LINDENI AMANI ACHANENI NA WANASIASA WALIOFILISIKA KISERA - KENANI.
Maelfu ya Wananchi wamejitokeza katika mkutano wa Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu. ๐๐ฒ๐ป๐ฎ๐ป๐ถ ๐๐ถ๐ต๐ผ๐ป๐ด๐ผ๐๐, ambao umefanyika katika Kata ya Nyamwaga, Halmashauri ya Tarime Vijijini Mkoani Mara, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani humo leo Mei 16, 2026.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenezi Kenani amehimiza wananchi wa Tarime kulinda ardhi yao ya nyumbani na kuachana na wanasiasa waliofilisika kisera wenye kuchochea machavu na wasio na uzalendo kwa Taifa letu ambao baada ya kuchochea vurugu wenyewe hujificha na familia zao huziamishia nje ya nchi huku akisema hilo ni wazi kuwa wana dhamira mbaya kwa Taifa na sio siasa zenye kuzingatia matakwa ya Watanzania.
โ๐๐ข๐ป๐ช ๐บ๐ข ๐ข๐ฎ๐ข๐ฏ๐ช, ๐ฌ๐ข๐ป๐ช ๐บ๐ข ๐ถ๐ด๐ข๐ญ๐ข๐ฎ๐ข, ๐ฌ๐ถ๐ญ๐ช๐ฏ๐ฅ๐ข ๐ธ๐ข๐ป๐ฆ๐ฆ ๐ธ๐ฆ๐ต๐ถ, ๐ธ๐ข๐ต๐ฐ๐ต๐ฐ ๐ธ๐ฆ๐ต๐ถ, ๐ฎ๐ข๐ฎ๐ข ๐ป๐ฆ๐ต๐ถ ๐ฏ๐ข ๐ง๐ข๐ฎ๐ช๐ญ๐ช๐ข ๐ป๐ฆ๐ต๐ถ ๐ฌ๐ธ๐ข ๐ถ๐ซ๐ถ๐ฎ๐ญ๐ข ๐ฏ๐ช ๐ฌ๐ข๐ป๐ช ๐บ๐ฆ๐ต๐ถ ๐ด๐ช๐ด๐ช ๐ธ๐ข๐ฏ๐ข๐ค๐ฉ๐ช ๐ธ๐ข ๐ฉ๐ข๐ฑ๐ข ๐๐ข๐ณ๐ช๐ฎ๐ฆ, ๐ข๐ด๐ช๐ซ๐ฆ ๐ฎ๐ต๐ถ ๐ฌ๐ถ๐ฌ๐ถ๐ซ๐ข๐ป๐ข ๐ฎ๐ข๐ฏ๐ฆ๐ฏ๐ฐ ๐บ๐ข ๐ค๐ฉ๐ถ๐ฌ๐ช, ๐ฑ๐ข๐ฌ๐ช๐ฉ๐ข๐ณ๐ช๐ฃ๐ช๐ฌ๐ข ๐ฉ๐ข๐ฑ๐ข ๐ธ๐ข๐ป๐ฆ๐ฆ ๐ธ๐ฆ๐ฏ๐ถ ๐ฉ๐ข๐ธ๐ข๐ฏ๐ข ๐ฑ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ฌ๐ช๐ฎ๐ฃ๐ช๐ญ๐ช๐ข, ๐ธ๐ข ๐ฑ๐ช๐ญ๐ช ๐ฏ๐ช ๐ธ๐ข๐ต๐ฐ๐ต๐ฐ ๐ธ๐ฆ๐ฏ๐ถ ๐ธ๐ข๐ฅ๐ฐ๐จ๐ฐ ๐ฉ๐ข๐ธ๐ข๐ฏ๐ข ๐ฑ๐ข ๐ฌ๐ธ๐ฆ๐ฏ๐ฅ๐ข ๐ฏ๐ข ๐ธ๐ข ๐ต๐ข๐ต๐ถ ๐ฏ๐ช ๐ฎ๐ข๐ฎ๐ข ๐ป๐ฆ๐ฏ๐ถ ๐ฉ๐ข๐ธ๐ข๐ฏ๐ข ๐ถ๐ธ๐ฆ๐ป๐ฐ ๐ธ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ซ๐ช๐ต๐ฆ๐ต๐ฆ๐ข, ๐ญ๐ช๐ฏ๐ฅ๐ฆ๐ฏ๐ช ๐๐ข๐ณ๐ช๐ฎ๐ฆ ๐บ๐ฆ๐ฏ๐ถโ ๐๐๐ฃ๐๐ฃ๐.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
WASIRA AKONGA NYOYO ZA WANANCHI KIGOMA MJINI
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewahutubia na kukonga nyoyo za mamia ya wana CCM na wananchi wa Kigoma mjini huku akiwataka kudumisha amani, umoja na mshikamano.
