Timu bora kwenye michuano ya veteran arusha @arushadfa arusha coaches ndio wamebeba back to back mashindano haya
#coaches #arusha #tanzania #sports #football
MABINGWA Wa Ligi ya Wilaya Arusha Mjini 2025 @ctido_sports_academy Ligi ambayo imechezwa na Vijana wa Umri chini ya Miaka 17. Baada ya kuongoza Group B kucheza Nusu Fainali na Arydo Academy na kupata Ushindi wa Matuta na Kuelekea Fainali dhidi ya Timu Ngumu ya Uhasibu Academy na Kuibuka na Ushindi wa Goli Mbili kwa Moja @mirambo81@fikiri.elias@itaelialfred@tanfootball #paliponautaliimpiralazimauchezwe
Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arusha (ADFA) kinapenda kuwataarifu wapenda soka na wadau wote wa michezo kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi uliofanyika leo, tarehe 18/04/2026, umehitimishwa kwa mafanikio makubwa, amani na maelewano.
Kamati ya Uchaguzi ilisimamia kikamilifu zoezi la upigaji kura kwa uwazi na haki, na hatimaye kuwatangaza viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza ADFA katika kipindi kijacho.
Matokeo ya Uchaguzi ni kama ifuatavyo: • Mwenyekiti: Athuman Mhando • Makamu Mwenyekiti: Mwansasu Kabarika • Katibu Mkuu: Fredrick Limo
Wajumbe: • Josephat Chacha • Justin Mollel • Phinius Nyamandege • Upendo Mwakasata (Ameteuliwa) • Samwel Sumwa (Ameteuliwa)
Chama cha Mpira Arusha Mjini kinawapongeza viongozi wote waliochaguliwa na kuwatakia utekelezaji wenye mafanikio, uwajibikaji na uongozi bora katika kuendeleza soka la Arusha Mjini.
Pia tunawashukuru wanachama na wadau wote kwa ushirikiano wao uliofanikisha uchaguzi huu kwa amani na ustaarabu
Draw rasmi ya makundi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) PAMOJA 2027 itafanyika Jumanne, Mei 19, 2026, jijini Cairo, Misri. Timu 48 zitagawanywa kwenye makundi 12, huku wenyeji Tanzania, Kenya, na Uganda wakifuzu moja kwa moja na kuwekwa kwenye makundi hayo kwa ajili ya maandalizi.
Hongera Serengeti Boys Kwa Kufuzu Kombe la Dunia 2026 Qatar
Serengeti Boys Wamekata tickets hii mara baada ya kuibuka na ushindi wa goal 0-3 dhidi ya team ya Taifa ya Angola 🇦🇴
@serengetiboystz
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira Wa Miguu Wilaya ya Arusha Mjini Bwana Fredrick Limo akizungumza na Kamati pamoja na Wanachama waliohudhuria mkutano hapo jana, ambapo alieleza kuwa kigezo cha kwanza cha kuitambulisha na kuikuza soka la Arusha Mjini ni nidhamu pamoja na kuwa na kiwango kikubwa cha utimamu wa mwili (High Fitness) kwa wachezaji.
Aidha, aligusia umuhimu wa walimu na makocha kuendelea kujifunza na kuongeza elimu ya ukocha ili Arusha iweze kuwa na idadi kubwa ya walimu wa soka wenye viwango bora na uwezo mkubwa wa kuendeleza vipaji vya vijana.
Kikao kazi cha mustakabali wa sura mpya ya soka la Arusha kimefanyika leo kikiongozwa na viongozi wa Chama Cha Mpira Wa Miguu Wilaya ya Arusha Mjini.
Waliohudhuria ni Makamu Mwenyekiti Bwana Mwansasu Kabalika, Katibu Mkuu Bwana Fredrick Limo, Mjumbe wa Kamati Bwana Samweli Sumwa pamoja na Chacha Chenco.
Kikao hicho kimejikita katika kujadili maendeleo ya soka, uimara wa mashindano na kuweka mikakati ya kuleta mabadiliko chanya katika mpira wa miguu wa Arusha Mjini.