmi ndani ya Polos kupitia Swahili Culture, ambapo kutakuwa na maonesho ya ubunifu wa mavazi, sanaa, performances mbalimbali pamoja na hatua za Robo Fainali hadi Fainali za mashindano ya gaming.
Swahili Culture ni jukwaa linalolenga kuonesha ubunifu wa vijana kupitia fashion, sanaa na utamaduni wa Kiswahili katika muonekano wa kisasa unaounganisha burudani na vipaji vya vijana.
Hii ni nafasi ya kuonesha uwezo wako, kushindana na wachezaji bora, kuonesha ubunifu wako na kuwa sehemu ya historia mpya ya gaming na culture ndani ya Mbeya.
Kwa taarifa zaidi kuhusu usajili na ratiba, fuatilia kurasa rasmi za Mbeya Gaming Tournament.