Wasira amewahutubia wananchi hao leo Mei 16, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kawawa uliopo Kigoma mjini akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
== ==
๐ ๐๐๐ก๐๐๐๐๐ข ๐ฌ๐ ๐ ๐ญ๐๐ ๐จ๐ก๐ ๐ฌ๐๐ง๐๐๐๐ง๐ช๐ ๐ก๐ ๐๐๐ข๐ก๐๐ข๐ญ๐ ๐๐ก๐๐ฌ๐๐ง๐ข๐๐๐ก๐ ๐ก๐ ๐๐๐ ๐ฃ๐๐๐๐ - ๐๐๐ฉ๐จ
โ๐๐ป๐ช๐ฎ๐ถ๐ฏ๐ช ๐ฎ๐ฏ๐ข๐ต๐ข๐ฌ๐ข ๐ฎ๐ข๐ฆ๐ฏ๐ฅ๐ฆ๐ญ๐ฆ๐ฐ ๐ฆ๐ฏ๐ฅ๐ฆ๐ญ๐ฆ๐ท๐ถ, ๐ฎ๐ฏ๐ข๐ต๐ข๐ฌ๐ข ๐ถ๐ธ๐ข๐ซ๐ช๐ฃ๐ช๐ฌ๐ข๐ซ๐ช, ๐ฎ๐ฏ๐ข๐ต๐ข๐ฌ๐ข ๐ฌ๐ช๐ฐ๐ฏ๐จ๐ฐ๐ป๐ช ๐ข๐ฏ๐ข๐บ๐ฆ๐ซ๐ข๐ญ๐ช ๐ธ๐ข๐ฏ๐ข๐ฏ๐ค๐ฉ๐ช, ๐ฎ๐ฏ๐ข๐ต๐ข๐ฌ๐ข ๐ฎ๐ต๐ถ ๐ข๐ด๐ช๐บ๐ฆ ๐ฏ๐ข ๐ฎ๐ข๐ฌ๐ถ๐ถ ๐ข๐ฎ๐ฃ๐ข๐บ๐ฆ ๐ฎ๐ต๐ข๐ฎ๐ต๐ถ๐ฎ๐ข ๐ฏ๐ข ๐ข๐ฌ๐ข๐ด๐ฆ๐ฎ๐ข ๐ฌ๐ธ๐ข ๐ฏ๐ช๐ข๐ฃ๐ข ๐บ๐ฆ๐ฏ๐ถ ๐ฌ๐ถ๐ญ๐ฆ ๐๐ข๐ญ๐ฎ๐ข๐ด๐ฉ๐ข๐ถ๐ณ๐ช ๐ฃ๐ข๐ด๐ช ๐ฎ๐ต๐ถ ๐ฉ๐ถ๐บ๐ฐ ๐ด๐ช ๐ฎ๐ธ๐ฆ๐ฏ๐จ๐ช๐ฏ๐ฆ ๐ฃ๐ข๐ญ๐ช ๐ฏ๐ช ๐๐๐๐ ๐๐๐ก๐ช๐ข ๐๐๐จ๐๐ฃ๐๐ ๐ข๐ฏ๐ข๐บ๐ฆ๐ต๐ฐ๐ฌ๐ข๐ฏ๐ข ๐ฏ๐ข ๐๐๐, ๐๐ค๐ฉ๐ข๐จ๐ถ๐ฆ๐ฏ๐ช โ
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Idara ya Oganaizesheni Ndugu. ๐๐๐๐ฎ ๐๐ฎ๐ท๐ถ ๐จ๐๐๐ถ ๐๐ฎ๐๐ (๐ ๐ก๐๐) leo tarehe 16 Mei 2026 wakati akiongoza jahazi akiwa Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Udiwani katika Kata ya Mzimuni iliyopo Wilayani Kinondoni Jijini Dar es salaam katika Viwanja vya Muhuto.
Gavu amewaeleza wananchi kuwa kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป inatokana na usambamba uliopo wa maelewano mazuri ya viongozi wenye kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2025/26) na nianya kweli ya kuleta maendeleo endelevu ambapo amesema usambamba huo unamaanisha uwepo wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa anayetokana na CCM, Diwani kutoka CCM, Mbunge na Rais ndio maana kazi inakuwa inafanyika kwa urahisi kwakuwa hakuwezi kuwa na upinzani usiojali maendeleo ya wananchi.
Katika uzinduzi huo, Maelfu ya wananchi wamejitokeza kwa wingi kusikiliza sera za CCM na kuonesha ishara tosha ya kuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya pamoja wameshiriki katika uzinduzi huo huku Wanachama, Wadau na Wananchi kwa ujumla wakionesha kuunga mkono sera za CCM na kuahidi kumpa kura za ndio Mgombea Ndugu. Saidi Salum Masanga.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
MKUTANO wa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, umevutia mamia ya wananchi katika Kata ya Nyamwaga, Halmashauri ya Tarime Vijijini mkoani Mara
Kihongosi ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne mkoani humo leo Mei 16, 2026 amefika katika Halmashauri hiyo na kukagua uhai wa chama kupitia mashina, kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.
Kiongozi huyo ambaye amekuwa na namna tofauti katika mikutano yake akivutia namba kubwa ya wanachama na wananchi ambao si wanachama kuhudhuria mikutano hususani katika Jimbo hilo la Tarime Vijijini ambalo liliwahi kuwa la upinzani
Mbali na kiongozi huyo kuendesha mikutano hiyo kwa namna yake tofauti ya kusikiliza hoja na mistari yake ameendelea kuvutia wanachama wa vyama vingine vya upinzani kuhamia CCM na miongoni mwa watu hao ni Mwenyekiti wa Chadema Tawi la Sokoni Sirari, Mohabe Manga Bunyige
TARIME YAFURIKA MKUTANO WA MWENEZI WA CCM KOMREDI KENANI KIHONGOSI
Mwenezi anaendelea na ziara Mkoa wa Mara Kesho atakua Wilaya ya Bunda kuendelea na ziara ya kuimarisha Chama kukagua miradi na kusikiliza wananchi
KIHONGOSI: โMSIRUHUSU SIASA KUINGIA KWENYE MAENDELEOโ
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amewataka wananchi kutokuruhusu siasa kuingia katika maendeleo akiwasisitiza walinde miundombinu inayopelekwa na serikali.
Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 16,2026 alipotembelea na kukagua mradi wa shule ya Sekondari ya Nyasarisho Kata ya Binagi Tarime Vijijini mkoani Mara, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mkoa huo.
Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Kihongosi amewasisitiza wananchi kulinda miundombinu inayopelekwa na serikali katika maeneo yao kwani yanapelekwa kwa manufaa yao wenyewe, hivyo wasiiharibu wala kuichoma kutokana na uchochezi wa kisiasa.
Kihongosi amesema siasa ifanyike lakini isiingie katika maendeleo ya nchi, akisisitiza kuwa mtu mwerevu analinda nyumbani kwao lakini mtu ambaye si mwerevu anaharibu nyumbani kwao.
Amewataka wananchi kutokuruhusu siasa kuingia katika maendeleo, akiwasisitiza walinde miundombinu na miradi ya maendeleo wanayopelekewa ikiwemo shule hiyo kwani ni kwa manufaa yao wenyewe.
โSasa siasa isiingie kwenye maendeleo, siasa ifanyike maendeleo ya nchi yasonge mbele watu wa Tarime msipolinda miundombinu yenu hakuna wakuwalindia, shule ikichomwa maana yake watoto wote warudi nyumbani hiyo ni hasara kwa wazazi na wananchi usika,โ amesisitiza.
Akitoa taarifa fupi ya mradi huo Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyasarisho, Paschal Sobu amesema shule hiyo ni ya mchanganyiko na ina vijana wa kidato cha kwanza hadi cha sita, huku kidato cha kwanza hadi cha nne ni wavulana na wasichana lakini kidato cha tano na sita ni wavulana tu.
Amesema shule hiyo imejengwa kwa kiasi cha Sh bilioni 1.6 ambapo Sh bilioni moja zimetoka katika serikali kuu na zaidi ya Sh milioni 600 zimetoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri ya Tarime.
โTunayo miuondombinu kama ulivyoikagua yako madarasa 13, ofisi tano, lipo jengo la utawala eneo ulilosimama, maabara za kisasa ulizoziona, ya Kemia na baolojia lakini tunabwalo la chakula, jiko la ndani ambayo yanatumia nishati safi,โamesema Sobu.
WASIRA AFICHUA SIRI CCM KUJIFANYIA TATHMINI.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutaka Chama kijifanyie tathmini, unalenga kupata viongozi bora na kushughulikia kikamilifu changamoto za Watanzania.
Amesema wakati wana CCM wakielekea katika uchaguzi mkuu wa Chama, ni vyema kila mmoja kujitathmini kabla ya kuomba nafasi ya uongozi kuhakikisha ana sifa zikiwemo za kimaadili.
Wasira aliyasema hayo jana mkoani Kigoma alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM kwa Nyakati tofauti katika wilayani Buhigwe, Kasulu pamoja na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa, akiwa katika ziara ya kichama mkoani humo.
Alisisitiza viongozi na wanachama wa CCM kuijua na kuizingatia Katiba ya Chama, kanuni na miongozo inayoongoza uendeshaji wa Chama.
โSiku hizi tunasema kuna njia kuu na mchepuko, njia kuu ya chama hiki imeandikwa katika hivi vitabu (Katiba, kanuni na miongozo) mchepuko ni tabia tunayoendesha nayo ambayo inapingana na vitabu, kwa hiyo tumechepuka tunataka kurudi njia kuu. Chama kinachoundwa na katiba hii kina madhumuni,malengo,Sifa za mwanachama, masharti ya kiongozi, wanachama, katiba na Kanuni.
โsifa za uongozi, hizi zipo katika kitabu kinaitwa kanuni za uchaguzi ndani ya CCM, inasema sifa ya kwanza kiongozi wa Chama akinai maadili ya Chama kwa maana ya kwamba ayajue na ayaishi na asiwe mtu wa kuyumbayumba katika mambo ya msingi.
โUnajua unaweza ukachagua kiongozi leo ana hili kesho ana lile sasa unaweza kumuuliza wewe hasa unasimamia nini maana yale uliyoyakubali jana ndiyo unayoyapinga keshoโฆwewe nawe ni mwanachama hatari na mwanachama wa namna ile anaweza akakidhulumu chama chenyewe.
Makamu Mwenyekiti Wasira alisisitiza kiongozi anapaswa kuwa na uwezo wa kazi anayoiomba.
WASIRA AFICHUA SIRI CCM KUJIFANYIA TATHMINI.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutaka Chama kijifanyie tathmini, unalenga kupata viongozi bora na kushughulikia kikamilifu changamoto za Watanzania.
Amesema wakati wana CCM wakielekea katika uchaguzi mkuu wa Chama, ni vyema kila mmoja kujitathmini kabla ya kuomba nafasi ya uongozi kuhakikisha ana sifa zikiwemo za kimaadili.
Wasira aliyasema hayo jana mkoani Kigoma alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM kwa Nyakati tofauti katika wilayani Buhigwe, Kasulu pamoja na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa, akiwa katika ziara ya kichama mkoani humo.
Alisisitiza viongozi na wanachama wa CCM kuijua na kuizingatia Katiba ya Chama, kanuni na miongozo inayoongoza uendeshaji wa Chama.
DKT.MIGIRO AIMARISHA USHIRIKIANO KIMATAIFA NA MABALOZI WA CUBA, VIETNAM, NA UN
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Asha-Rose Migiro, kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo ya makao makuu CCM, Lumumba, jijini Dar es salaam.
Mabalozi hao ni Mheshimiwa Yordenis Despaigne Vera, Balozi wa Jamhuri ya Cuba na Mheshimiwa Vu Thanh Huyen, Balozi wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, wote wenye makaazi yao nchini Tanzania.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya CCM na vyama rafiki vya CPCโCuba na CPVโViet Nam, hususan katika maeneo ya uongozi, mshikamano wa vyama vya siasa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Migiro, alifanya mazungumzo na Mheshimiwa Susan Ngongi Namondo, Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, ambapo walijadiliana vipaumbele vya maendeleo ya jamii katika utekelezaji wa baadhi ya maeneo yaliyomo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025โ2030 ambayo yanawiana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na Malengo ya Maendeleo ya Kimataifa (SDGs).
VIONGOZI WAONYWA DHIDI YA KIBURI CHA MADARAKA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amewataka viongozi hususani vijana walioko kwenye nafasi za uongozi,kuacha kiburi cha madaraka,na badala yake wajifunze na kufuata msingi uliojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwani uongozi si kiburi wala majivuno ya madaraka.
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 15,2026 alipozuru na kufanya ibada fupi katika kaburi la hayati Mwl Nyerere katika Wilaya ya Butiama mkoani Mara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Akizungumza baada ya ibada hiyo Kihongosi amesema viongozi wanapaswa kuishi kwa kufuata misingi ya Mwl Nyerere, kwani aliacha urithi wa uzalendo, upendo na umoja kwa kupiga vita ukabila, udini na ukanda na ndiyo maana leo Tanzania inaendelea kuwa taifa lenye mshikamano.
Amesema kutoka ana msingi huo ambao ndio urithi aliouacha viongozi wanapaswa kujifunza kwake kuwa uongozi si kiburi wala majivuno ya madaraka bali kiongozi bora ni yule anayewaunganisha watu, anayeprnda nchi yake na anayewatumia wananchi kwa unyeyekevu.
โviongozi hasa vijana nikiwepo mimi tunapaswa kujifunza kutoka kwake uongozi si kiburi wala majivuno ya madaraka, kiongozi bora ni yule anayewaunganisha watu, anayependa nchi yake na anayewatumikia wananchi kwa unyenyekevu kama alivyofanya Mwalimu Nyerere,โ amesisitiza Kihongosi.
Ameongeza akisisitiza kuwa ni muhimu kwa vijana waliopewa dhamana ya uongozi kuepuka kiburi cha madaraka na badala yake kujifunza kutoka kwa wazee waliotutangulia.
KIHONGOSI: MAAMUZI YA VIKAO YAHESHIMIWE
TARIME: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi wa chama ni vikao, hivyo maamuzi yanayotolewa katika vikao yanapaswa kuheshimiwa.
Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 15,2026 alipotembelea na kuhudhuria Shina namba tatu Tawi la Buhemba Kata ya Bomani jimbo la Tarime Mjini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Mara.
Kihongosi alisema watu wanapaswa kuheshimu maamuzi ya vikao kwa sababu ndipo watu wanapokaa kufanya mipango na kukubaliana hivyo maamuzi ya vikao ndiyo maamuzi ya chama.
โKiongozi aliyeiva itikadi ya CCM maamuzi ya mwisho ya vikao ndiyo maamuzi ya chama na wanachama hao, vyama vyetu au chama chetu tunasema msingi wa chama ni vikao, kwenye vikao tunakaa, tunapanga tunakubaliana tunasonga mbele,โ amesema Kihongosi.
Kihongosi ameongeza kuwa kazi ya chama itafanywa na wanachama watiifu na wazalendo wa chama, hivyo ukiona kuna mtu ana mambo yake mengine huyo si mwanachama aliyoiva itikadi ya CCM.
Katika hatua nyingine amewataka viongozi wa CCM walinde chama kwa sababu chama ndicho kimewapa heshima ya uongozi, hivyo waachane na mambo ambayo yanaharibu chama kwahiyo lazima tulinde maslahi yetu mapana yawe ndani ya chama.
โJambo ninalopenda kulisisitiza hapa katika mkutano wetu huu wa ndani naomba wana CCM tukipende chama kuliko kupenda watu ndani ya chama, maana yake chama kwanza watu baadaye,โ amesisitiza Kihongosi.
โNinacho maanisha hapa Tarime tunahitaji, umoja upendo na mshikamano ili kuwa na CCM imara na madhubuti lazima kama kuna makundi yafe, kama kuna mambo hayaeleweki yamalizwe ili Tarime Chama Cha Mapinduzi kiwe Imaraโ.